January Makamba: Sikuhusika katika mchakato wa utungwaji wa Sheria ya makosa ya Mitandao kwa sababu nilikuwa Naibu Waziri Mawasiliano

January asitake kujivua hii dhambi, yeye alikuwa anaishabikia huku akijua hiyo sheria haina tofauti na sheria walizokuwa wanapitisha wazungu enzi za apartheid. Kwa maneno haya ni udhibitisho kile ambacho huwa tunasema kwamba bunge huwa halitungi sheria bali ni rubber stamp ya kupitisha kila takwa la serikali. Na ukijaribu kuangalia ni utashi wa rais aliye madarakani ndio hutungwa kuwa sheria, na huko bunge hupitishwa tu kwani nusu ya wabunge wamepatikana kwa wizi wa kura hivyo hawana ubavu wa kukataa chochote.
 
Mkuu tusiwakejeli haya ni majembe na Safari hii inabidi kuunganisha nguvu kuna mabadiliko makubwa yanakuja mimi nahisi watu wanajipanga ndani ya CCM na sisi tujipange nje halafu kwa pamoja tushambulie.
Pamoja mkuu
 
Wengine wanaitumia bandari kutoa baadhi ya gharama kwa mizigo inayoingia wanatamani wafute hata kodi kwa mizigo wanapoingiza wafanyabiashara ili wapate kura 2020 wanashindwa aisee kumbe huwa wanajua wanawaumiza Wananchi ni viburi vyao tuu...
 
Ni wakati wa #kutubu kila mtu atatubu.......
😎😎.....😛😛😛😛

"Kuhusu Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Mwaka 2015, Sikuhusika katika mchakato wa utungwaji kwa sababu Nlikuwa Naibu Waziri Mawasiliano, na mchakato ulihusisha wataalamu wa wizara, makatibu wakuu, mawaziri, Mimi sikuwa miongoni mwa makundi hayo."

-January Makamba
Kuna aliyemuuliza?
 
Back
Top Bottom