January Makamba, kamati yako mliliangaliaje suala hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January Makamba, kamati yako mliliangaliaje suala hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HGYTXK, Apr 24, 2012.

 1. HGYTXK

  HGYTXK Senior Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Wakati kamati ya bunge inayohusika na masuala ya nishati na madini ikitoa ripoti yake bungeni nilishtushwa na suala moja ambalo linaniumiza kichwa mpaka sasa,Mwenyekiti wa kamati hiyo January Makamba alitoa ripoti kuwa serikali bado haijatekeleza mapendekezo ya kamati ya kuzika bomba la kusafirisha gas toka Mtwara mpaka Dsm ili kufua umeme utakaoingizwa kwenye grid ya taifa. Na akaongeza kusema kuwa mkataba umeshasainiwa na wachina ila bado pesa hazijatoka.

  Nataka kuiuliza kamati kuwa hivi ni kweli ktkt tasmini yao kwenye jambo hili walibaini kuwa garama za kuzika bomba toka Mtwara hadi Dsm ni nafuu kuliko kufua umeme Mtwara na kuusafirisha umeme kuuingiza kwenye hiyo grid ya taifa?.

  Kwanini wanaamini kuwa kila kitu cha kitaifa ni lazima kiende Dsm kwanza na si kwingineko? Mie nadhani haya ni mawazo mgando na ata kama kamati ya bunge mmeamua hivi basi nanyi ni miongoni mwa vikwazo vya maendeleoa ktk baadhi ya maeneo.

  Kwanini mtumie nguvu nyingi za kuhujumu kitu ambacho tulikiona kingekuwa chachu ya maendeleo ktk mikoa ya kusini? Wabunge wetu nanyi mpo ktkt hili au nayi mnasubiri kupiga meza tu na kusimama spika anapoingia na kutoka?.
   
Loading...