January magamba kwa madudu yote haya umekubali kuhujumu juhudi za wazalendo bungeni!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January magamba kwa madudu yote haya umekubali kuhujumu juhudi za wazalendo bungeni!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by richone, Apr 22, 2012.

 1. r

  richone Senior Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nilisikitishwa sana na muongozo aliouomba January Magamba! najua ni mpango aliousuka yeye na mafisadi wenzake ili kuhujumu jitihada za wazalendo wanao pigania usawa katika taifa hili. najua yeye anasema anajua mengi ndio maana hachongi ila kuna ambao hawajui mengi ndiyo maana wanachonga! naomba nimwambie ukweli nilisikitika sana alipojidai anauliza swali huku akijinafikisha lengo lake ni kuweka umoja katika bunge na kuwafanya wabunge kuwa wamoja.
  Namwambia Janary Magamba niliamini yeye alikuwa tofauti sana na Baba yake Mzee Magamba lakini nimejiridhisha hana tofauti hata kidogo na baba yake. Ni kweli tunda huanguka chini ya mti, kwa haya sina imani tena naye na ajue hakuna siku atakaa aaminike hata kama atatumia kigezo cha viongozi vijana yeye sii role model yetu tena na najiandaa kwenda kuwaelimisha wananchi jimboni kwake naamini mchango wangu utasaidia kumfanya akose huo ubunge kwani ni msaliti mkubwa kwa watanzania.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Ukiusikiliza ule muongozo aliouomba January, katika sheria kuna maswali fulani yakiulizwa huwa yanapigiwa objection kwa sababu wanasema yanamuongoza shahidi (leading the witness).

  Hutakiwi kuuliza "ulipofika pale ulikiona kisu chenye damu mbichi mkononi mwa mtuhumiwa?". Badala yake unatakiwa kuuliza "Uliona nini mkononi mwa mtuhumiwa". Kwa sababu swali la kwanza limemsaidia shahidi kujua jibu fulani na anaweza kukubali bila ya ukweli. Lakini la pili halimuongozi katika jibu.

  Yaani swali anaulizwa Spika kama January anaomba muongozo wa Spika, lakini ukilisikiliza kwa makini utaona swali ndilo linamuongoza Spika ajibu vipi.

  Nilivyosikia hivyo tu nikaona January anafanya kazi yake ya kuitetea serikali ya CCM.

  Huyu jamaa yuko pale kutetea status quo, full stop.
   
 3. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  January makamba ni kama fisi anamvizia mtu anapotembea kwa matumaini ya mkono kudondoka tu hauokote mwisho wa safari huambulia patupu.Kimoyomoyo January anaomba hoja hii hipite kwa mawazo ya kupata uwaziri.
   
 4. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijawahi kuwa na imani na Mwezi wa kwanza Makamba tangia siku ilipoleak kwamba aliombewa sponsorship na JK (yeye na Jairo) ya kwenda US nilijua something is wrong with him. Pia ishu ya kuombewa hela za kampeni na dada yake kwa kutoa rushwa ya.......... basi kabisa.
   
Loading...