January kwenye Power Breakfast: Aelezea tatizo la Mgao wa Umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January kwenye Power Breakfast: Aelezea tatizo la Mgao wa Umeme

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 30, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Anasema miaka 10 iliyopita serikali iliamua TANESCO ibinafsishwe; anatoa historia ya mgao; walipokuja NETGROUP solutions kuendesha TANESCO, walitumia maji mengi kuzalisha umeme.Hawakuwekeza kwenye chochote hasa miundombinu hivyo tatizo likaanza ukichanganya na uhaba wa mvua.

  Walitumia jitihada kubwa kukusanya madeni kwa vile mkataba uliweka kipengere cha bonus .So walikazana sana kukusanya madeni kwa sababu ya motisha wa bonus. Mwaka 2006 SERIKALI IKARUDISHA TANESCO serikalini. Matatizo y aumeme kwa kiasi yanatokana na mambo mengi. Haijakuwepo big investment katika uzalishaji hata ugavi.

  Pia anasema kuwa umeme mwingi unapotea njiani kutokana na uchakavu wa miundo mbinumore than 20% ya 1100MW inayozalishwa. Anasema umeme unapotea mathalani, ni mwingi kuliko ule unaozalishwa na Songas!

  Anaelezea matatizo ya umeme:

  a. Kiwanda cha MBolea kufungwa mara tatu
  b. Vodacom wanatumia fedha nyingi
  c. Viwanda vidogo


  Anasema wananchi wanalalamika na kuwauliza kama "wana akili" kwamba watu wanawashangaa iweje iwepo mitambo ipo imezimwa. Anasema yapo mapendekezo 30 la kuwasha mitambo ya Dowans ni moja tu.

  Ameulizwa swali "kwanini miaka mitano ya kwanza Serikali haikuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme?" Jibu lake: "Swali unaloniuliza ndilo na mimi nauwaliza serikali" (akimaanisha barua yake kwa Ngeleja).

  Anaelezea suala la Stielger's Gorge anasema tatizo limekuwa ni suala la mazingira ndio limechelewesha sana. Anasema lakini sasa hivi jambo hilo linazungumzika na kuwa wapo taasisi binafsi ambazo wako tayari kuwekeza (akigusia suala la RUBADA na Brazili). Kwa hiyo anasema ni suala la kulinda maslahi ya "mazingira" na yale ya wananchi.

  Ameuliza kuhusu suala la Dowans na anakiri kuwa Mtambo haujawashwa na anakiri ni kwa sababu ya "unafuu uliopo sasa kwa sababu ya mvua" lakini anasema kuwa "ni unafuu wa muda". Anasema kwa sababu mabwawa yaliyojaa maji sasa hivi ni yale yanayotegemea maporomoko ya maji (water falls) lakini siyo yale mabwawa ya hifadhi (water reservoir) kama Mtera.

  Anaunga mkono kubadilisha sheria ya manunuzi ya umma ambayo itaruhusu manunuzi ya vitu vilivyotumika. Anasema kwa mfano nchi kama za kwetu na mazingira yetu na ya kibiashara dunia ni vizuri kuruhusu manunuzi hayo. Anasema sheria lazima iwe "flexible". Anasema nchi kama za kwetu haziwezi kupata vitu vipya kila wakati na anatolea mfano wa ndege.

  Ameulizwa "kuna emergency ya kununua ndege"? anasema hata barabara siyo emergency - wanacheka tu - kwani anaambiwa kuwa mambo mengine ni ya mipango ya muda mrefu. Anasema "udharura" mwingine ni wa kujitakia. Anadai kuwa ( naamini kwa makosa) kuwa huwezi kwenda kununua mtambo wa kuzalisha umeme MW100 ni lazima usubiri miaka miwili.

  Anasema kuwa serikali inataka kukodisha mitambo ya Tanesco ya 260 na amewatumia ujumbe Tanesco kuwa ahadi yao isipotimizwa basi "watakamatana" na "kuulizana vizuri" huko Dodoma.


  Ametoa wito kwa watu ambao wameathirika na uchakachuaji wa mafuta wafike ofisi za Bunge jijini Dar leo ambao wanakusanya maoni ya nini cha kufanya.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Msikilize tu, mwishoni lazima atapigia kampeni serikali kununua mitambo CHAKAVU ya Dowans!
  Yuko kikazi fulani zaidi huyu dogo!
   
 3. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Radio yenyewe ni ccm, hadi hao wakurugenzi, hapo katumwa kuweka mambo ya serikali yao sawa
   
 4. K

  Kalila JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hana jipya kaulizwa y govt imeshindwa kuendesha mitambo ya mafuta mazito kama iptl na ile ya mwanza wakikodi hiyo ya 260mw wataiweza kweli anachekacheka 2 ubunge wenyewe kapata bila ridhaa ya wananchi hana jipya kilaza tu
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Vodacom kutumia pesa nyingi, imenishangaza kidogo.
  Kulikuwa na sababu ya kuizungumzia Vodacom?
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  anaonekana kuelewa mambo mpaka unajiuliza jinsi TZ "ilivyojaliwa kuwa na vichwa'!!
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kule si kuna ndugu yake jina limenitoka mwishoni Makamba

  Labda aliteleza tu akamkumbuka ndugu yake.

  Hao Voda juzi si walikuwa kwa rais Ikulu hapo.
   
 8. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Wanaume kama mabinti!
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Mbona hajasema kuwa suala la umeme liko mikononi mwa JK toka 1988?
   
 10. H

  Haika JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kama ningekuwa naulizwa kama mitumba ya mitambo itumike ningekataa, lakini offcourse hakuna atakaetaka maoni yangu
   
 11. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Amekwenda kuwashukuru akina Gerald kwani walikuwa watu wa mwanzo kumpa airtime kabla ya kutangaza nia ya kugombea ubunge Juni mwaka jana.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Thanks MMKJ,

  My take:
  Netgroup walitumia maji mengi kuzalisha umeme!! kivipi. Ina maana walimwaga maji tu au. Mfano, Kama Cub.meter 100 zinatoa megawatt 1, ina maana labda netgroup walitumia Cub.m 150 kwa megawatt 1 !!. Engineers nisaidieni kunifahamisha.

  Umeme unapotea njiani kwa miundo mbinu mibovu: Sasa NSSF wakianza kuzalisha kiwira si umeme huo utapotea njiani pia? wale tuliosema tatizo si makaa ya mawe au kiwira ni zaidi ya hapo tulikosea au kushambulia taasisi yoyote.

  Viwanda athirika: Mbolea, Vodacom na viwanda vidogo! hee! kwanini vodacom na si Airtel, Tigo, Breweries, cements, Irons, textiles n.k!

  Watu wanashangaa kwani hatuwashi na mashine zipo: January! january! si wabunge wa CCM walisema hapana Ubungo plaza, si rais wako alisema hata yeye hakubali malipo Dowans. Sasa umeme ungewashwaje bila kulipa Dowans. January mamilioni ya watu walioandamana na baiskeli wakisema Dowans hapana hao hukuwaona, au una maana watu ni akina nani. January !

  Stielger Gorge: Tatizo si mazingira. Michoro ya kwanza ya mradi huu ulichorwa na wajerumani.( Chuo kikuu au nyaraka za serikali wanazo ). Hili la mazingira umelitunga wewe na wenzako. Ipo proof ya mradi huu kuanzia enzi German rule.

  Badilisha sheria za manunuzi: Ok! Ili tununue Dowans ya rafiki yako.
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni Mwamvita makamba.
  Tumbo moja na January.
   
 14. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Huyo dada anayeongea na JK ndiye ndugu yake, anaitwa Mwamvita
   
 15. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  sasa kwa Watanzania waungwana mnaanza kuona tambo za January zina slow down hata kabla ya 'robo' ya safari. Wengi walijua kuwa maneno maneno yote yale kumbe anatimiza masharti ya kuwa kwenye list ya 'payroll'. Mungu tunusuru na janga la kitaifa: CCM NA WATU WAKE
   
 16. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280

  basi kama ni hivyo tukubaliane na kuwa waungwana "TUWAONEE HURUMA (kama alivyowahi sema baba yake)" January na washirika wake/wao wauze mashine zao za DOWANS kwa TANESCO ilieile kama 'a special case' badala ya kubadilisha sheria

   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Sasa mpaka amshikeshike mbele ya mabosi wake?
   
 18. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  hivi alikwenda kuwania au alipewa tu ili kumwondoa nafasi ya u-PA wa mkulu baada ya kuvujisha issue ya mkulu kutaka kumtema baba yake nafasi ya ukatibu mkuu wa chama?
   
 19. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  kaaaaz kweli kweli.....mi hata lakusema sina manake naona ni sanaa tu inafanyika!
   
 20. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  mi kwa maona yangu ya fasta, huyo jamaa kwenye picha bado ana control hii gemu! View attachment 26048
   
Loading...