January Makamba akiweza kutatua tatizo la umeme nchini atakuwa amejisafishia njia

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Hivi sasa nchi inapitia wakati mgumu kwa watumiaji wa umeme na mafuta. Kwa mtazamo wangu naona hizi changamoto zitakuwa zinamkosesha usingizi waziri husika.

Lakini kuna kitu kinaniambia kwamba huyu kijana hatokubali kushindwa kuzitatua hizi changamoto. Sababu kubwa ni kwamba yeye anajua fika kuwa baada ya mama kumaliza wakati wake ifikapo 2030 watu watampima kutokana na utendaji wake. Na kama akiweza kutatua hizi changamoto atakuwa amezikosha nyoyo za Watanzania.

Mawaziri wenzake wengi sasa hivi wabakaribia kwenye miaka ya 60.

Mpaka ifikapo 2030 wengi wao watakuwa wameshajichokea. Kwa hiyo kama akifanya kazi yake kwa weledi ifikapo 2030 ana nafasi kubwa ya kutoboa!
 
Kutoboa kwenda wapi? Uwezo wa kiwa Rais hana. Msamuzi yake ya kwenda kujitetea Twitter bado yana ujana mwingi. Lilipotokea swala la vifurushi kupanda bei 2015 alienda Twitter kujitetea, hili la mafuta nalo kaenda Twitter, la crane nalo yupo Twitter.

Anajali sana watu wa Twitter wanasemaje. Akipata mtu wa aina ya kigogo kama Magufuli au ZeUtamu kama JK atachanganyikiwa.
 
Naona unaanza kumuoteshea mapembe January.....anyone can be a president come the next election. Hii Hali ya kutaka tuamini kwamba makamba ndiye smart and potential leader kuliko wengine ni hujuma.

Unamfanya asifanye kazi kwa utashi akijua mbeleni Kuna urais.

Mkuu Kaa kwa kutulia hata wewe unaweza kuwa Rais. Nobody knows tomorrow.
 
Mtoa mada unaweza ukawa mjinga kiasi fulani. Kwanini unatamka wazi hiyo 2030? Wewe akili zako ni fupi. Wewe sio Muumba mbingu na Dunia utamke 2030. Sisi binadamu hatuijui siku wala saa ya kuondoka hapa ulimwenguni. Sasa wewe endeleza huo ujinga
 
Mleta uzi ni kati ya wanao nufaika na uwepo wa Makamba
 
Naona unaanza kumuoteshea mapembe January.....anyone can be a president come the next election. Hii Hali ya kutaka tuamini kwamba makamba ndiye smart and potential leader kuliko wengine ni hujuma.
Unamfanya asifanye kazi kwa utashi akijua mbeleni Kuna urais.

Mkuu Kaa kwa kutulia hata wewe unaweza kuwa Rais. Nobody knows tomorrow.
Sijui watanzania katuroga nani?
Hivi Makamba awe rais kwa kigezo kipi au kwa sifa zipi?
 
Kutoboa kwenda wapi? Uwezo wa kiwa Rais hana. Msamuzi yake ya kwenda kujitetea Twitter bado yana ujana mwingi. Lilipotokea swala la vifurushi kupanda bei 2015 alienda Twitter kujitetea, hili la mafuta nalo kaenda Twitter, la crane nalo yupo Twitter. Anajali sana watu wa Twitter wanasemaje. Akipata mtu wa aina ya kigogo kama Magufuli au ZeUtamu kama JK atachanganyikiwa.
Hatufai kabisa kwenye nafasi ya urais huyu ni kati ya watu wanao pigania uongozi kwa juhudi sana.

Akiupata ni rais sana kutuuza kama taifa.
 
Back
Top Bottom