Uchaguzi 2020 January Makamba asema hana uhakika kama atagombea Ubunge 2020

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,476
215,295
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania
 
Hizi Kick za Wanasiasa achana nao kabisa, Hiyo Desemba atakuja na Ngonjela ooooohhhh Wazeee wa Bumbuli wamenifuata na kunisihi saaaana niendeleee na Kijiti cha Kusogeza mbele maendeleo ya Jimbo letu pendwa la Bumbuli hivyo sina budi kuendelea. Time will Tell
 
Aachie vijana sasa,ameshavuna vya kutosha

Japo kwa asilimia kubwa anawachezea mchezo akili ndogo ili wamtoe kichwani

Lkn kuna watu sio waongeaji wanamjua nje ndani
 
Hizi Kick za Wanasiasa achana nao kabisa, Hiyo Desemba atakuja na Ngonjela ooooohhhh Wazeee wa Bumbuli wamenifuata na kinishi saaaana niendeleee na Kijiti cha Kusogeza mbele maendeleo ya Jimbo letu pendwa la Bumbuli hivyo sina budi kuendelea. Time will Tell
Kweli kabisa
 
Kutafuta tu sympathy ...wanasiasa wanapaswa kujua siasa zinapita ila utu utaendelea kubaki...kupata na kukosa kwake ni yeye na familia yake!
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom