January Makamba amewekwa kwenye mtego, aliyoyakataa sasa anaenda kuyasimamia

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,363
2,372
Mbunge wa Bumbuli January Makamba alikuwa Waziri wa Mazingira katika serikali ya awamu ya 5 kwa miaka minne mpaka alipotenguliwa mwaka 2019.

Inasemekana January Makamba kwa kuwa alikuwa Waziri wa Mazingira kwa hiyo kimya kimya alikuwa anapinga mradi wa Bwawa la Nyerere kuwa eti utasababisha ukataji wa miti na hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira nchini.

Leo ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati huku Bwawa la Nyerere litakalozalisha zaidi ya megawatt 2115 likiwa limefikia 52% ya utekelezaji wake na tarehe 15/11/2021 litaanza kujazwa maji rasmi.

Je, January Makamba ataenda kumalizia ujenzi wa hili bwawa au ataenda kufutilia mbali ujenzi wake iki kuokoa mazingira kama msimamo wake ulivyo tangu zamani?

Yetu macho na masikio.
 
Unatunga uongo wako na kusema inasemekana alafu unauliza swali Kama atamalizia mradi?

Danganyaneni huko huko chato kwenu. January hajawai pinga mradi wa Bwawa la Nyerere. Acha kusema uongo
 
The comeback Kid...

Ashindwe yeye sasa, upewe nini tena zaidi ya kujenga jina na kuonyesha umahiri?!

Kazi kwake Mh J Makamba..
 
Bora mzee Chamuriho ametolewa ujenzi maana alikuwa mzigo mzito,
sasa Prof Mbarawa fuatilia ujenzi wa barabara,
 
Back
Top Bottom