January Makamba: Kamwe CCM haiwezi kuachia dola mwaka 2015

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
08 OCTOBER 2012

Na Yusuph Mussa, Korogwe

MJUMBE wa Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. January Makamba, amesema chama hicho hakiwezi kuanguka katika Uchaguzi Mkuu 2015 na wanaosema kimefikia ukingoni kuongoza dola wamepotea.

Bw. Kamanda aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Tanga uliofanyika katika ukumbi wa Mamba Club mjini Korogwe.

"Kuna maneno yanasemwa mitaani kwa bahati mbaya hata baadhi ya wana CCM wenzetu wanaogopa na wanayaamini kuwa ya kweli lakini mimi nimekuja kama mjumbe, nataka kuwapa siri ya Kamati Kuu, kamwe CCM haiwezi kuachia dola mwaka 2015.

"Hali ya unyonge kuwa tutashindwa mwaka 2015 imepandikizwa, wapo wanaosema CCM inakimbiwa na vijana lakini ukiangalia mkutano huu hakuna chama kinachoweza kuwakusanya vijana kama hivi zaidi yetu," alisema.

Alisema moja ya mikakati ya kuifanya CCM isiondolewe madarakani ni vijana kuisemea mahali popote ambapo vyama vya upinzani vinaonekana kuungwa mkono na vijana kwasababu ya mikutano mingi waliyoifanya.

Naye Bw. Yusuph Makamba aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, alitumia fursa hiyo kutangaza kujiuzulu nafasi ya Kamanda wa UVCCM, mkoani hapa na kutaka uchaguzi huo utumike kuwaweka viongozi wenye mvuto ili chama hicho kiweze kuibuka na ushindi mnono katika Uchaguzi Mkuu 2015.

"Ili mchezaji aonekana mzuri lazima awe na pumzi ya kucheza dakika 90, lakini kama hana uwezo huo msimpe nafasi hiyo na kama anacheza lakini anaonekana kuchoka, lazima apumzishwe na kupewa nafasi yake mtu mwingine," alisema Bw. Kamamba.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa ambaye alimaliza muda wake, Bw. Rodgers Shemwelekwa, aliwataka vijana waache kuchagua wagombea wanaotoa rushwa ili wachaguliwe.

"Msikubali kupewa fedha na wagombea ili wawatumie kama ngazi ya kupata madaraka ya uongozi," alisema.

#############################

Wanamichezo watatu waula CCM


Na Omari Mngindo, Bagamoyo



WANAMICHEZO watatu wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamefanikiwa kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa.

Wanamichezo hao ni John Bolizozo Katibu anayemaliza muda wake wa uongozi ndani ya Chama Cha Mpira wa Miguu wilayani hapa (BFA), Mousin Bharwan mlezi wa timu zinazotoka ndani ya kijiji cha Vigwaza na Yussuf Kikwete mdau wa michezo Bagamoyo mjini.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Cha Sanaa na kusimamiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Abdul Marombwa, pia ulishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa na Katibu wa (CCM), Joyce Massi ambapo Bolizozo ameshinda nafasi ya Uenezi akiwaacha wapinzani wake Emmanuel Panduka na Kassim Gogo.

Bharwan ameibuka kidedea nafasi ya Mkutano Mkuu Taifa ambaye ameshinda nafasi hiyo kwa kujinyakulia kura 753 na kuwaongoza wenzake wanne ambao ni Shumina Sharif, Yussuf Kikwete, Aeshi Khatibu na Issa Kibwana nao wamechaguliwa nafasi hiyo iliwaniwa na wagombea 15.

Wakizungumza baada ya matokeo hayo, Bharwan alianza kwa kuwashukuru wajumbe wa Mkutano huo kwa kuweza kumchagua na kwamba atatumia nafasi hiyo kuhamasisha michezo ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama hicho.

"Katika Ilani ya chama chetu inagusia michezo, nitatumia nafasi hii kuhamasisha michezo mbalimbali ndani ya wilaya yetu kwa kuwapatia vijana fursa ya kimichezo kwani utakumbuka kuwa michezo kwa sasa ina nafasi kubwa ya ajira," alisema Bharwan.

Naye Bolizozo alisema baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya BFA akiwa Katibu atageuzia makali hayo katika nafasi ya Uenezi ili kuhakikisha vijana wanapata nafasi nzuri ya kushiriki michezo sanjali na kuhamasisha kujiunga na chama hicho.

"Nitatumia nafasi hii kuchagiza uendelezwaji wa michezo ndani ya Wilaya ikiwa ni kuunga mkono ilani ya CCM inayotaka kuendelezwa kwa michezo kwa wananchi bila kubagua itikadi za kisiasa," alisema Bolizozo.

 
522860_371976106210237_156410267_n.jpg
 
Kusema CCM hakitakufa ni kushindwa kuelewa kanuni za dayalectiki. Nashauri ujipe muda umsome George Hegel kuhusu nadharia ya mabadiliko. Thesis - antithesis - synthesis. CCM lazima inapitia na kwa maana hiyo kitakufu japo si lazima iwe 2015. Madai kwamba vijana wengi wasomi wanajitokeza, sio hoja yenye bali ni antithesis hiyo.

Kwanza hao ni waganga njaa tu kwani si ndo mnawapa kubeba mabegi ya pesa za kununulia kura mnadani na gulioni. Fuata nyuki ule asali ati. Kwa taarifa tu sasa hao vijana ndo wanaenda kumalizia ubomokaji wa chama, kwanza wana tamaa hivyo wala bila hata kunawa tena kwa mikoni miwili. Wao wanchotaka ndani ya hii miaka miwili wapata magari, miziki, majumba nk.

Subiri uone watakachowafanya.
 
Makamba hajakosea ikizingatiwa kuwa wana CCM sasa wanaishi kwa matumaini kama waathirika na isitoshe siku zote wanaishi kwa kujidanganya. Bado wanadhani Tanzania ni ile ya mwaka 47. Kwa fisadi mtoto kama huyu ambaye amefikia alipo kwa kubebwa na mfumo mchafu kama huu hawezi kuona kiama cha CCM. Hata wenzake akina Uhuru Kenyatta na Gideon Moi walikuwa wakiwabeza wapinzani mwaka 2002.

Makamba hawezi kuona uhalisia wa maisha na kukata tamaa kwa watanzania kiasi cha kulilia ukombozi. Amezaliwa na baba fisadi akamtengenezea njia na kumrithisha ulaji, Hajui njaa wala kufikiri zaidi ya kumuachia baba yake na mfumo mchafu kufanya hizo kazi za kufikiri, Vijana hata kama wanaganga njaa waliomo CCM bila kuwa na majina makubwa wanatapeliwa.

Wakitaka kujua ninachomaanisha, wajiulize. Wakati wao wanasoteshwa na mikopo, mwenzao Januari licha ya kuiba mtihani alitimka kwenda kusomea Marekani haraka haraka na akarudi na kuajiriwa katika ofisi ya rais. Huyu si mwenzao bali ni nyoka anayewachuuza wakidhani watakula tunda na kuukata wasijue ndiyo kiama chao.

Shame on you Januari!
 
January kama na wewe unaogopa kivuli cha vijana ,kaa usubiri moto,hao hao vijana ndio watawang'oa CCM yenu!labda mtumie dola kuwarudisha madarakani maana usemi wako unatisha kidogo,hamuwezi kuachia dola?kivipi?kama kura zenu hazijatosha mtafanyaje??hiyo ndio siri ya CC yenu?basi mmeshaua demokrasia!
 
Nami nimestuka sana na kauli yake nzito sana sana!!aulizwe ili afafanue maana nasikia ameandaliwa for 2025 awe President
 
Wadau hii kauli ya huyu jamaa imenipa mawazo kiasi!!

"nataka kuwapa siri ya Kamati Kuu, kamwe CCM haiwezi kuachia dola mwaka 2015."

Hivi hawa watu wana mpango gani?Ina maana hata tukipiga kura za kuwang'oa madarakani,hawatatoka?

akili za baba yake.
 
Kwani kuna ubishi tena Lowassa ndio anakabidhiwa nchi na swahiba wake hata watanzania wote wakipigia chadema bado ccm itazidi kuwa madarakani.
 
Ukweli husemwa:

"chama hicho hakiwezi kuanguka katika Uchaguzi Mkuu 2015 na wanaosema kimefikia ukingoni kuongoza dola wamepotea."


CCM haiwezi kuongoza nchi milele, hata kama mwisho wake siyo 2015, lakini ukweli ni kuwa, kimefikia ukingoni mwa safari ya kuingoza jamii. Wapenzi na wanachama wa CCM naomba mlitambue hilo na ukweli ukubalike.

Kama binadamu anapitia miongo furani mpaka kufa na hakuna jinsi nyingine, ni lazima afe tu, vilevile hata chama nacho lazima kiwe hivyo hivyo.

kilicho na mwanzo, hakikosi kuwa na mwisho.


 
Back
Top Bottom