January Makamba ajibu hoja hii ya Raia Mwema....

Suala la January na wengine (Salma Kikwete, Rithiwani Kikwete, Alfani Kikwete) waliotajwa kwenye makala ya Mmbwambo lilikuwa pia na sura nyingine...Muda wanaotumia kufikia hapo walipo!!

Inawezekana kweli January anao uwezo wa kuiongoza, ila angeweza kufikia mafanikio hayo ndani ya kipindi kifupi? Hili nalo linasikitisha sana kwani kwa mazingira yetu, mafanikio ya haraka haraka lazima yaandamane na ufisadi wa aina fulani....ama wa pesa au matumizi mabaya ya madaraka!!

Tatizo kubwa kwa hawa vijana ni kwamba tukuwagusa wanasema tuna wivu wa kike....very pathetic! Hata hivyo hizi hoja zisipofanyiwa kazi basi wajue wanajichimbia makaburi yao wenyewe!
 
Mkuu kama unaongelea RI1 kwa sasa ni wazi kujua katajilika vipi
baba RI1 hakuwakilisha pesa aliyopewa na waarabu wa mahotel na kutoka saudi kwenye CHAMA CHA MAJUHA
chama kikaiba hela a umma kufanya kampeni

hiyo hela aliyokusanya VASCO DAMA kutoka kwa maswahiba wake na nchi mbalimbali ikiwemo libya
ndizo RI1 anafanyia biashara, hivyo ndivyo familia ya magogoni iliyotajirika sana, na wanahela hao
Tatizo ni sasa wengine ndani ya chama cha majuha wamejua hiyo siri kutoka wikileaks

Haya majizi ya kalamu!
 
Madaraka ya koo za mafisadi,mtu hana weredi anabebwa na mbeleko ya chuma ili asianguke,ili mladi apate pa kutajirikia.
 
mimi bado hainiingi akilini kila ninapofikiria na kukuta orodha kama hii,Jakaya kikwete-Ridhiwani kikwete,Yusuph makamba-January makamba,Hassan mwinyi-Hussen mwinyi,Pius msekwa-Anna abdalah,John malecela-Anna kilango malecela,Wiliam shelukindo-Beatrice shelukindo,Aisha kigoda-Abdala kigoda nk.ukija kwenye ajira ndio utachanganykiwa ma ana ni kama ma-Public relations wa makampuni makubwa karibu yote utakuta ni surname za wanasiasa vigogo tupu,na sasa uteuzi wa ma RC na ma DC ndio ushkaji mtupu,je tutafika
 
Mkuu mimi maoni yangu ni kuwa kweli wapo wanaostahili kwa nafasi walizopewa au kuzawadiwa na wazazi wao. Lakini hapa kuna tatizo kubwa sana la kiuongozi kwani hawa viongozi wetu walio madarakani wameonja utamu wa madaraka na hivyo hwataki tena kujitenga na huo utamu. Hapa ndipo wanapoamua kuanza kutafuta mbinu za kuwapenyeza watoto wao ili na wenyewe warithi huo utamu wa madaraka.

Kwa kuwa Tanzania kuwa kiongozi si kazi sana kwani hata ukiwa si muwajibikaji utalindwa tu so long as unatimiza matakwa ya aliyekuweka. Kama kungekuwa na utamaduni wa kuwajibishana kwa kila mmoja mwenye makosa bila kujali tofauti basi hapa uongozi ungekuwa na taswira tofauti sana na hii iliyopo sasa.

Chukulia mfano, Mh Rais J.M. Kikwete aamue kumpigia debe mwanae Ridhiwani Kikwete awe waziri mkuu baada ya yeye kuondoka madarakani. Hivi unafikiri hata kama akipwaya kuna mtu anaweza kumuwajibisha? Hapa labda rais mwenyewe anaweza kuwa amewekwa na mzazi wa huyo huyo anayetuhumiwa. Upo mfano mzuri sana wa Mh Hussein Mwinyi ambaye ni waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa. Hata kama ataboronga vipi lakini Mh rais Kikwete hatothubutu kumuwajibisha kwa kuwa anaogopa atamuudhi mzee mwinyi kwa kuwa hata yeye mzee mwinyi amechangia hapoa alipo sasa.

Hivi hawa viongozi tulionao sasa wanataka hii nchi iwe ya kifalme au? Wangekuwa hapa kama baba wa taifa hili mzee wetu mpendwa mwalimu J.K. Nyerere angetumia mfumo huu walionao wao? Hapa ni jukumu la viongozi wetu kuvumbua vipaji vya uongozi kwa vijana wenye damu changa kwa kuwapa fursa ili waweze kuonekana vipaji vyao vya uongozi kama wao walivyopewa fursa hiyo na mwalimu.

Kwa mtazamao wangu mimi, wapo vijana wengi sana ambao wana uwezo wa hali ya juu kwenye hili suala la uongozi lakini hawapati hizo fursa. Wanaopata fursa ni watoto na ndugu wa viongozi wetu. Chukulia mfano kama kijana Mh J.J. Mnyika mbunge wa ubungo, kama si jitihada zake binafsi na msukumo wa chama chake na uma kwa ujumla asingeliweza kufika sehemu kama alipo sasa. Tazama alivyo sasa, ni ishara tosha ya kuwa hata watoto wa masikini nao wanaweza. Hapa mh J.J. Mnyika ameonyesha kwa vitendo. Wapo wengi sana, lakini kwa uchache naweza kuwataja ni kama mh Mkosamali, mh Zitto, mh wenje, mh halima mdee, na wengine wengi.

Kwa vijana kama Mh. January Makamba mimi naona jina la mzee wake limembeba sana hadi hapo alipo na si juhudi zake, hivyo kusema kama anaweza au la hapa yatupasa tusubiri kidogo ili tumpe muda wa kumtathimini. Kama wangekuwa wanawekwa kwenye mzani wenye usawa katika kufikia vyeo vya juu basi hapa ndipo tungepata kusema fulani ana uwezo mkubwa wa uongozi.

Vijana wetu mungu yupo pamoja na ninyi, hivyo aluta continua mtafikia malengo yenu. Lakini chonde chonde ulevi wa madraka ni nomaaaaaaaaaaaaaa!

Nakubaliana na uchambuzi wako na hasa huo mfano ulioutoa wa Hussein Mwinyi ambae sasa hivi ni waziri wa ulinzi. Hussein Mwinyi yupo hapo alipo kwa nguvu ya jina la mzazi wake ambae ni Rais mstaafu; hakuna hata kitu kimoja alichokitenda kwa jamii ya kiTanzania ambacho kinampa sifa ya kuweza kushika nyadhifa zote za kisiasa alizowahi kushika tokea kuwa mbunge wa Mkuranga mpaka sasa kuwa waziri, vyote alivyopata vimetokana na nguvu za baba yake. Hivyo hivyo kwa mdogo wake ambae sasa ni mbunge wa bunge la Afrika Mashariki ; huyu hata kampeni hakufanya wakati wa uchaguzi kwani rushwa yote ya pilau na fedha ilifanywa na kutolewa na mzazi wake pamoja na fedha za Epa toka kwa wahindi zilizotumika kuwahonga wabunge. Sasa hii ni dhahili kuwa hawa wanabebwa na sio uwezo wao na huwezi kuwafananisha na wakina Halima Mdee na Mkosamali vijana ambao wamejipambanua kuwa wanauwezo na watu tumedhihilisha hivyo!! Athari za viongozi kuwarithisha watoto wao vyeo hata pale wanaonesha wazi hawana uwezo wa kuongoza tumeziona kwa waziri wa ulinzi Hussein Mwinyi pale aliposhindwa kuongoza wizara hata tukapata majanga ya mabomu kule Mbagala na Gongo la Mboto; lakini hata hivyo kwa mtindo ule ule wa kubebana hakuna aliyeweza kumuwajibisha!!
 
Naungana na waliochangia mada hii kusema kwamba January Makamba ajibu hoja.

Lakini ukweli ulisimama kidete ni kwamba kila abebwaye abebeke na wapiga kura na atekeleze ilani iliyompa madaraka. Kuhusiana na kwamba aliyebebwa ni mtoto wa kigogo fulani hii haina nguvu sana iwapo hakuwekwa kwa mtutu wa bunduki au ukandamizaji au rushwa. Ebu tupime la rais George Bush Sr kumtayarisha mwanaye George Bush Jr, kuchukua nchi kwa uchaguzi wa democracy ya kimarekani.. Je alimbeba na kumpa nchi?? Jibu: HAPANA

Karume kuongoza Zanzibar je marehemu babake alimbeba jibu: HAPANA. Pamoja na ushawishi wa majina ya wazazi watoto nao hurithi tabia zao kama isemavyo methali ya kiswahili: MTOTO WA NYOKA NI NYOKA.. Akiwa nyoka kweli sawa atatusaidia lakini akiwa mjusi tumeliwa maana mzee wangu alisema kwamba KATIKA MSAFARA WA MAMBA NA KENGE WAMO!!!! Ni jukumu la wapiga kura kupambanua na ,kuamua nani anafaa kuwa kiongozi wao bora. Hii ndiyo demokrasia ya kweli!!
 
so binafsi nafikiri Makamba angejibu hii hoja kwa kuandika
Makala kwenye gazeti hio hilo la Raia Mwema.......

nipo curious kujua anaweza kujibu vipi hoja hiyo na nafikiri huu ni mjadala muhimu kwa taifa...

LEO WATOTO WAO,KESHO NANI?WAKE ZAO?....

Pengine nikukumbushe tu kwamba hili suala January alishawahi kulizungumzia huko nyuma. Kuna mahojiano alifanya na Absalom Kibanda na gazeti la UMOJA, na vile vile yamo kwenye maelezo ya ndani ya website yake binafsi:

Jarida la UMOJA Aug 2010:


"5. Je kuna uhusiano wowote wa kuwa kwako msaidizi wa Rais Kikwete na ukweli kwamba wewe ni mtoto wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba?


Rais Kikwete aliponiteua kuwa Msaidizi wake, tarehe 21 mwezi Januari 2006, Mzee Makamba alikuwa bado hajawa Katibu Mkuu wa CCM (ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mwezi Juni 2006). Kwahiyo labda ungeuliza kwamba kuna uhusiano wowote kwa Mzee Makamba kuwa Katibu Mkuu kwasababu mimi ni Msaidizi wa Rais. Hata hivyo, dhana iliyomo kwenye swali lako kwamba Rais Kikwete anaweza kufanya uteuzi wa msaidizi wake mmoja kwasababu tu ni baba au mtoto wa msaidizi wake mwingine haina msingi, na inaashiria kutoelewa jinsi Rais Kikwete anavyofanya kazi na anavyofanya maamuzi. Rais Kikwete anateua watu kwa sifa zao na uwezo wao. Kama huko mbele baadhi yao wanamuangusha, huo ni mjadala mwingine.

6. Katika siku na miaka ya hivi karibuni umeibuka msamiati maarufu katika vyombo vya habari na katika jamii wa ‘watoto wa vigogo’ ambao unahusisha mafanikio ya kimaisha, kikazi na kidhamana ya watu wa aina yako na viongozi wa juu ambao ni wazazi wao. Unalisemeaje hili?
Cha msingi cha kutazama ni kama hao wanaoitwa “watoto wa vigogo” wana sifa za kushika dhamana walizonazo. Jambo la msingi ni kwamba hao wanaoitwa “watoto wa vigogo” wasipendelewe kwa kupewa kazi na dhamana ambazo hawana sifa za kuzishika kwasababu tu ni “watoto wa vigogo”, lakini vilevile wasinyimwe haki ya kupata kazi na kupewa dhamana zinazolingana na sifa zao kwasababu tu ni “watoto wa vigogo”. Bahati mbaya sana ipo dhana kwamba ukishakuwa unatoka kwenye familia ya siasa, basi mafanikio yako binafsi, ambayo umeyapigania kwa jasho lako, yanaonekana sio ya kwako, inaonekana kwamba lazima umebebwa. Baadhi yetu tunaoitwa “watoto wa vigogo” tumeishi maisha ya kawaida, tumechunga mbuzi, tumepata kuwa na funza miguuni, tumesoma shule za kawaida za Serikali hapa nchini na tumesota kweli hadi kumaliza shule na kutafuta kazi kwasababu hata hao vigogo wenyewe wapo wengi tu ambao wanapenda watoto wao wafanikiwe kwa jasho lao wenyewe. Halafu kuna hii dhana kwamba sasa nchi inaingia kwenye uongozi wa kurithishana kwasababu tu kuna vijana wanaotoka kwenye familia za siasa ambao wameamua kuingia kwenye siasa. Dhana hii haina msingi ukitazama hali halisi. Kwanza, naamini zaidi ya asilimia 95 ya wanasiasa wa Tanzania wa sasa hivi hawajatokea kwenye familia za siasa na wazazi wao hawakuwa kwenye siasa. Pili, naamini zaidi ya asilimia 95 ya wanasiasa waliopo sasa wasingependa kuona watoto wao wanaingia kwenye siasa kwasababu wao wameshaionja shubiri yake. Tatu, vijana wengi wanaoitwa “watoto wa vigogo” ambao wameamua kuingia kwenye siasa hawakusukumwa na wazazi wao. Vijana wengi siku hizi wana uhuru wa kujiamulia wanataka kufanya nini na maisha yao. Na kama wakiamua kuingia kwenye siasa basi wasishambuliwe au kusakamwa kwasababu tu wazazi wao nao wamo au walikuwemo kwenye siasa."
January Makamba.com

"My Story", from his website Dec 2010:

"But, I have been lucky that I was spotted and given an opportunity to prove that I am indeed worthy of big responsibilities. Other young people, perhaps more competent than I am, have not been spotted yet. I have therefore made a point of advancing young talented people in positions of public service. I won’t mention names but I am proud that there are more opportunities for young people now to serve their country and society. I will finish by admitting that my last name has helped me because of the ready-made network of willing helpers. But also it has placed undue burden and responsibilities, including inheriting enemies who we haven’t even crossed paths. I also had to work twice as hard to prove that I am my own person, and my successes are borne out of my own efforts. I saw my family fortunes go up and go very down – one of the lowest points was when both my parents were unemployed and we lived with relatives in Korogwe while father tried-out timber business. It is rare to get an opportunity to tell my story which indicates a humble background – internal displacement, growing up with jiggers and stomach worms, raised under a leaking roof. I grew up with value of fierce independence, concern for others and being true to one’s self. I hope to bring these values into my political career." January Makamba.com
 
Nadhani mtoa hoja ume eleweka, kama wapo waliobebwa tuwapime kwa utendaji wao kama unatufaa na tuweke wazi vigezo vya ulinganishi. Ikiwezekana pia tuangalie ukubwa wa mbeleko iliyotumika.
 
Namkubali sana Johnson Mbwambo

na gazeti la wiki hii la Raia Mwema amerudia tena kusema January Makamba na watoto wengine
wa vigogo wanabebwa na kupewa madaraka kitu ambacho kitakuja kuleta vurugu hapo baadae nchini...

But hapa kuna hoja mbili.......
kwanza watu wanabebwa huku hawafai.......

pili kuna wanaobebwa lakini pengine wana uwezo....au pengine
tunawahukumu kwa sababu ya majina yao......

Gazeti la Raia Mwema wana utamaduni wa kukubali hoja kutoka kwa watu
hata ambao linawashutumu....so binafsi nafikiri Makamba angejibu hii hoja kwa kuandika
Makala kwenye gazeti hio hilo la Raia Mwema.......

nipo curious kujua anaweza kujibu vipi hoja hiyo na nafikiri huu ni mjadala muhimu kwa taifa...

LEO WATOTO WAO,KESHO NANI?WAKE ZAO?....

Hapo kwenye bold mkuu vyama vingi tu vina huo ugonjwa kuna chama fulani kina baba, mtoto na mkwe na wote ni wabunge wa chama chao tena hawa tujaalie wachukue madaraka sijui itakuwaje! kuna chama fulani kina jimbo sehemu ya usukumani hicho chenyewe kinaendeshwa kama taasisi ya mtu binafsi na kuna malalamiko yalishawahi kutolewa.

Kwa hilo la kubebwa sio wa serikalini kwetu hadi kwenye mashirika na vyama vya siasa vya upinzani. Yaani haka ni kaugonjwa sote tunaugua.
 
Namkubali sana Johnson Mbwambo

na gazeti la wiki hii la Raia Mwema amerudia tena kusema January Makamba na watoto wengine
wa vigogo wanabebwa na kupewa madaraka kitu ambacho kitakuja kuleta vurugu hapo baadae nchini...

But hapa kuna hoja mbili.......
kwanza watu wanabebwa huku hawafai.......

pili kuna wanaobebwa lakini pengine wana uwezo....au pengine
tunawahukumu kwa sababu ya majina yao......

Gazeti la Raia Mwema wana utamaduni wa kukubali hoja kutoka kwa watu
hata ambao linawashutumu....so binafsi nafikiri Makamba angejibu hii hoja kwa kuandika
Makala kwenye gazeti hio hilo la Raia Mwema.......

nipo curious kujua anaweza kujibu vipi hoja hiyo na nafikiri huu ni mjadala muhimu kwa taifa...

LEO WATOTO WAO,KESHO NANI?WAKE ZAO?....

I know January well. The guy is one of the most brilliant JK ever had. Yaani hotuba alizokuwa akiandika JK hatakaa kuona kama hizo katika utawala wake. January for President wapende wasipende 2015. Na ukiwa Rais, wa kwanza kupeleka lupango ni JK, Mama Salama na Riz1 wajinga sana. huu ni wivu wanaotumia kumchafua january baada ya kuona nyota yake inapanda. jamaa kichwa
 
Januari makamba hana uwezo ukilinganisha na nafasi aliyonayo.Hawa wamepata nafasi kutokana na uwezo na majina ya wazazi wao.Tanzania hatuna jukwaa la kuwapima uwezo hawa viongozi wa CCM ,kwa wachache ambao tunafuatilia unaweza ukaona/kupima/kulinganisha uwezo wa mtu kama Januari Makamba na John Mnyika,sio kwa kujibu/kuchangia hoja bali hata kihistoria .January makamba hana historia katika kujishughulisha na maswala ya kijamii utakayosema imembeba.
Moja ya mambo ambayo ni dhahiri unaweza kumpima mtu ni katika kujibu hoja papo kwa papo.Huyu ameshawahi shiriki mdahalo gani mpaka tuseme tumempima uwezo wake? achilia mbali ya mambo aliyowahi kufanya kama mwanaharakati/kiongozi/kijana ambapo hana historia hiyo.

Wengi wa hawa watoto wa wakubwa kwanza hawana uzoefu na maisha halisi ya maiisha ya watanzania,sifa mojawapo ya kuwa kiongozi bora ni uwe na uzoefu na hali halisi ya maisha ya watu unaowaongoza.Wapo wenye umri sawa na Januar Makamba na wanauwezo mkubwa kuliko yeye tena mmara 1,000 ila kama ada,Chama Cha Mapinduzi kina mfumo mbovu sana wa kupata viongozi.Ndio maana leo hii vijana wengi wenye kuelewa mambo(wenye mwellekeo sahihi wa kimapinduzi/kimaendeleo) huwezi ukawakuta CCM.Hata ukifuatilia kwenye mitandao ya kijamii .

Misingi mibovu ya uongozi iliyowekwa na CCM ndio inapelekea wananchi kupumbazika na kufikiri kuwa watoto wa wakubwa ndio wenye uwelewa na sifa za kuwa viongozi.Uongozo si kazi ya kugawa urithi wa mali za marehemu kwamba wanafamilia ndio wanajua mali za marehemu na mgawanyo halisi/sahihi uweje.
Hawa tunaowaona leo kina Januar Makamba kina Hussen Mwinyi nk hawana muda mrefu itabaki historia kwa sababu Vijana wa kitanzania tumenyimwa nafasi kwa muda mrefu sasa kazi ni moja kujikomboa wenyewe kwa kutumia uwezo wetu binafsi kumshinda/kumwondoa mkoloni mweusi aliyejivisha joho la Chama Cha Mapinduzi.
 
We kwel mtoto wa mama!
Ongea point CHADEMA co ya Chaggaz
Bac kat ya wanaoleta udini we unaongoza
Soon utasema CHADEMA ya wakirsto na CCM ya waislan
Ndo mana mme waoa CUF
Daah!wat a fool
 
We kwel mtoto wa mama!
Ongea point CHADEMA co ya Chaggaz
Bac kat ya wanaoleta udini we unaongoza
Soon utasema CHADEMA ya wakirsto na CCM ya waislan
Ndo mana mme waoa CUF
Daah!wat a fool

mtoto wa mama ni wewe. janury yuko juu na mwamvita yuko juu. watoto wa makamba ni wachapa kazi wakubwa sana. Mwamtita kajiunga VODACOM 2008 oneni alipo sasa hivi. hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa. Januayr kaingia ikulu 2006 angalia alipo. Mtabaki na wivu tu huko CHADEMA. Na weni wanaoonewa wivu ni waislamu. Nyie wote mmetumwa na JK kumchfua January. January mwendo mdundo hadi hao mafisadi wacheza kiduku watoke ikulu
 
Binafsi hasira zangu ni kwa wale wanaobebwa wakati uwezo hawana kabisa, au wana elimu lakini sio real experience bali ile ya kupandikizwa aka kimbizwa kimbizwa !
Tena mimi siangalii sana mtu km january ambaye hata kabla ya uchaguzi, zilivuja kuwa anaandaliwa kwa kyeo na nadhani hiyo pia ilizidisha kiburi chake . Wapo wengine katika mashirika na taasisi mbalimbali ambao wamepewa ajira, vyeo, tripu na kila aina ya favors just kwa majina yao. Tena na wengine imefika mpaka bf au gf zao, washkaj wao nk nao wanaota pembe na wanakuwa hawaguswi hata wakifanya makosa.

Mbaya zaidi ni kwa wale wanaopewa dhamana za hata "kubeba" roho za watu iwe ktk sekta za utatbibu, ukaguzi au hata usafiri. kuna dogo mmoja mpiga maji sana, na aliambulia nunge shuleni lakini akaajiriwa kwa zengwe na kwenda kusomeshwa nje ili kuwa kurusha ndege za taasisi flan. Huyu dogo anaendesha huto tududu km anaendesha samurai na kuna siku aliporomoka nako mashambani (uzuri wa ganja wala sio muoga....) akakashiti huko na kudandia boda boda barabarani na kuingia barakuda na kuanza kukata maji km kazi (watu wakawa wanashangaa shati jeupe lina dam). Ila kwa vile wanamjua.. hawakushangaa mpaka pale alipokutwa usiku wa manane chakari huku polisi wakiwa wanamtafuta kwa kudhani kaumia au kafia mashambani..

Huu ni mfano mmoja, wapo wengi waliongizwa majeshini (polisi, magereza..) na kugawiwa manyota kibao, na wengine ndo hao hao wachora michoro ya ujambazi kila siku, wapo wanaopangiwa "maeneo mazuri" tuu ili kuchuma vizuri na kuendeleza libeneke la ufisadi, na wale akina Kinjeketile, wanaoibua miradi na tenda zozote anazotaka, tishia au piga watu risasi halaf kesi zinaishia uvunguni, hata wale majizi waliopigisha cheki kibao na ghafla wamerudi hapa bongo na kupatiwa vyeo tena ktk mabenki...
 
Huo ni utamaduni huko Tanzania na hakuna wa kumlaumu na wala mwenye uwezo wa kujitanzua na hilo.

Hata Chadema ni hivyo hivyo.
Mbowe ni zao la Mtei ( Mkwe)
Dr Slaa amemweka mkewe mbunge viti maalum.
Tindu Lissu kamweka dadaye na wengine wengi.

Lakini Makamba kumweka Mwanane inakuwa kama kihoja.
Acheni unafiki.

Mkuu hapo kwenye RED kuna tatizo kidogo. Si kweli kuwa ujinga unaofanywa na CCM na CDM ndiyo utaratibu wetu watanzania.

Naamini ni tabia mbaya sana anayozidi kujengeka, na kama hatutakuwa makini ni kweli uongozi utakuwa wa watu fulani na mwisho wake tutaurudisha mikononi mwa wananchi kwa njia hizi hizi za Arab Spring!

Siyo kweli kwamba hao watoto wa vigogo ndiyo wazuri katika uongozi bali wengine wengi wenye uwezo zaidi ya hao watoto hawapewi nafasi ya kuonyesha uwezo wao PERIOD


 
sio kweli kwamba nyerere hakuruhusu, mwenyewe ni mtoto wa chief na amepata hiyo preveledge na kina rupia mifano kwa uchache tu, wakina warioba, msuguli na gama si mashemeji wajomba n.k

hii ni afrika bana?
 
Mada yako Boss ni ya muhimu na si CCM peke yao bali hata CHADEMA manake nao wanatia mashaka sana ukiangalia wanavyopeana ubunge wa viti maalum. Makala ya Johnson iwe funzo kwetu tusijefika kuleeeeeee!
 
Back
Top Bottom