Elections 2010 January Makamba atumia ofisi ya rais kujitangaza jimboni Bumbuli kwa ubunge 2010

Madevu

Member
Apr 19, 2010
25
1
katika harakati za viongozi wa CCM wilaya Lushoto kumnadi Bwana Januari Makamba na kuwashawishi wananchi kumchagua, kampeni za kabla ya wakati zinaendelea ikiwa ni pamoja na vipepelushi vyenye jina la ofisi ya raisi kutumika.

namba iliyokuwepo kwenye kipepelushi ni ya Mwenyekiti wa UVCCM bwana Ramadhani Mahanyu ambaye ndie mpiga debe kubwa wa Bwana January.

wanachama wengi wamelalamikia ukiukwaji wa kanuni za chama juu ya kumnadi mgombea mmoja kabla ya wakati na kuashiria uchaguzi hautakuwa wa haki na usawa maana inaonekana chama kinashinikiza mtoto wa bosi wao ndio awe mbunge...

wananchi ndio watakaoamua...
January ubunge bumbuli.jpg
 
kwani huo uongozi umekuwa wa kifalme, baba na familia yake wamo au ndio kazi maalum inayoifaa familia ya bwana makamba, mi nashindwa kuelewa hapa hii Tz sijui itaishia wapi jamani kwa mtindo huu.
 
Jamani, lawama zingine hazina mantiki. Januari Makamba ni kweli yuko Ofisi ya Rais. Sasa akitaka kujitambulisha na kuelezea anakofanya kazi kwa sasa asemeje, anauza nyanya Kariakoo?

Huyu kijana ni bahati mbaya tu kwamba amejikuta amekuwa mtoto wa the controversial Katibu Mkuu wa CCM na ukiacha mambo personal ya mtu - ujana - anao uwezo binafsi kuweza kuwa Mbunge na akafanya kazi nzuri. Tumuache ajaribu bahati yake ili mradi anafuata utaratibu!

Halafu niliposoma kichwa cha post hii nilidhani ametumia karatasi yenye nembo ya Ikulu kumbe sivyo. Hii karatasi inaweza ikaandikwa na mtu yeyote ili kumharibia Januari!
 
Wakihojiwa utasikia wakikana. lakini pamoja na yote wamefikisha ujumbe!!
Systems za nchi hii zimejaa hujuma, uongo, ulafi, uzandiki, chuki binafsi, chuki za maendeleo, ufisadi na ulaghai uliokithiri.

Lakini hebu tuangalie kwa undani style ya Kikwete na watoto wa vigogo wenzake Ikulu na katika mtandao wake unatisha. Nadhani isifike wakati tukaanza kutengeneza himaya za kifalme na kichifu katika kuongoza nchi hii. Nchi hii tunahitaji viongozi na si watawala!

Si lazima uwe mwanasiasa ndiyo usaidie wananchi wa jimbo lako au wa nchi yako!!!
 
Maisha bora kiukweli si vibaya mtu kujitambulisha na kutambulisha mahala pake pa kazi, lakini ukisoma matumizi haya ya ofisi anayofanya kazi Januari hakukuwa na sababu ya yeye kuweka hapo ni wazi aliweka makusudi kabisa na hiyo ni matumizi mabaya ya ofisi yake, kwani angeandika tu " Mchagueni kijana wenu Januari Y makamba" kingeharibika kipi?

Halafu na hili la kugawa kadi bure CCM si walikataa mwaka huu, kama nakumbuka walisema hataruhusu wanachama wenye kadi mpya ambazo zimetolewa mwaka huu kupiga kura za maoni!? au kwa sababu huyu ni Januari Yusufu makamba yeye ni exceptional!
 
Maisha bora kiukweli si vibaya mtu kujitambulisha na kutambulisha mahala pake pa kazi, lakini ukisoma matumizi haya ya ofisi anayofanya kazi Januari hakukuwa na sababu ya yeye kuweka hapo ni wazi aliweka makusudi kabisa na hiyo ni matumizi mabaya ya ofisi yake, kwani angeandika tu " Mchagueni kijana wenu Januari Y makamba" kingeharibika kipi?

Halafu na hili la kugawa kadi bure CCM si walikataa mwaka huu, kama nakumbuka walisema hataruhusu wanachama wenye kadi mpya ambazo zimetolewa mwaka huu kupiga kura za maoni!? au kwa sababu huyu ni Januari Yusufu makamba yeye ni exceptional!

Kilembwe, hivi kweli unaweza kuwa na uhakika gani kwamba karatasi hii ameiandika January? Je haiwezi ikawa imeandikwa na mahasimu wake ili kumchafulia tu? Haingii akilini kijana mwenye elimu na uelewa alionao Januari kuweza kuandika ama kuagiza karatasi ya aina hiyo iandikwe.

Kitu kingine kinachonifanya niwe na mashaka ni namna jina la Mzee Shelukindo lilivyoingizwa humo.
 
Yote yanawezekana kwenye chama kinachoendeshwa kiimla na usultani
 
BoraMaisha kama alivyosema Mani yote yanawezekana hasa katika zama hizi za dirty politics!

OK let us give Januari a benefit of doubt na tuseme basi ahusiki, basi kwa kuwa vipeperushi hivi sasa viko hadharani na aje akanushe aseme yeye hausiki navyo basi!

Vinginevyo lazima tutaendelea kumnyooshea vidole! na kama ni yeye kuna siku atachomeka katika hotuba ya rais maneno ya kujipigia kampeni (yeye si muandishi wa hotuba za rais, na ukizingatia Rais wetu aliyo...) na Rais bila kujua atamrusha hewani.

Ni bora kuchukua tahadhari sasa!
 
Jamani, anybody can type a letter, scan it, and post it on the internet kwa nia ya kupiga majungu. Barua haina muhuri wala sigininecha.

And instead of people asking for the validity of this document mnaanza moja kwa moja kuosha vinywa. Unbelievable!
 
This is below the belt. U could see kwamba hiyo ni forged document....unapotaka kufanya propaganda..basi bora ufanye
zile zinazofanana na ukweli.

I'm not sure kama ni naivety ya Madevu au kuna political motivation ya ku mu undermine huyo mtoto wa Makamba?
Hivi ni mtu gani mwenye nia ya kugombea Ubunge hapiti kufanya kampeni za chini chini? Si ni last week Mnyika alikuwa kwenye
ziara Ubungo....si last week tumemuona Nape akiwa Ubungo pia?

Madevu tafuta agenda nyingine....hapa huna hoja....ushindani wenu muupeleke huko huko jimboni....usishindwe kwenye battle field
ukaanza kuleta baseless flimsy attacks ambazo sidhani kama zinaongeza nguvu ya kampeni ya mgombea unayemuunga mkono.
 
Barua feki...Iweje mhusika ashindwe kuandika jina lake kwa usahihi mara mbili kama katika hii barua hii.....Jina hapa ni "Jaruary" badala ya "January".....
 
jamani, lawama zingine hazina mantiki. Januari makamba ni kweli yuko ofisi ya rais. Sasa akitaka kujitambulisha na kuelezea anakofanya kazi kwa sasa asemeje, anauza nyanya kariakoo? Huyu kijana ni bahati mbaya tu kwamba amejikuta amekuwa mtoto wa the controversial katibu mkuu wa ccm na ukiacha mambo personal ya mtu - ujana - anao uwezo binafsi kuweza kuwa mbunge na akafanya kazi nzuri. Tumuache ajaribu bahati yake ili mradi anafuata utaratibu! Halafu niliposoma kichwa cha post hii nilidhani ametumia karatasi yenye nembo ya ikulu kumbe sivyo. Hii karatasi inaweza ikaandikwa na mtu yeyote ili kumharibia januari!
mie si mpenzi wala shabiki wa chama chenu ila naona points zako hapa.....apewe nafasi kama ataweza kweli!!!
 
Duh, naona haikuchukua muda 'wahusika' kujitokeza kujisafisha..mmhh

Kwanini watu mnajifichaficha kaa unazini vile, wee kaa unataka ubunge we weka mambo hadharani tu haina mbaya.

BTW GT yuko wapi ??lol
 
Endeleeni kuchekelea tu upuuzi wa watawala kuwaweka familia zao ndani ya mfumo wa kitawala.

Wakati mnataka kuchukua hatua ndipo mtagundua kwamba mmechelewa.
ENDELEENI KUCHEKELEA TU ndugu zanguni. VIZAZI VYENU VITAWALAANI huko mbeleni
 
Sisi tunaoelewa kinachoendelea tumechukua hatua gani? Kulaumu haisaidii, kinachohitajika ni matendo....
 
Halafu Tume na Msajili wa VYama wote wanajifanya hayaoni haya ya Makmba na kutaka kugeuza nchi kuwa ya kisultani wameshafukuza mwenyekiti wa UVCCM sasa wanataka wana ccm Bumbuli wasipige kura za maoni mbona Ngeleja wamemkatalia kule sengerema mbona hatumuoni chiligati au mkuchika kumpiga marufuku January na Babaye Yusufu kukoma kutumia janja ya nyani
 
Kuelimishana haitoshi wakati wengine wanachukua hatua. Je, tumejiandikisha kupiga kura? Je tumehamasisha jamii kujiandikisha? Je tumejitokeza kugombea hizi nafasi?
 
Back
Top Bottom