January Makamba: Sikuhusika katika mchakato wa utungwaji wa Sheria ya makosa ya Mitandao kwa sababu nilikuwa Naibu Waziri Mawasiliano

January asitake kujivua hii dhambi, yeye alikuwa anaishabikia huku akijua hiyo sheria haina tofauti na sheria walizokuwa wanapitisha wazungu enzi za apartheid. Kwa maneno haya ni udhibitisho kile ambacho huwa tunasema kwamba bunge huwa halitungi sheria bali ni rubber stamp ya kupitisha kila takwa la serikali. Na ukijaribu kuangalia ni utashi wa rais aliye madarakani ndio hutungwa kuwa sheria, na huko bunge hupitishwa tu kwani nusu ya wabunge wamepatikana kwa wizi wa kura hivyo hawana ubavu wa kukataa chochote.
Mkuu umemaliza kila kitu. Kwa upande wa ccm Wabunge wao ni zero.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kuhusu Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Mwaka 2015, Sikuhusika katika mchakato wa utungwaji kwa sababu Nlikuwa Naibu Waziri Mawasiliano, na mchakato ulihusisha wataalamu wa wizara, makatibu wakuu, mawaziri, Mimi sikuwa miongoni mwa makundi hayo."

-January Makamba
Vipi pale bungeni wakati spika anauliza walioafiki na wasio afiki yeye alikuwa upande gani?
 
  1. Uwajibikaji wa pamoja haukubaliani na utetezi wake. Kama kweli kasema hivyo, basi kuwajibishwa kunamhusu.
 
Mkuu tusiwakejeli haya ni majembe na Safari hii inabidi kuunganisha nguvu kuna mabadiliko makubwa yanakuja mimi nahisi watu wanajipanga ndani ya CCM na sisi tujipange nje halafu kwa pamoja tushambulie.
Japokuwa hawa ni majembe ya matumbo yao na wanafiki but hapa tulipofikia itabidi tuunge Mkono njia au nyenzo yoyote kutuondolea hili balaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu yaani 2020 upinzani wakipata mtu anayeweza kugongelea misumari vizuri kampeni zitakua nyepesi sana!
Bunge laivu
sheria ya mitandao
ajira
watumishi kutoongezewa ajira
etc...

Polisi kubambikizia raia makosa/kesi
 
Mkuu tusiwakejeli haya ni majembe na Safari hii inabidi kuunganisha nguvu kuna mabadiliko makubwa yanakuja mimi nahisi watu wanajipanga ndani ya CCM na sisi tujipange nje halafu kwa pamoja tushambulie.

Wanasiasa sio wa kuwaamini kirahisi rahisi tu ,hasa hawa ambao wapo ktk Madaraka wakifakamia Keki ya Taifa 🙄🙄...
 
Kuna nini tena? Mwigulu naye juzi juzi kasema yule aliyemtolea bastola nape hakusema kama sio askari alisema sio polisi,haya nape naye bunge live sio yeye na yeye marope kaja!
 
Screenshot_2019-02-20-10-25-22.png


Wametokea wanachama walimuweka Magufuli madarakani na kuyakana mambo mazuri yaliyofanywa na chama na serikali wao wakiwa watu wazito katika maamuzi. Alikuja Mwigulu,amekuja Nape na leo Makamba.

Kuna nini kinaendelea huko VUTA-NKUVUTE ?
 
View attachment 1027114

Wametokea wanachama walimuweka Magufuli madarakani na kuyakana mambo mazuri yaliyofanywa na chama na serikali wao wakiwa watu wazito katika maamuzi. Alikuja Mwigulu,amekuja Nape na leo Makamba.

Kuna nini kinaendelea huko VUTA-NKUVUTE ?
Mwigulu baada ya kufanya mahojiano yale akapata ajali ya punda !
 
Back
Top Bottom