Januari makamba acha purukushani za Urais, huziwezi Baba!

Status
Not open for further replies.

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
Pirika pirika za January Makamba zimejikiti zaidi katika harakati zinazofanana na zile za kikwete alipokuwa anawinda urais. Hali hii inachagizwa na Watendaji wengi wa ccm hasa makatibu wa wilaya kupatikana kwa influence ya baba yake. Baada ya Baba yake kuenguliwa kwa aibu. amenyamaza kimya [huenda kuto-draw attention kwa jamii] ili mtoto aendelee kujiimarisha. Je haya ni maandalizi ya kugombea ile ofisi ya magogoni?
 
Kuna watu wamejipofusha na hawataki tena kutibu upofu wao. Ni jambo la hatari kuona watu walio katika system/mfumo wa nchi wanang'ang'ania kuishi katika historia badala ya kuishi katika uhalisia
Wanajiandaa kwa mambo mengi yajayo lakini hawaangalii nyakati wala mazingira, uwezo walio na wala wa wapinzano wao, wanategemea historia, as if wanajiandaa kupasua mawe.
 
Ni haki ya kila Mtanzania!! Mwacheni ajaribu bahati yake kwani kwa TZ ya Magamba lolote lawezekana!!
 
Kuna watu wamejipofusha na hawataki tena kutibu upofu wao. Ni jambo la hatari kuona watu walio katika system/mfumo wa nchi wanang'ang'ania kuishi katika historia badala ya kuishi katika uhalisia
Wanajiandaa kwa mambo mengi yajayo lakini hawaangalii nyakati wala mazingira, uwezo walio na wala wa wapinzano wao, wanategemea historia, as if wanajiandaa kupasua mawe.

Wanadai watatawala milele!
 
Nchi ishakua ya familia kama chama tawala ni cha familia basi na nchi ndio hivo tena kama mmeshindwa kuikomboa kaeni kimya manake mkiambiwa ufaham mnadai wanavunja amani ******i type!
 
Pirika pirika za January Makamba zimejikiti zaidi katika harakati zinazofanana na zile za kikwete alipokuwa anawinda urais. Hali hii inachagizwa na Watendaji wengi wa ccm hasa makatibu wa wilaya kupatikana kwa influence ya baba yake. Baada ya Baba yake kuenguliwa kwa aibu. amenyamaza kimya [huenda kuto-draw attention kwa jamii] ili mtoto aendelee kujiimarisha. Je haya ni maandalizi ya kugombea ile ofisi ya magogoni?

wachaga wanasema
waikukapa !!!??mleu nkiki see noanza
 
VIONGOZI WAZURI WA TANZANIA YA VIPINDI VYA HUKO BAADAYE HAWATOTOKANA KAMWE NA MAGENGE UCHWARA, VIMBELEMBELE, WALA-RUSHWA WALA WENE UCHU WA MADARAKA

Mkuu ikiwezekana basi karudie ujumbe huu walau mara 100 tu kwa sikio la Makamba na Zitto ili wapate kujua kwamba wenye kujitia kimbelembele na kujiketisha jukwaa kuu huenda wakaombwa tena kwa aibu kubwa kurudi kwenda kukaa kwenye viti vya kawaida kabisa nyuma ya mkusanyiko wa wenye kiu na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni vema wakamuulize Mhe Lowassa na jinsi sisi kama taifa tulivyomdelete kwa kuonyesha kukuru kakara nyingi mno ambazo watu tulifika mahali tukaanza kujihoji kwamba huyu mwenzetu kulikoni; mbona akilala anaota Magogoni, akiamka anayo Magogoni kichwani na hapa pale ukimuangalia sasa kwenye ibada kwa Nabii Emmanuel huonekana kukatishwa mtiririko wa misa rohoni pindi tu wazo la Magogoni linapokatisha tuu akilini?

Waheshimiwa Kitila Mkumbo, Benno Malisa, John Mnyika, Hlima Mdee, Kiwelu, Heche ... Millya na wengine wa aina yenu, hebu endeleeni na huo utaratibu wenu wa Uongozi wa Kutumikia Umma kwani huku nje ya uwanja tayari tumeshawaoneni mara baada ya uongozi wa Dr Slaa hapo 2025.

Na endapo mlikua mnajidharau huko na kuwa sababu ya nyinyi kuendelea kujichimbi viti vya nyuma basi tangu sasa mjue kwamba kiongozi mzuri hutambulika hasa pale ambapo hana fedha nyingi sana wala madaraka makubwa mno.

Nyinyi ni wasikivu, waadilifu na wachapakazi wenye matamanio makubwa kunufaisha jamii nzima ya tanzania na wala si kujikimbizia ovyo dili za kuangamiza taifa letu. Wenzenu huku tayari tumewasikia, tumewatambu, na tutawafikia kwa wakati mwafaka.

Kuna watu wamejipofusha na hawataki tena kutibu upofu wao. Ni jambo la hatari kuona watu walio katika system/mfumo wa nchi wanang'ang'ania kuishi katika historia badala ya kuishi katika uhalisia.

Wanajiandaa kwa mambo mengi yajayo lakini hawaangalii nyakati wala mazingira, uwezo walio na wala wa wapinzano wao, wanategemea historia, as if wanajiandaa kupasua mawe.
 
Urais wa 2015 - 2025 Dr Willibroad Slaa

Urais wa 2025 - 2035 Ni chaguo kutokana na wale anaowalea hivi sasa CDM na wale wa aina ya huko CCM

NB: Mungu awalinde na kuwaendelezea tabia njema za KUCHAGULIKA kwao.

Unamaanisha urais wa mwaka 2050.
 
acha wengine wahangaike rais 2013 ni Dr.slaa makamu wake ni Zitto kabwe...........hata vjjn wanalijua hilo. maana ya 2013 nkwamba kikwete hatamaliza miaka 5.
 
Urais wa 2015 - 2025 Dr Willibroad Slaa

Urais wa 2025 - 2035 Ni chaguo kutokana na wale anaowalea hivi sasa CDM na wale wa aina ya huko CCM

NB: Mungu awalinde na kuwaendelezea tabia njema za KUCHAGULIKA kwao.

Slaa hafai hajasoma...

Elimu yake ni kuungaunga...

PhD church management (anafaa sawa awe rais wa TEC)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom