January Makamba Adai Magazeti Yanampendelea LOWASSA Kwa Kumpigia Kampeni

makambaz.jpg


Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ameonesha kutokubaliana kwake na ripoti za kinachojili kwenye mikutano ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na kueleza kuwa Magazeti hutumiwa kupiga kampeni.

Makamba ameeleza hayo kupitia mtandao wa Twitter baada ya mtu mmoja anaetumia jina la &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Gachanja Muigai', kumueleza kuwa kutokana na kile wananachokisoma, inaonekana kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono Lowassa. Na akataka kupata maoni ya Makamba kutokana na hali hiyo kama anadhani wataweza kushinda.

"@JMakamba From what we read here, it seems [HASHTAG]#Lowassa[/HASHTAG] is resonating with Wananchi. Una hakika si wakati wa kuvuka sakafu?" Aliuliza.

Makamba alimjibu kuwa wapinzani wanatumia baadhi ya magazeti kama sehemu ya kampeni zao lakini tafiti na hali halisi nchini inaeleza tofauti.

"They've turned some newspapers into their campaign fliers. But the polls & mood across Tanzania tell another story."


Maoni yangu:-
Hivi kiongozi kama huyu anavyoongea vitu kama hivi anajiweka katika kundi gani? kwa uhalisia unaonekana kwenye TV mbali mbali isipokuwa TBC sasa anavyo sema magazeti yanampendelea Lowasa vipi kuhusu gazeti la UHURU na MZALENDO anaweza kutuambia linampendelea nani?
Naona anashindwa kuelewa habari inayouza kwa sasa ni LOWASSA na ndio habari ya Mjini, Vijijini na kila sehemu ndani ya nchi hii na ningemuomba leo aende sehemu yeyote kwenye mkusanyiko wa watu wanapoangalia taarifa ya habari saa mbili usiku na aangalie kama itaanza habari ya Lowassa kabla ya Magufuli je watu wataendelea kuangalia hiyo taarifa ya habari?
Angejua hata yeye Makamba angempigia kampeni Lowassa
 
Back
Top Bottom