Election 2020 January Makamba asema hana uhakika kama atagombea Ubunge 2020

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
67,096
Points
2,000

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
67,096 2,000
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
5,559
Points
2,000

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
5,559 2,000
Aachie vijana sasa,ameshavuna vya kutosha

Japo kwa asilimia kubwa anawachezea mchezo akili ndogo ili wamtoe kichwani

Lkn kuna watu sio waongeaji wanamjua nje ndani
 

Forum statistics

Threads 1,379,670
Members 525,486
Posts 33,752,986
Top