January makamba ni mwepesi mno!cdm inatakiwa kujipanga tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January makamba ni mwepesi mno!cdm inatakiwa kujipanga tu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Apr 5, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot] Natambua kwamba Mwanasiasa kama January Makamba ni mfano wa kuigwa kwa vijana,kutokana haiba na uwezo wake wa kujenga hoja na kuwasilisha katika jamii,lakini kisiasa January ni mwepesi mno, Kimsingi January alitumia umaarufu wa Baba na uwezo wa kifedha kumshinda Mh. Shelukindo tofauti na mwanasiasa kama Mh.Zitto au Mnyika ambaye hawakuegemea kwenye mgongo wa ukoo na mtandao wa fedha chafu, January aliweza kutumia uwezo wa kifedha kushawishi mgombea wa CDM kujitoa na yeye kupita bila kupingwa. Mgombea wa CDM alisusa fomu za kugombea ubunge na kuacha jukumu hilo kwa viongozi wa jimbo yeye akiwa Dar kutokana na ushawishi wa Babu yake ambaye ni kada mkubwa wa CCM. Kuna mchezo ulifanyika wa kusajili wadhamini wa fomu za ubunge kwa kutumia namba za kughushi (kutoka kwenye shahada za kupigia kura) ili fomu zisipitishwe na tume na yeye kutangazwa kupita bila kupingwa. [/FONT]


  [FONT=&quot] Kwa mtu asiyeishi maeneo ya jimbo la Bumbuli anaweza kumuona Mh. January Makamba yupo imara kisiasa kutokana na kuwa bingwa wa kudeal na vyombo vya habari na kushiriki kwenye kwenye mitandao ya kijamii. January anajitahiji sana kujijenga kitaifa zaidi huku akisahau wapiga kura wake wa Bumbuli. .
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa mtazamo huu zipo hisia ziliyojengeka kwamba ni vigumu kupenyeza siasa za CDM jimbo la Bumbuli, kitu ambacho si kweli. Kwa mtazamo wangu kutokana na nilivyojifunza kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Funta mwaka 2011 jimbo la Bumbuli lina wapiga kura wengi wenye ushawishi mkubwa wa mabadiliko kuliko majimbo yote ya wilaya ya lushoto (Lushoto na Mlalo) kinachokosekana ni mkakati kabambe wa kienezi kwa kutumia wanasiasa wenye ushawishi mkubwa ndani ya CDM na viongozi makini wa chama ndani ya jimbo la Bumbuli. Japokuwa CDM haina diwani Bumbuli kama ilivyokuwa Arumeru na CDM ikashinda ,naomba nidhibitishe kwamba CUF haipo Bumbuli kudhibitisha, kutokana na mtazamo wa wengi kwamba mkoa mzima wa Tanga CCM na CUF ndio wapinzani wakuu (sio sasa ni zamani!).

  ChondeChonde CDM wekeni viongozi makini Bumbuli.
  [/FONT]
   
Loading...