January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

Alikuwa anapima upepo, alifikiri wataalamu ni wa kukoromewa na kila mtu.
Amekuta maji marefu ameanza kugeuza kila lugha.
Usiige kunya kwa tembo...Mambo ya kukoromea watu wakaogopa aliwaweza Mwendazake tu.
 
Am strongly opposed Tanesco kujiendesha kibiashara kabla haijawafikishia watanzania wengi umeme....unapojiendesha kibiashara kuna mahali utaacha kupeleka umeme kwa sababu hakuna returns.
 
Waziri wa Nishati January Makamba ametembelea ofisi za Tanesco na kulipongeza shirika hilo kwa kufikisha wateja 3.2 millioni ndani ya miaka 5 iliyopita.

Wanaoliwezesha kukusanya zaidi ya trillioni 2 kwa mwezi na kulifanya kuwa shirika pekee linalokusanya fedha nyingi nchini.

Makamba ametoa wiki mbili kwa shirika hilo kuacha kukata umeme la sivyo ataanza kuwafukuza kazi mameneja wote wazembe wote wanaokata umeme.

--
makamba-pic-data.jpg
Waziri wa Nishati, January Makamba ametoa wiki mbili kuhakikisha hakuna tatizo la kukatika umeme nchini Tanzania.
Leo Ijumaa Septemba 17, 2021 Makamba amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya malalamiko ya wananchi kuongezeka kuhusu kukatika kwa umeme.

Makamba amesema atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake na malalamiko ya kukatika kwa umeme yakiendelea kujitokeza, wahusika wote watachukuliwa hatua.

"Ndani ya wiki mbili sitaki kusikia kukatika kwa umeme nikisikia kuna malalamiko nitachukua hatua Kwa wahusika walioshindwa kutekeleza wajibu wao," alisema Makamba.

Alisema wanahitaji Shirika hilo lijiendeshe kibiashara, kisasa ambapo mabadiliko yenye tija yataongeza ufanisi na mapato yataongezeka.

"Shirika lina wateja wa mita 3.2 milioni wanakusanya zaidi ya Sh2 tirioni na hakuna Shirika lolote hapa nchini linalotengeneza fedha hizo, hivyo wateja wanatakiwa kuongezeka ili Shirika liweze kujiendesha" amesema

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji wa Umeme, Pakaya Mtimakaya amesema wameyapokea maagizo hayo na watayafanyia kazi.
 
Subiri Stigler ikamalike ndio utapata umeme wa kudumu na mwingine wa kuuza nje ya nchi
 
3.2 million customers & 2 trillions per month. Its about time that such achievements should reflect the quality of services offered including further expansion to accommodate more newer customers.
 
Aisee! Yeye si ndio alisema amri hizi ziliwafanya Tanesco washindwe kufanya ukarabati ambao sasa hivi unafanyika na ndio sababu ya umeme kukatika hovyo?!! Ama kweli mwanasiasa akikwambia sasa hivi ni usiku toka nje kahakikishe.
 
Subiri Stigler ikamalike ndio utapata umeme wa kudumu na mwingine wa kuuza nje ya nchi
Umeongea mwenyewe, unacheka mwenyewe na hizo emoj, we sio mzima itakuwa,

Sasa nn cha kuchekesha hapo shoga angu
 
Guardiola(January) ni MTU wa sinema Sana inakuaje waziri husika unashindwa kujua tatizo la kukatika umeme?
Huyu jamaa ni waziri wa michongo Tu
 
Kati ya hizo trillion 2, ni ngapi zinalipwa Songas, na kiasi gani kinatumika kununulia gas? Si ajabu hata mishahara ya watumishi ni ruzuku kutoka Serikalini.
 
3.2 million customers & 2 trillions per month. Its about time that such achievements should reflect the quality of services offered including further expansion to accommodate more newer customers.
ukute makusanyo kwa mwezi ni 2T na matumizi kwa mwezi ni 1.9T, hii nchi anything is possible...
 
Kweli zama zimebadilika... yaani umeme unavyokatikakatika hivi na bado watu mnapongezana... Hii habari enzi zile ingehusu kutumbuliwa
 
Kweli zama zimebadilika... yaani umeme unavyokatikakatika hivi na bado watu mnapongezana... Hii habari enzi zile ingehusu kutumbuliwa
habari yenyewe ya mwezi September kabla wahindi hawajampelekea dili la kuuza majenereta saizi tuko November
 
Kati ya hizo trillion 2, ni ngapi zinalipwa Songas, na kiasi gani kinatumika kununulia gas? Si ajabu hata mishahara ya watumishi ni ruzuku kutoka Serikalini.
wanakusany trillion 1.8 to 2 trioni kwa mwaka siyo kwa mwezi
 
Maneno mengi utekelezaji mdogo. Hapa wamekata umeme bunju toja asubuhi na nlikuwa na kazi kibao.
 
Aisee! Yeye si ndio alisema amri hizi ziliwafanya Tanesco washindwe kufanya ukarabati ambao sasa hivi unafanyika na ndio sababu ya umeme kukatika hovyo?!! Ama kweli mwanasiasa akikwambia sasa hivi ni usiku toka nje kahakikishe.
Loh! Mithili ya kinyonga kubadilika rangi kufuatana na mazingira.
 
Back
Top Bottom