Ukiondoa mikwara ya bwana mkubwa ni kwamba serikali yake inafanya kazi kwa mazoea kabisa. Ndiyo! Unakumbuka ni lini umeona ziara za kushutukiza? Unakumbuka ni lini umesikia mtu anatumbuliwa? Unakumbuka ni lini umesikia mtu amepewa siku kadhaa atekeleze jambo fulani?
Ukiwa unatafakari maswali yangu nikukumbushe kwamba serikali ilitangaza kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwamba ni siku ya usafi. Nikukumbushe pia kwamba waziri anayehusika na mazingira ni January Makamba. Nikukumbushe pia kwamba jana ilikuwa Jumamosi ya mwisho wa mwezi alafu nikuulize uliwahi kumuona Makamba akifanya au akihimiza usafi wapi na lini?