January Makamba Adai Magazeti Yanampendelea LOWASSA Kwa Kumpigia Kampeni

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
makambaz.jpg


Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ameonesha kutokubaliana kwake na ripoti za kinachojili kwenye mikutano ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na kueleza kuwa Magazeti hutumiwa kupiga kampeni.

Makamba ameeleza hayo kupitia mtandao wa Twitter baada ya mtu mmoja anaetumia jina la ‘Gachanja Muigai', kumueleza kuwa kutokana na kile wananachokisoma, inaonekana kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono Lowassa. Na akataka kupata maoni ya Makamba kutokana na hali hiyo kama anadhani wataweza kushinda.

"@JMakamba From what we read here, it seems #Lowassa is resonating with Wananchi. Una hakika si wakati wa kuvuka sakafu?" Aliuliza.

Makamba alimjibu kuwa wapinzani wanatumia baadhi ya magazeti kama sehemu ya kampeni zao lakini tafiti na hali halisi nchini inaeleza tofauti.

"They've turned some newspapers into their campaign fliers. But the polls & mood across Tanzania tell another story."


Maoni yangu:-
Hivi kiongozi kama huyu anavyoongea vitu kama hivi anajiweka katika kundi gani? kwa uhalisia unaonekana kwenye TV mbali mbali isipokuwa TBC sasa anavyo sema magazeti yanampendelea Lowasa vipi kuhusu gazeti la UHURU na MZALENDO anaweza kutuambia linampendelea nani?
Naona anashindwa kuelewa habari inayouza kwa sasa ni LOWASSA na ndio habari ya Mjini, Vijijini na kila sehemu ndani ya nchi hii na ningemuomba leo aende sehemu yeyote kwenye mkusanyiko wa watu wanapoangalia taarifa ya habari saa mbili usiku na aangalie kama itaanza habari ya Lowassa kabla ya Magufuli je watu wataendelea kuangalia hiyo taarifa ya habari?
 
mwambieni akimaliza kusoma UHURU awe anasoma pia HABARI LEO,JAMBO LEO na DIRA YA MTANZANIA ili asuuzike na roho yake kwa habari zinazosifia ccm.magazeti ya watu makini kv MWANANCHI,NIPASHE,MTANZANIA kwake ni ya upinzani! ati aliingia tano bora ccm huyo.ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.
 
Magazeti mpaka hayaandiki ya bomba LA gesi badala yake linaandika na kuweka picha ya wahuni kupiga deki?! anyway ..wataelewa kwamba maharage si mboga kuanzia 25 na hapo vijisenti walivyopewa vitakuwa vimeisha na njaa kari itawatafuna, ndipo watajirudisha wenyewe kuandika habari za serikali
 
Magazeti mpaka hayaandiki ya bomba LA gesi badala yake linaandika na kuweka picha ya wahuni kupiga deki?! anyway ..wataelewa kwamba maharage si mboga kuanzia 25 na hapo vijisenti walivyopewa vitakuwa vimeisha na njaa kari itawatafuna, ndipo watajirudisha wenyewe kuandika habari za serikali
Ni kweli mkuu utakuwa unalia na kusaga meno wakati CCM itakuwa chali.
 
ndio kujichungulia nyeti huku..Magazeti karibu yote yanatangazo la CCM ukurasa wa mbele..
 
kwa upande wa wagombea urais mgombea wa ccm anapendelewa sana na media. tbc, star tv, tbc fm,redio uhuru na hata cloufs fm habari zao 100% ni za kuibeba ccm. pia magazeti ya jambo leo,habari leo na hata zanzibar leo huipendelea c kwa kiasi kikubwa...
 
Ccm,fulana bure, kofia bure, usafiri kwenda kwenye mikutano ya kampeni bure wataweza nunua magazeti?
 
Christopher Cyrilo > ‎MWANAHALISI FORUM
MWENZANGU NA WEWE NI MWANACHAMA WA CCM?
Taarifa zinasambaa, kwamba msanii nguli wa muziki wa bongo fleva, Diamond, amelipwa Tsh. 1.3 bilioni kwa ajili ya kufanya kampeni za CCM, Wema sepetu ambaye amewahi kuripotiwa kucheza filamu za ngono, amepewa Tsh. 600 milioni. Kuna wasanii karibu 30 wanaofanya kampeni za CCM huku wakilipwa na CCM. Mabilioni ya pesa yanatumika huko kwa ajili hiyo.
K/mkuu Kinana anaripotiwa kujichukulia karibu Tsh. 3 bilion kutoka mfuko wa kampeni kisha akatoa taarifa kwa JK kuwa pesa za kampeni zimeisha. Alipoulizwa zimeishaje akajibu, Diamond Bil. 1.3, Wema mil. 600, wamekifanyia nini Chama? Mimi nimezunguka nchi nzima kukinadi chama nimepata nini, sasa nimechukua na sirudishi. Hapo K/mkuu alikataa kuwa msumari, utaelewa baadae.
Sio hivyo tu, humo humo kwenye kampeni kuna wapigaji wanafanya kazi yao. Ukisikia CCM wamekopa mabilioni ya pesa kutoka CWT, na kuuza hisa za TBL kwa bil. 80, ili zisaidie kampeni usidhani zote zinakwenda kwenye kampeni, nop, watu wanajiandalia maisha baada ya uchaguzi. Kuna dalili bilioni 1.3 na ishara milioni 600 za CCM kukosa Urais, kwa hiyo lazima watu wajiandae kuishi ndani au nje ya Tanzania baada ya kutolewa kwenye utawala.
Sasa wewe mwenzangu na Mimi, unayetoka mishipa kushabikia CCM, wewe ni kada au mtoto wa kada gani maarufu? Wewe ni mwanafamilia wa kada gani anayelalia mabilioni ya Shilingi za walipakodi? Na wewe ni mpigaji? Au unajiandaa kuwa mpigaji? Una undugu nao? Au unajipendekeza tu ili upate nafasi ya kupiga pesa baadae?
Baba ako analipwa ngapi? Mama ako analipwa ngapi? au anajichukulia ngapi? Kwako wewe gharama za maisha haziongezeki sio? Huduma mbovu za elimu haikuhusu eti ee? Ukisikia wanyama wamepandishwa ndege kutengeneza vituo vya utalii huko ughaibuni wewe huna habari, unatafuta majibu au matusi kwa watu wanaopinga hayo mambo. Unajiita CCM kwa fulana na elfu 10, huwezi kujitafutia hivyo vitu kisha Ukawa huru kupambana na wanyang'anyi? Wana CCM wenzako wananufaika na meno ya tembo na biashara za dawa ya kulevya wewe ni mmoja wao? Unashinda mitandaoni kupost picha za kampeni za magufuri wakati wenye CCM wanakula maisha, wanatuachia maiti za tembo, mateja mitaani na mashimo matupu migodini, wao wanakesha baa, wakitoka na maV8 yao haaoo kwenye mahoteli ya kifahari, wakitoka humo ni ughaibuni.
Na wewe unafanya hivyo? Kama ndio basi 'big up', Ila kama unatukana tu, unahangaika kuitetea CCM kwa buku 10, basi angalia vizuri nembo ya CCM utaona kuna alama ya NYUNDO, na wewe umechagua kuwa MSUMARI, kazi ya nyundo ni kugonga misumari, kwa hiyo wewe unagongwa na CCM. Na Kamwe masumari haugeuki kuwa Nyundo.
Utaishia kugongwa tu na Mimi nasema ugongwe tu maana hamna namna nyingine.
1 hr · MWANAHALISI FORUM
More
 
Back
Top Bottom