Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,489
- 51,070
Sasa hivi TANESCO wanakata umeme, hawatoi taarifa, biashara na shughuli zetu zinasimama. Huu ujinga utaisha lini nchi hii?
Mmeturushia zigo la sisi watumiaji umeme kulipa kodi ya majengo, halafu mnatuambia sisi tumalizane na wenye nyumba HALAFU bado hata umeme huo mnaukatakata. Hivi nyie mnajitambua kweli, mnajielewa? - Mnatutia hasira sana aisee
Tunajua wanasiasa mna majumba ya kupangisha kedekede, kwa hiyo mnanufaika kwa kodi kulipwa na mpangaji kuliko nyie ndo maana hata bungeni hamkupambana kumtetea mpangaji kwa sababu hii sheria inawalinda matajiri na kumuumiza masikini! , maana kwa mijumba yenu mingi mnayomiliki kwa mwaka mnatakiwa kulipa hela ndefu.
Mimi naamini kama kweli mkitaka Mwenye nyumba alipe mnaweza maana mna uwezo wa kujua namba za simu za wenye nyumba, mnaweza kuwakata wao direct kupitia miamala wanayofanya au mnaweza kujua benki account zao na mkawakata kwenye miamala yao badala ya kuja kutukata sisi Wapangaji.
Yaani mgekuwa na lengo la kumlinda mpangaji mngeweza kuweka hata sheria ya kumlinda mpangaji lakini hamjafanya hivyo.
Waziri tunataka umeme wa uhakika, haya mambo ya kukatikakatika yanakera sana.