Januari Makamba kukataliwa na Wajumbe 1,463 kati ya 1,915 inatoa taswira gani kisiasa?

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Januari Yusuph Makamba, Mwanasiasa kijana mwenye ushawishi mkumbwa ndani ya Chama cha Mapinduzi ambaye Mwaka 2015 aliingia 5 bora ya wagombea wa Urais.

Hivi majuzi tumeona kwenye uchaguzi wa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) akishika nafasi ya 11 kwa kupata kura kiduchu 452 kati ya kura 1915 kwa tasfiri nyepesi wajumbe 1,463 walimkataa kwenye sanduku la kura.

Ni nini hasa kimemdondosha kisiasa kijana huyu machachari kutoka 5 bora za Urais 2015 hadi nafasi 11 na kushindwa hata kuingia 10 bora licha ya taarifa kudaiwa ndiye mgombea aliyetumia pesa nyingi kuliko wagombea wote wa NEC.

pic-makamba.gif
 
Ni kura moja kwa mtu mmoja ? Huenda sio kwamba anakataliwa bali wengine wanapendwa zaidi yake...

Anyway binafsi nasema...
 
Januari Yusuph Makamba, Mwanasiasa kijana mwenye ushawishi mkumbwa ndani ya Chama cha Mapinduzi ambaye Mwaka 2015 aliingia 5 bora ya wagombea wa Urais...
Kiburi, kujisikia ana akili kuliko wengine, kuwa na baba anaeongea pasipo breki, kujulikana kuwa protegee wa Kikwete, kujisikia kuwa ndio raisi ajae, kusikia kwamba aliweka mashari apewe wizara gani na wafukuzwe wateule wa Magufuli Tanesco na wizarani, matatizo ya umeme, majibu ya uongo anapohojiwa au kuulizwa maswali, visingizio vya kumlaumu Magufuli katika kukatika umeme, kuwa na dada tapelitapeli, suala la kreni nk.
 
Januari Yusuph Makamba, Mwanasiasa kijana mwenye ushawishi mkumbwa ndani ya Chama cha Mapinduzi ambaye Mwaka 2015 aliingia 5 bora ya wagombea wa Urais.

Hivi majuzi tumeona kwenye uchaguzi wa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) akishika nafasi ya 11 kwa kupata kura kiduchu 452 kati ya kura 1915 kwa tasfiri nyepesi wajumbe 1,463 walimkataa kwenye sanduku la kura.

Ni nini hasa kimemdondosha kisiasa kijana huyu machachari kutoka 5 bora za Urais 2015 hadi nafasi 11 na kushindwa hata kuingia 10 bora licha ya taarifa kudaiwa ndiye mgombea aliyetumia pesa nyingi kuliko wagombea wote wa NEC.
Hiyo kauli ya "ushawishi mkubwa" ungeifuta kwanza ili tujadili hoja ya msingi.

Ushawi upi ikiwa amekataliwa na asilimia 95%. Au unazungumzia ushawishi kwa chama cha "mambuzi"
 
Kiburi, kijisikia ana akili kuliko wengine, kuwa na baba anaeongea pasipo breki, kujulikana kuwa protegee wa Kikwete, kujisikia kuwa ndio raisi ajae, kusikia kwamba aliweka mashari apewe wizara gani na wafukuzwe wateule wa Magufuli Tanesco na wizarani, matatizo ya umeme, majibu ya uongo anapohojiwa au kuulizwa maswali, visingizio vya kumlaumu Magufuli katika kukatika umeme, kuwa na dada tapelitapeli, suala la kreni nk.

That endless catalogue of January Makamba's epic failures and dishonorable family and political connections is astounding.
 
Back
Top Bottom