January Makamba adai mbele ya Dr. Bashiru kwamba ukweli umekuwa adimu ndani ya CCM. Watu wengi wameumizwa kwa mambo ya uongo

Tafunaneni tu, Lissu alivyoyasema haya ya kuhusu kuonewa mlimwona hafai siyo.

Sasa huyo unayesema asimamie HAKI na UKWELI ndani ya CCM ndiye huyo huyo aliyebariki ule uhuni wa uchaguzi Serikali za mitaa ili uwe ukweli - Unafikisha mashikataka to a wrong person.

Mfumo wa umbeya, kusengenyana, kujikomba komba kumetawala ndani ya CCM, maana bila kufanya hivo huwezi kuishi humo.
 
January bado hajaiva! Na mtu yeyote atakayemsifia kwa kuongea vitu alivyoviongea basi hajui siasa.
 
..Je, anayoyasema January Makamba yana ukweli?

..kwamba ndani ya CCM ukweli umekuwa nadra, na uongo umekuwa na nguvu.

..pia anadai viongozi wameumiza wanachama kwa kuamini taarifa zisizo za kweli wanazopelekewa.

..sikiliza video clip hapa chini.


January ulishiriki dhambi ile , lakini inafahamika kwamba Mshahara wa dhambi ni mauti
 
Na bado, alijisemea Lissu na Lema, wakimalizana na sisi watarudi na kwenu pia. Kunyweni kikombe hicho ni cha kwenu
 
Kweli ccm ukweli ni adimu. Kabla ya huyu wa sasa wapinzani walimsema sana Jk. Vinara ccm walipinga kwa nguvu zote. Alivokuja huyu wa sasa wapinzani wansema sana kwa mambo mengine na vinara wanapinga kwa nguvu zote na wanamsema yule wa zamani hadharani kwa pointi zilezile za waponzani. Juzi kinara mmoja kamshutumu JK hadharani na kumsifu wa sasa. Mbona wakati ule hawakumsema Jk kama wanaupenda ukweli. Inaonyesha huyu wa sasa akitoka tu nao wataanza kumsema. Ukweli ni mgumu kama jiwe kutafuna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, anayoyasema January Makamba yana ukweli?

Kwamba ndani ya CCM ukweli umekuwa nadra, na uongo umekuwa na nguvu.

Pia anadai viongozi wameumiza wanachama kwa kuamini taarifa zisizo za kweli wanazopelekewa.

Sikiliza video clip hapa chini.



Huo ndio ukweli kuwa CCM ni waongo.
IIa ni wanaccm wachache sana wenye ujasiri wa kusema hilo.

Hapo utasikia anahujumu chama, kwa kutounga mkono ilani ya ccm.
 
Back
Top Bottom