DENLSON
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 944
- 1,253
Ni ajabu sana kwamba kwa miaka 5 hatuwahi kuwa na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara kama ilivyo sasa. Wote tunajua umeme ulikuwa ukikatika lakini sio kwa kasi hii iliyopo sasa hasa baada ya uteuzi wa January Makamba kama Waziri wa Nishati.
Uteuzi wako ulifuatiwa na uamuzi wa wewe kuvunja bodi ya Tanesco kisha kuingia mkataba wa bilioni 63 za kitanzania kwa madai ya kuboresha mfumo, mfumo ambao wewe hukuwahi kujua mapungufu yake wala uimara wake ila ghafla ndani ya mwezi mmoja tu tokea uingie ofisini unavunja bodi na kuingia mkataba wa mabilioni ya shilingi na kibaya zaidi hatua hizo zilifuatiwa na ukatikaji wa umeme nchi nzima.
Tanesco wakatoka na kauli kwamba hakuna mgao bali ni magengenezo ya kawaida, Waziri ukasema ni kwa wiki mbili tu leo ni zaidi ya miezi mitatu umeme haumalizi siku bila kukata, Je Mh January uliteuliwa ili ukasimamie zoezi la ukataji wa umeme?