January Makamba: Hata kama una vibali vya ujenzi, bomoa bomoa ni lazima

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
16,974
13,145
Hii taarifa imetolewa Leo, nashindwa kuiatach hapa ila hints ni Hizi.

1.Bomoa bomoa itaendelea baada ya mwaka mpya.

2. Wote waliojenga kwenye eneo lisiloloruhusiwa basi ahame kuanzia sasa.

3.Bomoa bomoa hii haitochagua mtu.

4.Hata kama utakuwa na vibali vya ujenzi au shughuli yeyote ile kwenye eneo lisiloruhusiwa ,haitozuia chochote utekelezwaji wa hii sheria ya mazingira ya mwaka 2004.

Taarifa hiyo imesainiwa na J. Y. Makamba.

Waziri wa mazingira, leo jijini Dar.
 
Saaaafi. asiye na hati ile kwake na mwenye hati afidiwe.
 
Katika utekelezaji wa matakwa ya Sheria pamoja na kanuni yeyote ile nzuri au mbaya Hekima, Busara na misingi mikuu ya usimamizi wa Haki haipaswi kubezwa kwa kisingizio chechote ama sababu yeyote ile.
 
Tatizo la watu wa mijini ni tofauti sana na vijijini wao kule kunapotokea tofauti na serikari kitu cha kwanza wanakimbilia mahakamani na kutafuta tafsiri ya sheria za ardhi kama wanavyozijua kabla ya tarehe za matukio ili kujikinga au kutafuta utaratibu mwingine ndio maana ukuti wanaburuzwa ovyo ovyo kama binamu zao wa mijini.

Sheria ni sheria na kama watu wamevunja lazima waondolewe lakini kuna sheria pia Tanzania kama ya 'occupiers liability 1968' mmiliki wa ardhi binafsi au serikari anatakiwa kusimamia ardhi yake muda wote kitendo cha kuacha watu wajenge, waanze kuvuta umeme, waweke makazi mpaka sehemu iwe na mitaa unaweza ukasema ni uzembe wa kuachia 'repeated events', allurement kutokana na ardhi kuzagaa and without warning to trespassers or settler on what they should do on that land (at least in English law version to the same statute) nadhani ata ukipekuwa katika statute law za contract ya makazi unaweza kukuta uzembe wa serikari pia kusimamia ardhi yake umepelekea watu kutapeliwa kuuziwa ardhi na kupewa hati bandia kwenye shemu ambazo mwenye ardhi akuzijali na ndio encouragment iliyowafanya watu wajenge (kama sakata la Tegeta garage na mmiliki) kwa hivyo kama ni makosa ya pande mbili ambayo mahakama inabidi iamue kwanza sio mwenye ardhi kwa kushindwa kuilinda ardhi yake in the first place.

Sasa serikari aijaenda hata kupata court order ya kuwatoa jamaa wanakuja wanavunjiwa na kubaki wanalia maana kuna sheria pia kama wanadamu zinawalinda hakuna mtu anaepinga kutimuliwa lakini kwakweli si kwa stahili za kinyama ambapo kuna watoto pia wanaoathirika; alikadhalika kwa upande mwengine on pure personal level unaona waache tu tatizo la watu wa dar ni ujuaji mwingi na wao nakuhakikishia wangekuwa wanavunja vijijini isingekuwa rahisi kama ilivyo sasa.
 
Hivyo vibali walivitoa wapi?

Vibali mtoe wenyewe halafu baadaye mje mvikatae na kuwaadhibu watu ambao pengine hawana makosa.

Je, hao waliovitoa hivyo vibali adhabu yao ni ipi?

Kwa mwendo huu hii serikali itakuja kuzikana hata passport, birth certicates na nyaraka zingine walizotoa wao kwa kigezo kuwa hii ni awamu nyingine na wao hawakutoa hizo
 
Kwa mwendo huu hii serikali itakuja kuzikana hata passport, birth certicates na nyaraka zingine walizotoa wao kwa kigezo kuwa hii ni awamu nyingine na wao hawakutoa hizo

Mimi siielewi kabisa hii serikali.

Kuna baadhi ya mambo ambayo inayafanya ambayo ni ya kipumbavu kabisa.

Kama watu walipewa vibali halali na kitengo cha serikali iweje muwabomolee tu nyumba au majengo waliyoyajenga?

Ifikie sehemu waanze kuongozwa na busara na hekima na si huu upumbavu wa kutaka sifa.
 
Back
Top Bottom