January Makamba: Mafanikio katika Safari ya Kisiasa na Mustakabali wake

willpower

Member
Joined
Dec 3, 2019
Messages
78
Points
400

willpower

Member
Joined Dec 3, 2019
78 400
January Makamba: Malengo, Vikwazo, Makosa ya Kisiasa na Mustakabali wake

Mwanasiasa January Yusuph Makamba aliyezaliwa 28 January 1974 akiwa anakaribia kutimiza miaka 46 nimeona ni vyema sasa niandike kuhususiana na maisha na mapito ya mwanasiasa huyu. Nikiri wazi kuwa nimewahi kukutana na kufanya mazungumzo kwa dakika chache na January Makamba mwaka 2012 baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akiwa na kaka yangu Makame Mbarawa.

Wakati huo nilikuwa mwanafunzi wa shahada ya pili. Haikuwa rahisi lakini baada ya kuonana naye ni wazi kuwa January ni mtu asiyejivuna maana nilizungumza naye kama watu ambao tunafahamiana na alinisaidia kufikia lengo.
Mwanasiasa msomi aliyepita katika vyuo vya Saint John kule Minnesota na baadaye George Mason University mwaka 2004.

Huyu ni mwanasiasa lakini pia ana elimu ya kutosha kuwezesha kufanya siasa kwa namna iliyo bora kabisa.
Nilianza kuwa na mvuto kwa January Makamba mwaka 2005 wakati Rais mteule Jakaya Mrisho Kikwete alipomchagua kuwa Personal Assistant to the President – Special Duties. (PAP-SD) nafasi ambayo aliishika mpaka mwaka 2010.

Jina la January Makamba liliibuka tena na kufanya nimfuatilie tena mwaka 2013 baada ya kutokea katika orodha ya World Economic Forum – Young Global Leader lakini pia mwaka huo huo alipata tena kutokea kwenye Democracy Award kutoka taasisi ya National Democratic Institute. Mwaka mmoja baadaye 2014 January Makamba akaibuka tena katika Jarida la Forbes katika orodha ya 10 Most Poweful Men in Africa.

Tuzo hizi zilinifanya nimuangalie January Makamba kwa umuhimu na utashi zaidi. Kufikia wakati huu niliona kabisa inawezekana huyu anaenda kuwa mwanasiasa mkubwa katika siasa za Tanzania. Kadiri miaka ilivyokuwa ikienda nikaona ni wazi kuwa utabiri wangu unaenda kutimia.

Kwa yalitokea mwana 2019 inaweza kuwa kikwazo ama doa katika safari ya kisiasa ya January Makamba. Moja kati ya maswali ambayo wadadisi wengi waliuliza ni kuwa:

- Je January amepoteza umakini? Mtu mwenye umakini asingeweza kutojali kiasi cha kufanya alichofanya kama alikuwa anazijua siasa za kutafutana za Tanzania.

- Je January amefikia mwisho wa mafanikio yake hivyo hakuna alichopoteza?

- Je January atakuwa na ushawishi wa kutosha miaka ijayo baada ya kikomo cha serikali ya awamu ya tano?

- Je January Makamba hakuridhika na nafasi ya Uwaziri katika ofisi ya Makamu wa Rais?

- Je January aliyefikia hatua ya mwisho katika mchujo wa tiketi ya urais pale Dodoma bado atakuwa na ushawishi katika mchujo wa mwaka 2025?

- Je alikuwa anawindwa na maadui zake wa kisiasa ili wamwangushe kwa maslahi mapana ya miaka ijayo hasa mwaka 2025?

Kwa sasa sitashughulika kujibu maswali haya, lakini nataka tumuangalie January Makamba kabla ya yaliyotokea mwaka 2019 kisha tutarudi kwenye maswali na mustakabali wa kisiasa wa January Makamba.

Weka jambo moja akilini, kilichotokea 2019 kimemuathiri sana January Makamba kisiasa, na kama hana mipango stahiki ni wazi kuwa hii inaweza kuwa safari ya kurudi nyuma na sio kwenda mbele kwa January Makamba.

Zingatia kuwa January Makamba ana sifa zote za kuwa kiongozi bora na kiongozi mzuri, anahitaji kuwa makini.
Lolote linaweza kutokea kwa aina ya wanasiasa kama January Makamba, muda unaweza kuamua vyema. Ni matamanio yangu kwamba January Makamba arudi katika kiwango cha ushawishi alichokuwa nacho kwa kuwa sioni katika CCM mtu anayeweza kuwa mpinzani kwa sifa za kiuongozi hasa nafasi ya Urais katika siasa za miaka ya 2025.

Sehemu ya Pili ya Makala hii itaangalia Makosa ya Kisiasa ya January Makamba na Mustakabali wake wa Kisiasa. Nakumbuka kuzungumza na rafiki yangu mmoja kuhusu January Makamba wakati wa mkutano wa mazingira jijini Nairobi na niligusia kuwa naona akifanikiwa kisiasa, rafiki yangu huyu mkongwe kwenye masuala ya Kisiasa alijibu kwa kifupi "he is too comfortable and that won't bring him far".. je January Makamba alikuwa comfortable sana?

Tukutane kesho.
 

Oumuamua

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2018
Messages
495
Points
1,000

Oumuamua

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2018
495 1,000
Hanaga chochote special cha kumwandikia makala let alone kitabu. Nafasi ya baba yake ndio iliyombeba.
Hivi zile tuhuma za kuiba mitihani Galanos ziliwahi kuthibitishwa? Eti huyu nae huwa anaonekana smart kichwani.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,538
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,538 2,000
Bila kusubiri sehemu ya pili ya hiyo hadithi yako ni bora tukupe ukweli ulivyo. Ukweli ni kuwa Januari hana uwezo unaosemekana anao, bali mafanikio yake ni kutokana mbeleko ya baba yake na rais mstaafu JK. January unapomtoa nje ya siasa za kubebwa hana lolote analoweza kufanya, mfano mrahisi ni hivi sasa Magufuli hambebi amegeuka kuwa mlegevu. Kama unamsifia ni haki yako, lakini kama ww mleta uzi ni January mwenyewe ngoja nikuambie ukweli, huna uwezo wowote zaidi ya kutegemea kubebwa.
 

Kimikaki

Member
Joined
Oct 20, 2019
Messages
31
Points
125

Kimikaki

Member
Joined Oct 20, 2019
31 125
Bila kusubiri sehemu ya pili ya hiyo hadithi yako ni bora tukupe ukweli ulivyo. Ukweli ni kuwa Januari hana uwezo unaosemekana anao, bali mafanikio yake ni kutokana mbeleko ya baba yake na rais mstaafu JK. January unapomtoa nje ya siasa za kubebwa hana lolote analoweza kufanya, mfano mrahisi ni hivi sasa Magufuli hambebi amegeuka kuwa mlegevu. Kama unamsifia ni haki yako, lakini kama ww mleta uzi ni January mwenyewe ngoja nikuambie ukweli, huna uwezo wowote zaidi ya kutegemea kubebwa.
Upo sahihi sana. Mambo mengine wala sio ya kumung'unya maneno.
 

THE BREED

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Messages
839
Points
1,000

THE BREED

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2019
839 1,000
Alifanikisha ishu ya mifuko ya plastic ikambeba moyoni mwa baadhi ya watz,halafu nasikia akapost kituoa cha wizi wa kura!Mkulu a.k.a jiwe akakasirika akamwondoa!!!Inawezekana akarudi kwenye uwaziri awamu ya pili kama akikaa kimya na akirudi Bungeni!!!
 

Forum statistics

Threads 1,389,266
Members 527,879
Posts 34,021,483
Top