Thanks MMKJ,
My take:
Netgroup walitumia maji mengi kuzalisha umeme!! kivipi. Ina maana walimwaga maji tu au. Mfano, Kama Cub.meter 100 zinatoa megawatt 1, ina maana labda netgroup walitumia Cub.m 150 kwa megawatt 1 !!. Engineers nisaidieni kunifahamisha.
Umeme unapotea njiani kwa miundo mbinu mibovu: Sasa NSSF wakianza kuzalisha kiwira si umeme huo utapotea njiani pia? wale tuliosema tatizo si makaa ya mawe au kiwira ni zaidi ya hapo tulikosea au kushambulia taasisi yoyote.
Viwanda athirika: Mbolea, Vodacom na viwanda vidogo! hee! kwanini vodacom na si Airtel, Tigo, Breweries, cements, Irons, textiles n.k!
Watu wanashangaa kwani hatuwashi na mashine zipo: January! january! si wabunge wa CCM walisema hapana Ubungo plaza, si rais wako alisema hata yeye hakubali malipo Dowans. Sasa umeme ungewashwaje bila kulipa Dowans. January mamilioni ya watu walioandamana na baiskeli wakisema Dowans hapana hao hukuwaona, au una maana watu ni akina nani. January !
Stielger Gorge: Tatizo si mazingira. Michoro ya kwanza ya mradi huu ulichorwa na wajerumani.( Chuo kikuu au nyaraka za serikali wanazo ). Hili la mazingira umelitunga wewe na wenzako. Ipo proof ya mradi huu kuanzia enzi German rule.
Badilisha sheria za manunuzi: Ok! Ili tununue Dowans ya rafiki yako.
Binafsi navutiwa na jitihada za January na inaniwia ngumu kuamini kwamba yupo kutetea maslahi ya wachache, tumuunge mkono kijana mwenzetu kwa maslahi ya Taifa letu Tanzania