January Makamba hili la Uteuzi wa Bodi ya TANESCO limekufunua mapema sana!!!

Kama kuwa na tuhuma tu ndo kigezo cha kujiuzuru Mbona Magufuli alikuwa na tuhuma ya kuuza nyumba za Serikali hadi Kwa hawara yake na akawa Rais na ukamuunga mkono humu?

TWO WRONGS DO NOT MAKE A RIGHT! Kutokuchukuliwa hatua Magufuli hakuzuii kumchukulia hatua January Makamba!!

Mchechu na mwenzie Raymond Mndolwa walikuwa wanachunguzwa na vyombo vya dola na mpaka ikatokea Raymond Mndolwa kukataliwa kuwa mgombea wa ubunge ingawa alishinda kura za Maoni na baba yake kuwa mjumbe wa Kamati kuu ya CCM!! Samia asiruhusu mambo ya namna hii kufanyika kwani yanaleta hisia mbaya juu yake kuwa alikuwa JASUSI ndani ya Serikali ya Magufuli!
 
Huyu kijana Raymoo amepata ukwasi mkubwa sana alipoanza kazi NHC yaani hela nyingi kaipatia hapo. Alipokuwa Dawasco alikuwa mtu wa kawaida tuu. Tanzania kuna maajabu sana.
 
Raymond ni mfanyabiashara mzuri sana. Akiwa Dawasco alikuwa na bar maarifu sana pale karibu na Kinondoni makaburini. Anaendesha pia bar nyingine hapo Mikocheni, sijui kama bado ipo!
 
Kumbe unamjua ni mfanyabiashara tangu akiwa na Bar Kinondoni halafu unashangaa kumuona ana ukwasi mkubwa akiwa NHC!! Fanya kazi acha majungu
 
Kumbe unamjua ni mfanyabiashara tangu akiwa na Bar Kinondoni halafu unashangaa kumuona ana ukwasi mkubwa akiwa NHC!! Fanya kazi acha majungu
Hapana sio mimi niliandika hivyo kuna makosa ya kiufundi yalifanyika yamerekebishwa!!
 
January Makama hana ethics za uongozi kwa hiyo hafai kuwa in any leadership opposition.Aachwe aka-fend for himself mtaani,that is the best option for him.Kuendelea kumbeba ni kulitia taifa letu hasara.Viongozi wetu tunaomba watuelewe.
 
January ana roho ya ngumu sana,aondoke.Hana huruma na Watanzania wa kawaida,hana aibu,haogopi viongozi wake,halipendi taifa lake,na nahisi kachanjiwa wizi.Ni aibu sana kwa Chama na Serikali kuwa na mtu kama huyu in any leadership position.

Nimpe ushauri wa bure Rais Samia.Uchaguzi 2025 unakuja.Kuwa-kumbatia watu kama akina Kinana,January,Nape na Ridhiwani to mention just a few ni hatari kwa hatma ya Chama na Serikali.Tanzania has 60+ million Tanzanians,why Kinana,why January,why Nape,why Ridhiwani.Tunaomba Rais awe na huruma na Tanzania na Watanzania.Kupeana uongozi kwa kujuana hakutalisaidia taifa letu kabisa.Au anataka uchaguzi wa 2025 utuwie mgumu kama wa 2015?Jamani hivi kwa nini hatujifunzi?
Mkuu, uchungu ulio nao ni kama nilivyo tu!!

Sielewi ni kwa nini Makamba anakumbatiwa na hizi kashifa zote

Kwa nini January katikati ya taifa lenye wasomi lukuki???

MTU asiye na huruma hata kidogo na wananchi na Taifa?

Unazuia shirika letu kuagiza mafuta unaruhusu wafanya biashara? Sababu za kuzuiliwa kwa uagizaji wa mafuta ni nini?

Unaagiza nguzo za umeme nje, hizi za kwetu zimekosa sifa gani?

Huyu mwenye kiwanda chake kule Bagamoyo aliyekuwa amepewa tenda ya nguzo za zege na Tanesco zimekosa sifa IPI na wakati tanesico wameanza kuzitumia miaka sasa..!

January ni nani?
 
Mbali na Mrema alipokua waziri wa Mambo ya ndani, sijaona waziri mwingine akilaumiwa Kama Makamba dogo.
Kuanzia alipokua fomfoo pale Galanos Tanga Hadi alivyopata ushindi wa bila kupingwa kwenye uchaguzi wa 2020, Hadi utendaji wake katika ofisi yake yasasa.
Mbona Kalemani hakusemwa Kama Makamba? Mbona hata Waitara hakusemwa semwa ukiachia tu tatizo lake la kupenda bia.
 
Mkuu, uchungu ulio nao ni kama nilivyo tu!!

Sielewi ni kwa nini Makamba anakumbatiwa na hizi kashifa zote

Kwa nini January katikati ya taifa lenye wasomi lukuki???

MTU asiye na huruma hata kidogo na wananchi na Taifa?

Unazuia shirika letu kuagiza mafuta unaruhusu wafanya biashara? Sababu za kuzuiliwa kwa uagizaji wa mafuta ni nini?

Unaagiza nguzo za umeme nje, hizi za kwetu zimekosa sifa gani?

Huyu mwenye kiwanda chake kule Bagamoyo aliyekuwa amepewa tenda ya nguzo za zege na Tanesco zimekosa sifa IPI na wakati tanesico wameanza kuzitumia miaka sasa..!

January ni nani?
Niache ni-express hisia zangu mkuu,hii nchi ni yetu sote,kwa nini watu wachache waisambaratishe huku tunaona?It is so painful.
 
Ndugu zangu Watanzania penye ukweli lazima tuseme hii Nchi ni yetu sote si ya watu fulani tu na siyo kwamba wengine wamekuwa Watanzania by default!

Nimeona nitoe mtazamo wangu ambao ninao kuhusu huu uteuzi wa January Makamba ktk Bodi ya TANESCO.

Kwanza Watanzania tukumbuke kuwa Wizara ya Nishati ndiyo imekuwa "Cash Cow" ya wapigaji/mafisadi kwa miongo kama miwili hivi!

Skendo zote kubwa kama Richmond,Dowans,Escrow n.k ni hapa.

Hata Rais Samia nadhani "ameshauriwa" vibaya sana kumtoa aliyekuwa DG wa TANESCO Dr.Tito Mwinuka na kumuweka Maharage Chande!

Rais Samia na January Makamba muda wote watambue kuwa suala la Umeme kwa Watanzania ni nyeti sana na si sawa na usambazaji wa visimbuzi vya Multichoice alivyokuwa akifanya Maharage Chande!

January Makamba amesukumwa zaidi na urafiki na "malengo yake ya baadaye" katika uteuzi huu!

Nehemiah Mchechu alipata tuhuma kubwa sana (tena toka kwa Rais Magufuli) kwa kujipa tenda za NHC) kupitia kampuni zake akiwa yeye DG pale! Amejisafisha lini na wapi?!

Balozi Maajar, huyu mama ndo aliwakilisha(kupitia kampuni yao Rex Attorneys) "wapigaji" wa TANESCO katika kesi za kimataifa!

January umeweka kwenye Bodi wafanyabiashara wakubwa ambao hawawezi kuwa think tank wa Nishati kwa Taifa hili!

TANESCO sasa inaongozwa na "Watuhumiwa" kuanzia Waziri January Makamba hadi wajumbe wa Bodi.

Hapa sio siri January Makamba umeonyesha uwezo mdogo wa uongozi unaofichwa na ambao wengi hawataki kuusikia!

January Makamba tunakutaka utengue mara moja hii Bodi yako ya hovyo na uunde Bodi madhubuti kwa maslahi ya Taifa hili na si kwa maslahi yenu wachache na "wapigaji" wenu!

Pia mshauri Rais Samia atafute DG anayeweza kum_ replace Dr.Tito Mwinuka kama issue ilikuwa ni kumtoa pale.
Vinginevyo January Makamba JIUZULU kwani hii Nchi ni ya Wananchi wote na si ya Viongozi pekee!

Na kama hii ndiyo strategy yako kwa "malengo ya baadaye" utafeli " big time"!

Soma pia:

1) Balozi Maajar kuwa mjumbe wa bodi Tanesco kuna walakini, tumesahau ya Dowans?

2) Profesa Shivji ashangazwa na uteuzi wa wafanyabiashara kwenye uongozi wa TANESCO

3) Waziri Makamba, Uteuzi wako wa Mama Maajar kuwa mjumbe wa bodi ya TANESCO una mgongano wa maslahi

4) TANESCO inarudi mikononi mwa mafisadi?

5) Waziri Makamba ameanza rasmi project alizotumwa TANESCO
Nimerudia kusoma uzi wako na uliyo yatahadharisha yametokea
 
Mkuu umepiga kwenye target. Kama ni kweli huyu anataka kuwa Rais baada ya kipindi cha Samia, basi hii ndiyo LITMUS paper yake. TANESCO anayoiona kwa kuwasha switch ukutani na mwanga unatoka ni tofauti na TANESCO ya Mtera, Kidatu, Kinyerezi, Hale, Nyumba ya Mungu na Kihansi. I bet ATAFELI tu

Wateule wake wengi wana mahusiano ya kikazi na kirafiki kwa muda mrefu. Katika kufanya maamuzi magumu ile timu ya Makamba haitakuwa na uwezo kwa sababu za mahusiano hayo
Na kweli Maharage na Makamba WALIFELI
 
Back
Top Bottom