January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

Eti ndio aliingia tano Bora na kumwacha Bilali, Pinda, Augustino Ramadhani nje kwenye Kinyanganyiro cha uraisi

yaani hiyo ya ngazi eti jamaa badala ya kupanda na kutoka nje ameamua kuivunja ngazi na kuifanya kuni, vijembe vya uswazi kabisa, au Magufuli kamuacha kwenye baraza lake?
Alidhani watu hawatabaini fumbo lake huko alipo kama anaingia JF atakuwa amezimia maana wengi wamempa makavu live.
 
Kwani wewe umezielewaje? Kwa picha uliyoweka ina tafsiri nyingi tofauti! Yategemeana na mtu anavyootafsiri. Wewe umeihusisha na Magufuli, mimi nimeihusisha na Afrika na nchi za magharibi. Pia nimeihusisha na mtu anayetakiwa kutoka ila alichotakiwa kukitumia ili kutoka hakimwezeshi kutoka! Hii ipo hadi ktk family level!

1. Kama ni family level, inamaana ndani ya familia ya akina February kuna mtu analindwa kama rais + mlinzi?

2. Anawafumbia nini watu wa mataifa mengine wakti yeye hata hayupo kwenye level ya urais? ili useme kuwa marais wenzie huwa wanapitia pitia instgrm yake au ukuta wake wowote?

3. Lakini kwakuwa yeye ni mtanzania na ni mwanasiasa na alishawahi kuwa kiongozi, kila anachokifanya lazima kihusishwe na mustakabali wa siasa za humu nchini!

4. Je, haikuiingii akilini ukiangalia hizo picha utaona ni mmoja wa nguruwe wale anasubiriwa aingie kwnye gari la kiongozi na mlinz pembeni? Mwingine atafikiria kwamba, tulidhania ni "MTU" huyo kiongozi, kumbe ni sawa na "NGURUWE"?

5. Hiyo ya Nyani, naona kama Manyani wakubwa "walio kwepa mishale mingi" wanamshangaa nyani kijana anadanga danda kwenye nyaya za umeme badala ya kwenye miti na tena, ana mkia wenye herufi kadhaa!
- Je, ni kiongozi anayefanya mambo Fulani ya hatari kama kushika nyaya za umeme ambzo zinaweza kumsababishia hata kifo, bila kuiga mfano wa nyani wazee wanaomshangaa sasa.......kwa akili ya kawaida kabisa ujumbe huu unaenda kwa nani?
-Kwa nafasi alionayo, alishindwa kumfuata muhusika na kwemwelezea wasiwasi wake badla ya kuvaa kanga zenye mipasho?
-Amegundua nini hadi aandike hayo sasa, au huyo "nyani" katika kudanda danda kwake, amekata waya wa umeme unaoenda kwa jm au kwa mzee ym?

WANANCHI kwa ITIKADI ZOTE, kwa DINI ZOTE, TUPO NYUMA YA MAGUFULI na TUNAMWOMBEA MAISHA MAREFU! Na akienda na moto huu, tutaomba ikifika 2025 kipengele husika cha katiba kibadilishwe ili {kama KAGAME} aongoze miaka mingine KUMI!
 
Makamba hana issue na hafai kuwa wazir sababu ana maneno ya uchonganish kwa wananchi km Nape.
 
Kwani wewe umezielewaje? Kwa picha uliyoweka ina tafsiri nyingi tofauti! Yategemeana na mtu anavyootafsiri. Wewe umeihusisha na Magufuli, mimi nimeihusisha na Afrika na nchi za magharibi. Pia nimeihusisha na mtu anayetakiwa kutoka ila alichotakiwa kukitumia ili kutoka hakimwezeshi kutoka! Hii ipo hadi ktk family level!

Kwa hiyo unamaana January alitaka kutoka na Uwaziri Mkuu kakosa?
 
Mtu unaifwatilia account na post za watu bila sababu za msingi na kutaka mtu asiwe huru ku express mambo yake ndiyo Utoto na Upumbavu. Kwani shida nini hapo we piga kazi fanya yako

Kama si kufuatilia wewe mbona umejibu hapa? inamaana umejibu kitu ambacho hujasoma???
Elimu
 
Km wiki moja imepita nilikuwa naongea na MTU wa Uvccm pale Lumumba, alimsifia sana huyu kijana kwamba ni smart sana, anawajua wakuu wa wilaya na mikoa wote kwa majina yao, anajua km za barabara zote, akahitimisha kwa kusema ni Hazina ya CCM wakimtumia vyema

Ati anajua nn???sasa hyo ni hazina ya kukiriri au???
 
Tuache utani, hapo January Makamba alikuwa anatuma ujumbe mzito kwa hali inayoendelea kwa sasa hapa nchini kuonyesha Makamba hakubaliani nayo, nadhani kuna wakubwa wamemtuma kufanya hivyo, Binafsi nimeelewa hivi.
1/Makufuli alitengenezwa tu kushika urais, ila waliomtengeneza wanamshangaa kujifinya mjuzi.
2/Makufuli ameanza kusahau alipotokea...
3/Makufuli hata afanye nini ili kujibadili sura lakini bado ni mfungwa...
4/Makufuli anajimaliza mwenyewe....

Wanaumia na Bade pamoja na Hawa watu wanaofukuzwa kila kukicha walizani tutaisoma namba kumbe wao ndiyo wanaisoma namba.
 
Rais Magufuli January hafai. Kamchafua sana, Kikwete, Ridhiwani, Lowassa na sasa Magufuli.

Dogo Jembe, ikulu siyo ya babako
 
Tuko na frame of reference tofauti, hivyo usinilazimishe niielewe unavyotaka wewe kuendana na matukio yaliyopo! Nimekuelewa unavyotaka niielewe! Ila sijaielewa hivyo, tafsiri ya kwanza kabisa ktk ubongo wangu haikuwa hiyo unayotaka niielewe mimi

Okei, ngoja nije kwenye level yako ya kuhusisha picha na matukio ya kisiasa nchini! Picha ya pili, mtu anatoka ktk position ya juu na yenye status anaenda kuwa "mchunga ng'ombe", hapo jee!

Mchunga ng'ombe wake Kwa Ulaya Ni MTU Wa kuheshimika sana.
 
attachment.php


Picha hii kuna mtu alisaidiwa na watu kufika juu lakini ameshuka na wale waliomsaidia kufika huko hawathamini tena yaani ndio hizo mbao za ngazi anazozichoma kwa hiyo kamwe hawezi kufika kileleni.


attachment.php


Hapa anamsema kiongozi mkubwa ambaye alijifanya mtakatifu lakini mwisho wa siku safari yake itaishia kwa NGURUWE na hapo heshima yake itashuka.

attachment.php


Hapa anamsema huyo mtu kuwa amejifanya mjanja kuruka kutaka kujiondoa kwenye hilo kundi huku akijisahau kuwa mkia wake umenasa hapo hivyo hawezi kujichomoa na atabaki anaelea hewani.

***Kwa picha hizi kama huyu atakuwa kaukosa uwazi basi hizi picha ni mahususi kwa aliyemnyima uwaziri.**
 
Nimeamua kuleta hili jibu kwenye uzi mpya kwa faida ya wengi ,
Ni jibu la swali liloulizwa kwenye uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-hizi-picha-unamaanisha-nini-maakubwa-7.html


Wengi tumebaki kumtukana January Makamba , na hata ukiingia kwenye page yake Instagram hakuna mtu mpaka sasa aliye na clue yoyote kuhusu ana chojaribu kueleza January .

Mi mwenyewe zilinichanganya baada ya kuziona , lakin baada ya kukaa na kuzichunguza kwa mda mrefu , angalau kidogo nikapata mwangaza na maudhui ya ujumbe wa hizi picha alizoweka January kwenye page yake ya InstaGRAM

Disclamer : Mimi simjui January na wala sijawahi kuongea nae , hichi ntachoandika hapa ni kwa maoni yangu mwenyewe .

Tuanze kwanza na January . Kwa wale ambao hamumjui , January ana elim ya Uzamili katika Uchambuzi wa Migogoro na Azimio ( MSc in Conflict Analysis and Resolution ) na pia alishawahi kusomea Mafunzo ya Amani .

Picha za January

Kwenye picha 3 alizoweka January , kwanza kabisa katumia mbinu ya tashtit ( satire ) kuleta maudhui ya ujumbe wa picha , anachofanya January ni kuleta maana fulani inayomaanisha maana nyingine kabisa na ile wewe audience unayoweza kufikiria , Kwa kifupi January anatumia michoro ya Paweł Kuczyński mchoraji kutoka Poland anayejihusissha sana na kuchora picha kwa kutumia mbinu ya tashiti ( satire ) zenye kutoa maoni juu ya masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kupitia tashtit. Unaweza kuona collection ya picha zake nyingine hapa

attachment.php

Maana ya picha za January kwa kufuata mtiririko wa tarehe alizoweka.

Picha namba 1 :
Dont burn your opportunities for a temporary comfort ( Usichome fursa yako kwa ajili ya faraja ya muda )

Ukiangalia vizuri hizo picha , ya kwanza inamuonyesha mtoto akiwa amewasha moto kwa kutumia kuni ambazo chanzo chake ni ngazi anayotakiwa kutumia kutokea nje ( juu ).Huu ni ujumbe mkubwa unaoonekana kwenye picha namba 1 ambao wengi wetu tutajaribu kuuchukulia kijuu juu na bila shaka kufikiri jamaa anawapiga madongo watu fulani kwa kuunganisha na matukio mawili matatu yaliyotokea hivi karibuni.

Picha namba 2 : If Only Animals Were Given the Red Carpet Treatment That Humans Get. ( Kama wanyama tu wangekuwa wanapata heshima ya zulia jekundu ambayo binadam anapata ) .

Ujumbe huu unaweza kuuona kama wa ajabu , wengine kwa tafsiri za haraka unaweza kuuona kama una chembechembe za udini ( Fikra ambayo hata mimi niipata mwanzoni ) , sabab ukijaribu kuangalia kwa jicho la mbele hii picha inaonyesha gari kama ya kiongozi mkubwa au mtu maarufu , mlango umefunguliwa na hao wanyama wametoka ndani , wakatembea juu ya zulia jekundu na kwenda kula huku mlinzi akiwa anawasubiri aweze kuwarudisha heshima ambayo huwa wanapewa viongozi na watu maarufu tu . Tatizo ni hao wanyama ambao ni aina ya nguruwe , kiongozi mkubwa wa nchi alikua wa dini ile ya itikadi kali , Sitaki uingie kwenye udini kama mimi nlivyofikiria mara ya kwanza bali tumia IQ yako ya ziada kuubadilisha huu ujumbe , uuweke kwenye uhalisia wa jamii yetu ya Tanzania. nakuachia wewe uanganishe viulizo ( kwa lugha ya kitashi wanasema Connect the dots ) .

Picha namba 3 : Evolution facebook ( Mageuzi ya Facebook )

Kama zilivyo hizo picha zingine , ujumbe wa picha hii ni mgumu kidogo kuupata , kwanza kuna mambo matatu hapo . Kwanza ni hao watu wawili hapo chini walioko kama sokwe mtu wakiwa wamevalia suti ( hawa nimewaita sokwe wajanja ) na pili ni huyo mtu anayeonekana kurukia kamba huku nyuma ana mkia lakin akiwa amevalia kaptula peke yake , na la tatu ni huo mkia wa huyo huyo mtu aliyevalia kaptula unaonekana umebadilika na kwenda kuwa na alama ya facebook. Sasa unaweza kujiuliza mbona mkia una alama ya facebook , Sasa kwa nini facebook , kwa haraka utapata jibu ya kuwa facebook ni mtandao wa kijamii ambao unakuwezesha kukuunganisha na watu , Sasa kwa nini Facebook ? ni ujumbe gani anajaribu kuuficha January hapa .? Anachojaribu kuongelea January hapa hakiusiani na facebook kabisa , Bali anamaanisha kizazi cha sasa na teknolojia ya mawasiliano ambayo kwa sasa imekuwa kubwa kushinda kipindi cha zama za zamani kidogo , sasa hapa unatakiwa kuweka mitandao yote ya kijamii dunian ( Facebook , Twitter , WhatsAPP etc ) , Huyo mtu baada ya kurukia iyo kamba ambayo ukiangalia kwa umakini unaweza kuona vitu kama nyaya nyingi za umeme na vifaa kwa juu , inamaanisha baada ya kurukia hiyo kamba kwanza alikua amekamata kwa mkono , lakin alipoweka mkia kwenye waya akaanza kupata ufahama wa habari wa mtandao baada ya mkia kuanza kubadilika kuwa na alama na rangi ya facebook ( Facebook evolution ) . na ukiangalia vizuri inaonyesha ya kuwa huo mkia uko kwenye stage ya mwanzo kabisa , maana yake kama ni ufaham basi ndo ameenza kuujua , Je itakuaje akija kubadilika na kuwa facebook kabisa , nikiwa na maana huyu mtu apo juu akija kupata access ya kila punje ya information iliyowawezesha hao sokwe wajanja hapo chini kuvaa suti na kumwacha yeye na kaptula atachukua hatua gani kama akigundua hawo sokwe walivaa suti zao kijanja ? na ukumbuke wakati ye anapata ufaham wa yote hayo hao sokwe hapo chini watabaki kuwa sokwe nikiwa namaanisha bado wamebaki na sura ya mnyama wakati yeye keshapata ufaham ( amekuwa binadam ) , Sasa jiulize ni adhab gani binadam huwapa wanyama ?

Sasa Je ni nini maudhui ya ujumbe katika picha hizi huu .?

Siko hapa kwa ajili ya kutoa maana ya picha , bali ninachojaribu kueleza ni maudhui ya hizo picha , kwa hiyo nitayasema kwa kifupi sana

Picha ya kwanza na ya pili January kazielekeza kwa viongozi wakubwa waliotangulia, sasa kwa yale niliyokwisha ongea hapo juu , unaweza pata picha mwenyewe ni mambo gani January anayojaribu kuwaeleza hawa watu ,

Picha ya tatu inajaribu kuwaambia sokwe wajanja ya kwamba jamaa bado kidogo anakwenda kujua ukweli
Baada ya kuumiza sana kichwa ili kujua ni kwa nini January ameamua kutumia picha kuufikisha ujumbe huu , ilibidi kuanza kumchambua , Mwaka 2014 alishanakiliwa na gazeti la mwananchi akisema Tanzania inahitaji Raisi ambaye atakua dikteta , baada tu ya kutangaza nia ya kugombea urais na moja ya vitu alivyoongelea ilikua ni kuhusu kuanzisha mahakama maalumu itakayoshugulikia ufisadi na mengine mengi. ( Nakuomba kama una mda nenda kasome hiyo habari ), ambapo watu wengi walimpinga wakiongozwa na jarida la Business Times la 24 Oct 2014 pia mwaka 2010 alishawahi kuandikwa na Jarida la economics la marekani akiponda utawala unaotoa ahadi kila siku bila kutekeleza . Baada ya kusoma hayo , mengine mengi na kupitia hizo picha za January Makamba ndipo nikapata hasa maudhui ya ujumbe ambayo amejaribu kuufikisha . Nao unasema

WEWE MWANASIASA ULIYETUMIA UONGOZI WAKO VIBAYA KWA KUWABAGUA , KUNYANYASA NA KUWANYIMA HAKI ZAO WANANCHI , JITAYARISHE MAANA SIKU ZAKO ZIMEKARIBIA KUFIKA MWISHO .
 
Mimi picha za nyani anayebembea kwenye nyaya za umeme pamoja na mtoto aloyetumia ngazi ya kujiokoa kukokea moto nimeelewa pasi na shaka kuwa anamgusa moja kwa moja Magufuli! Hiyo picha ya nguruwe nimeshindwa kabisa kutafakakri!
 
Back
Top Bottom