January Makamba na Umeme na Siasa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January Makamba na Umeme na Siasa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Jun 28, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Makamba amkingia kifua Waziri Ngeleja
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 27 June 2011 20:45 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Kizitto Noya, Dodoma
  MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Januari Makamba, amesema siyo sahihi kumlaumu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwa tatizo la umeme nchini.
  Akizungumza mjini hapa jana, Makamba alisema sekta ya umeme nchini imepita vipindi vitatu tofauti; kabla ya miaka ya 90 na baada kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2000, hivyo suala hilo limekuwa na historia.
  “Kimsingi siyo sahihi kumlaumu waziri wala Tanesco yenyewe, matatizo hayo yalikuwapo na waziri ameyakuta. Cha msingi kama Taifa, tushikamane na tuone tatizo hilo kama janga na tuungane kupambana nalo,” alisema Makamba.
  Akifafanua historia hiyo, Makamba alisema uendelezaji umeme nchini kabla ya mwaka 1996, Tanesco ilikuwa ikijiendesha kwa ufanisi mkubwa ikiwa inamilikiwa na serikali kwa asilimia zote.
  “Kipindi kilichofuata ni mwaka 1997 hadi 2006, Tanesco iliwekwa katika orodha ya mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa, lakini hakuna hatua iliyochukulia hadi mwaka 2006 uamuzi huo ulipobatilishwa,” alisema Makamba na kuongeza:
  “Wakati wote huo ikisubiri kubinafsishwa, hakuna uwekezaji uliofanyika katika shirika hilo wakati uchumi wa taifa ulikuwa unaendelea kukua kwa kasi kubwa kufikia kiwango cha asilimia saba na mahitaji ya umeme, yakiongezeka maradufu.”
  Kwa mujibu wa Makamba, baadhi ya miradi iliyotokana na uwekezaji mkubwa ni migodi ya madini na kampuni za simu, lakini wakati huohuo taifa lilikumbwa na ukame katika vyanzo vyake vya kuzalisha umeme wa maji, ikiwamo Mtera na Kidatu na taifa likaingia gizani.
  Alisema mipango mingi iliyobuniwa ianze kutekelezwa 2008 ambayo ilitarajiwa itakapokamilika ingezalisha megawati 645, hadi sasa ni miwili ndiyo imefankiwa; Ubungo (Megawati 100) na Tegeta (Megawati 45).
  unatarajiwa kukamilishwa na mkopo kutoka China wa dola 400 milioni za Marekani.
  Uwezo wa kitaifa hivi sasa wa kuzalisha umeme kama vyanzo vyote vya kuzalisha umeme vitafanya kazi ni megwati 1,100, ambacho Makamba alisema hakitoshi wateja wanaokadiriwa kufikia milioni sasa.
  Kwa mujibu wa Makamba, tatizo la umeme litakwisha iwapo serikali itaweka juhudi za makusudi kuwekeza katika uzalishaji umeme na kuweka kando tofauti za kisiasa.
  Alisema, iwapo juhudi zitafanyika haraka za kufanya uwekezaji mkubwa katika uzalishaji wa umeme kitaifa, kwa kutumia vyanzo vingine mbali na maji yanayozalisha asilimia 55 ya umeme wote nchini, taifa litaondokana na uhaba wa umeme.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Wakati Jerry Rawlings akiwa Rais wa Ghana, alichukua hatua za kufikisha nguzo na nyaya za umeme Ghana nzima, ikiwa ni pamoja ni vijijini kote. Kisha taifa la Ghana likabuni mbinu za kuzalisha umeme unaotosha nchi nzima.

  Kwetu sisi power grid inafika sehemu kidogo sana ya nchi, na tumebaki na stori tu za kwanini tusiwe na umeme. Waliotakiwa kuhakikisha taifa linakuwa na umeme mjini na vijijini ni serikali ya CCM na wameshindwa kufanya hivyo. Waachie ngazi. Hadithi hizi za akina Makamba hazisaidii chochote.
   
 3. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Tatizo siyo distribution bali ni generation. Kama hamna umeme, hamna umeme. Period. Hata nchi yote ikiwekwa kwenye grid. Huwezi ukaanza kuweka mikakati na kutumia billions kutengeneza miundombinu ya ku-distribute kitu ambacho hauna. Hiyo itakuwa ni irrational na uwongo mtupu.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,180
  Trophy Points: 280
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Miaka 50 baada ya UHURU, ilitakiwa tuwe tunakidhi kwa kiwango kikubwa matatizo yote mawili, ya generation na distribution. Ndio maana nikakupa mfano wa Ghana kuonyesha kwamba hata nchi zilizopatwa ma janga la kutawaliwa kwa nguvu na wanajeshi zimefanya vizuri kuliko sisi.

  Tutasherekea miaka 50 ya UHURU kwenye giza? Itakuwa ni ishara gani? Waingereza watakaokuja kuangalia tumewezaje si watasema (kama walivyosema wana UDSM miaka ya 1966) "Afadhali wakati wa mkoloni"!
   
 6. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hivi huyu kijana wa mzee marope hamnazo au Punguani? Si yeye aliyeandika ile barua kukosoa utendaji mbovu wa Ngeleja na wizara yake eenheee imekuaje sasa au kuna mabadiliko ya utendaji ktk hiyo wizara. Hii ndio uthibitisho kuwa wanasiasa wote ni WANAFKI, na wanafki hawataiona pepo
   
 7. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nami nilikuwa najiuliza vivyo hivyo! Tabia za kurithi ni mbaya sana! Huwa hazirekebishiki!
   
 8. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Makamba acha unafiki, Kwanza tunakutafuta sana ile kampuni yako ya Symbion ina utata , na wewe umeshiriki tunayajua yote na Documents tunazo, ipo siku yako utasema tu ukweli, watanzania tunakuangalia, na vijana wenzio tunakuangalia unavyofurukuta! acha kumuiga Ngeleja Mfanyakazi Wa Mafisadi( Rostam na wenzake) siku yake Ngeleja inakuja! take care zungumza ukweli acha brabra kama umeshindwa JIUZURU Sawa Bwana!
   
 9. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  ...love triangle at its best.....Ngeleja=Close aide and former attorney of Rostam/Vodacom
  ..........................................Dada wa January wa kule Vodacom=inasemekana ni small house ya Rostam
  ...........................................January Makamba=amkingia Ngeleja kifua sababu ya shemeji

  Hapo patamu, labda hadi Nape aingilie
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  nakumbuka huu jamaa aliandia waraka mrefu sana kwenda kwa ngereja.......akimwambia ajibu kwa nini nchi haina umeme na nini mikakati yake.....leo anakuja kivingine.......unafiki kitu kibaya sana
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Makambaaaaaa........hahahahaaaa
  ur not serious,sasa ile barua uliyomuandikia ngeleja na Mikwara kemkem ilikua inamaanisha nini???????
  Jaman wanasiasa hawa.........tuwaaache kama walivyo
   
 12. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,979
  Likes Received: 20,366
  Trophy Points: 280
  Sawa, ameyakuta na ni matatizo ya siku nyingi, je unataka kunambia hana mbinu za kuyaondoa kwa nafasi yake!!?? kuna maana gani ya yeye kuwa hapo kama hana namna ya kukabili changamoto au hili nalo ni suala lenye kusababishwa na hali ya kisisasa huko Libya, hebu tuache upumbavu wa kudhani kuwa upatikananje wa umeme wa uhakika hapa kwetu hauwezekani.

  Makamba anaanza kujikosha s ndani ya serikali kwani ana tuhuma zake za kupokea midolali so sasa inabidi achague upande sahihi kwa manufaa yake
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Majadiliano ya jana humu JF tulimkumbusha makamba kuwa kelele zake ni Urais wa 2025 kulingana na mipango yao ya kidini na JK kwa mipango kwamba; Asha Migiro/Hussein Mwinyi 2015-2025, baada ya hapo Makamba atagombea.Hizi ni ndoto za mchana MAKAMBA FIKIRIA NA CHUKUA HATUA KWANI UMEPOTEA
   
 14. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,989
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  zimwage hizo nyanga mkuu ili watu wasije wakasema na wewe unapika jungu tu...
   
 15. Rocket

  Rocket Senior Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimegundua huyu Makamba naye anatumiakia watu fulani kwani huwa anaongelea pande mbili kwa upendelo na kwa nyakati tofauti
   
 16. b

  beko Senior Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Babu, usanii hautaisha ndani ya CCM na serikali yake, tatizo la umeme limekua hadithi kila siku, watanzania tuna akili ya kufanya maamuzi na hatudanganyiki tena.
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tuungane kupambana nalo wakina nani? Mimi Mtanzania wa kawaida nina nguvu gani ya kutatua matatizo ya umeme? Halafu hichi kisingizio cha "aliyakuta" ni ya kitoto sana. Kwa kimsingi ilimradi matatizo tumeyakuta basi tusipo yatatua hakuna lawama???
   
 18. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  ameshavuta Bilioni mbili huyo na sasa wanajua watakuwa wamemshurutisha kusema la sivyo wanamvua gamba

  kwa kifupi na yeye kashiriki kunywa uji wa mgonjwa hahahaha
   
 19. c

  chachu Senior Member

  #19
  Jun 28, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  watanzania tutaendelea kuwa vichwa vya waenda wazimu mpaka lini, suala la uwajibikaji tunaliletea siasa. siasa mbovu, sera zisomakini ndio zinazotufikisha kwenye miaka 50 ya uhuru tukiwa gizani. mwanza ni siku ya tatu mfululizo hamna umeme huku mnaongelea mpango wa maendeleo ya mill je tutafika au ni blablaa.....! makamba watch out ili kufanikisha maendeleo kwa nchi yyt mhusika lazima uwajibike kwa namna moja au nyingine. if you dont have something to tell tz better to shut up.
   
 20. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Politics in this country have turned to be the Opium of Our Minds. How could someone stand in front of others in the time of a crisis like the one we are having now (mgao) and tell a story????I belive the politicians have become peoples' enermy Number One followed by illitrace, poverty and the rest of them. Kwa segere tunaloimbishwa sasa na watu waliokosa akili, busara na Moyo wakizalendo kama Makamba JR naomba maadui zetu wasomeke Kama ifuatavyo... Wanasiasa,Ujinga,Umaskini na Maradhi.
   
Loading...