BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imesema mpaka sasa Tanzania haina Uhaba wa Mafuta, hivyo hakuna Sababu ya Watanzania kuwa na Taharuki ya Ukosefu wa Nishati hiyo Muhimu.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati, Januari Makamba katika mkutano wake na Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta hapa nchini.
Waziri Makamba amesema hakuna sababu kwa Wananchi kuwa na Taharuki ya Uhaba wa Mafuta kwa sababu bado ipo shehena ya kutosha ya Mafuta Kwenye Maghala yaliyopo na yale ambayo yanashushwa Bandarini.
"Hadi kufikia leo tunayo mafuta ya kutosha kutumika kwa takribani Siku 27, pia Serikali imeshaagiza mafuta yatayotumika Mwezi wa tano na wa sita ambayo yapo kwenye Mchakato," amesema Waziri wa Nishati January Makamba.
Source: Wasafi FM