January Makamba aiagiza TANESCO isikodi mitambo ya dharura. Ataka mradi wa Rufiji usicheleweshwe

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,413
7,678
Waziri wa Nishati, January Makamba amelielekeza Shirika la Umeme (TANESCO) kuhakikisha kwamba pamoja na kadhia ya umeme inayoendelea, Shirika hilo lisijiingize kwenye kukodi mitambo ya dharura kutokana na historia mbaya ya mitambo ya aina hiyo kuwa na gharama kubwa kwa Serikali na kugubikwa na utata mwingi.

Badala yake Makamba amelielekeza Shirika kuhakikisha kwamba linaongeza miradi mipya ya uzalishaji umeme kwa njia ya upepo na jua ambayo inaweza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja ili mwakani katika kipindi kama hiki cha ukame Taifa lisikabiliwe tena na uhaba wa umeme.

Pia amewaelekeza TANESCO kama Msimamizi wa mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere, Rufiji, ihakikishe kwamba mradi huo hauchelewi kwa kiwango kikubwa ili nao uchangie katika majawabu ya kudumu ya upatikanaji wa umeme nchini.

Waziri Makamba amewasihi Wananchi wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wakati TANESCO ikihakikisha kwamba inadhibiti upungufu wa uzalishaji kwa njia mbalimbali ——— "Nimeingia katika nafasi hii katika siku 70 tu zilizopita, wajibu wangu ni kumsadia Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan, na kuisaidia nchi yetu, kwa kuisimamia TANESCO ipasavyo ili itimize wajibu wake na tuondokane na kadhia hii haraka iwezekanavyo”

Millard

Makamba January.JPG
 
Bomba la gesi toka Mtwara-Dar lipo na linatumika kwa 6% tu - ni kweli hatujamsikia Waziri akigusia pande hizo.
Hapo wanataka kuanzisha miradi ya jua na upepo ili ibume waje waseme kuna shida ya upepo na jua kwa hiyo wanarudi kwenye gasi. Ujinga mtupu
 
Sikubaliani na Makamba kwa sababu kuongeza miradi mipya ni process sio swala la overnight..

Kwa hiyo Mgao uendelee Kisa kuogopa vimaneno vya kijinga vya wafitini wake? Hizo mgwt xaidi ya 300 unaweza zipata fasta kwenye upepo? Makamba acha ujinga na jifunze kusimamia unachokiamini sio kuyumbishwa na maneno ya wapuuzi..

Makamba anakosa kujiamini kwa vile anahangaika na mitandao,mitambo ya mafuta sio mipya na mikoa mingi tuu bado inatumia majenereta.Kwa hiyo tuendelee kutumia kwa Mgao Kisa unaogopa kusema wawashe mitambo ya mafuta?
 
Seems kama Wizara imemshinda!! Hivi alipotoa wiki mbili kusiwepo na kukatika umeme itakuwa alikurupuka?
 
Sikubaliani na Makamba kwa sababu kuongeza miradi mipya ni process sio swala la overnight..

Kwa hiyo Mgao uendelee Kisa kuogopa vimaneno vya kijinga vya wafitini wake? Hizo mgwt xaidi ya 300 unaweza zipata fasta kwenye upepo? Makamba acha ujinga na jifunze kusimamia unachokiamini sio kuyumbishwa na maneno ya wapuuzi..

Makamba anakosa kujiamini kwa vile anahangaika na mitandao,mitambo ya mafuta sio mipya na mikoa mingi tuu bado inatumia majenereta.Kwa hiyo tuendelee kutumia kwa Mgao Kisa unaogopa kusema wawashe mitambo ya mafuta?
Nadhani kaongelea habari za mwakani..
 
We blame a lots,but let gives her more chance #January we are with you,be passion, watu walishazoea mserereko,sasa hili la gafla linaletea tabu kidogo watanzania.
LET BE PASSION.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom