January Makamba aiagiza TANESCO isikodi mitambo ya dharura. Ataka mradi wa Rufiji usicheleweshwe

Ngoja wakina Moto Matiko Mabanga wamchoree michoro ataingia mwenyewe kwenye 18 za kukodi.
 
Ukiona wanaanza kutaja taja kitu ujue kuna jambo...
Kodisheni tu mitambo...
Tumekuwa taifa la kukimbilia kila ushauri wanaotoa mulaya( sitaki kutumia hilo neno mzungu). Hivi juzi tu balozi wa Denmark alitoa twit ya hiki hiki alichokisema 'Mwezi wa kwanza'!
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amelielekeza Shirika la Umeme (TANESCO) kuhakikisha kwamba pamoja na kadhia ya umeme inayoendelea, Shirika hilo lisijiingize kwenye kukodi mitambo ya dharura kutokana na historia mbaya ya mitambo ya aina hiyo kuwa na gharama kubwa kwa Serikali na kugubikwa na utata mwingi.

Badala yake Makamba amelielekeza Shirika kuhakikisha kwamba linaongeza miradi mipya ya uzalishaji umeme kwa njia ya upepo na jua ambayo inaweza
Kwa hiyo sio matengenezo tena?
 
Huyu jamaa maneno mengi kama chiriku. Dr. Medard alitenda kazi bila uchiriku. Naona January anatuandaa kisaikolojia kwa dili zao za kifisadi.
bila shaka umeyasikia maneno haya:
Badala yake Makamba amelielekeza Shirika kuhakikisha kwamba linaongeza miradi mipya ya uzalishaji umeme kwa njia ya upepo na jua ambayo inaweza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja ili mwakani katika kipindi kama hiki cha ukame Taifa lisikabiliwe tena na uhaba wa umeme.
HAPA ndipo anajiandaa kuvuta 10% yake!
 
Sikubaliani na Makamba kwa sababu kuongeza miradi mipya ni process sio swala la overnight..

Kwa hiyo Mgao uendelee Kisa kuogopa vimaneno vya kijinga vya wafitini wake? Hizo mgwt xaidi ya 300 unaweza zipata fasta kwenye upepo? Makamba acha ujinga na jifunze kusimamia unachokiamini sio kuyumbishwa na maneno ya wapuuzi..

Makamba anakosa kujiamini kwa vile anahangaika na mitandao,mitambo ya mafuta sio mipya na mikoa mingi tuu bado inatumia majenereta.Kwa hiyo tuendelee kutumia kwa Mgao Kisa unaogopa kusema wawashe mitambo ya mafuta?
JPM alikua akiamua kitu, hajali mtasemaje, yeye atafanya tu, mlie mcheke atafanya,,
Hatuwezi kuwa tunaongoza huku tunaogopa mtandaoni watasemaje,, tunachopaswa kuangalia ni end product,, kwisha,,
Hao hao waluokuwa wanamsema jpm vibaya leo wanammiss
 
We blame a lots,but let gives her more chance #January we are with you,be passion, watu walishazoea mserereko,sasa hili la gafla linaletea tabu kidogo watanzania.
LET BE PASSION.
Loh! Hii ni lugha gani? Kama unaipenda hii lugha, nenda darasani. Mwanangu wa std 1, anakushinda. Siyo kwa kukutania, I mean it.
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amelielekeza Shirika la Umeme (TANESCO) kuhakikisha kwamba pamoja na kadhia ya umeme inayoendelea, Shirika hilo lisijiingize kwenye kukodi mitambo ya dharura kutokana na historia mbaya ya mitambo ya aina hiyo kuwa na gharama kubwa kwa Serikali na kugubikwa na utata mwingi.
Ndugu Waziri kaongea vyema. Wengi tunasubiri mradi wa JNHP uangaze nchi. Tukikamilisha huu mradi wa Rufiji itakuwa rahisi mno kwa nchi yetu kuwa na Dira ya miaka 50 mbele kwa kupanga miradi mingine mikubwa.
 
We blame a lots,but let gives her more chance #January we are with you,be passion, watu walishazoea mserereko,sasa hili la gafla linaletea tabu kidogo watanzania.
LET BE PASSION.
Andika tu kiswahili mkuu utaeleweka kisungu kimekupita kushoto.
 
Nimesikia ana rafiki zake anataka kuwapa dili la umeme wa UPEPO ndio anatafuta pakuanzia nini?
 
kwanza atuambie ,amezipata mashine/mitambo ya kuinulia mifuniko ya bwawa !?,au ndo amesahau !!sifa ya muongo ni uwezo wa kutotunza kumbukumbu!!
 
JPM alikua akiamua kitu, hajali mtasemaje, yeye atafanya tu, mlie mcheke atafanya,,
Hatuwezi kuwa tunaongoza huku tunaogopa mtandaoni watasemaje,, tunachopaswa kuangalia ni end product,, kwisha,,
Hao hao waluokuwa wanamsema jpm vibaya leo wanammiss
Kwa hiyo hata wakitaka kutuibia wakisema kwisha! Tupende tusipende kwisha! Hiyo hutokea tu endapo unalotaka kufanya Ni la haki na unaamini hivyo 100 % sio kwa Jambo ambako hata dhamira yako binafsi inakataa,haiwezekani bosi wangu la sivyo unapaswa kuwa na roho ya mwendawazimu.
 
Pia amewaelekeza TANESCO ...wajibu wangu ni.... kuisimamia TANESCO ipasavyo ili itimize wajibu wake na tuondokane na kadhia hii haraka iwezekanavyo”

anhaaa... sasa anaongea lugha ya kazi yangu ni kuisimamia na kuielekeza TANESCO...

siku ya kwanza alipoteuliwa akasema hataki kuletewa issue za TANESCO, hataki wanasiasa kuingilia TANESCO, alidhani kazi ya waziri ni kwenda Uarabuni na Ulaya kusaini mikataba...

tukamwambia you are out of your freaking mind...umeme ukikatika ni WEWE MAKAMBA, MAHARAGE, MAJALIWA, SAMIA na KIKWETE!
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom