January Makamba amewekwa kwenye mtego, aliyoyakataa sasa anaenda kuyasimamia

Hayo ya kupinga matumizi ya hilo bwawa ni mtazamo wake binafsi.
Mjinga sana mleta mada. Anashindwa kutofautisha msimamo wa serikali na msimamo au maoni binafsi. Serikali, taasisi au umma ukishaamua kufanya jambo hata kama kiongozi fulani hapendezeshwi na hilo jambo hana budi kulifanya kwa ajili ya wengine.

January ameapa kufanya kazi kwa kufuata sheria na katiba ya nchi na hajaapa kufuata maoni na mawazo yake binafsi.
 
Waziri tu afutilie mbali ujenzi wa mradi mkubwa kama huo tena ukiwa 50%!!😁.

Sema joto la urais ndiyo litachemka zaidi.
 
Mbunge wa Bumbuli January Makamba alikuwa Waziri wa Mazingira katika serikali ya awamu ya 5 kwa miaka minne mpaka alipotenguliwa mwaka 2019.

Inasemekana January Makamba kwa kuwa alikuwa Waziri wa Mazingira kwa hiyo kimya kimya alikuwa anapinga mradi wa Bwawa la Nyerere kuwa eti utasababisha ukataji wa miti na hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira nchini.

Leo ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati huku Bwawa la Nyerere litakalozalisha zaidi ya megawatt 2115 likiwa limefikia 52% ya utekelezaji wake na tarehe 15/11/2021 litaanza kujazwa maji rasmi.

Je, January Makamba ataenda kumalizia ujenzi wa hili bwawa au ataenda kufutilia mbali ujenzi wake iki kuokoa mazingira kama msimamo wake ulivyo tangu zamani?

Yetu macho na masikio.
Linapokuja suala la kukaa madarakani, CCM hii ipo radhi kutamka bila aibu kuwa "mavi ni chakula". Na wakati mwingine kuyala mavi kabisa.

Mnisamehe kwa kuongea Kisukuma!
 
Back
Top Bottom