Januari 5 na maadhimisho ya wapigania uhuru wa Arusha

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Januari 5, naikumbuka vizuri sana hasa ya mwaka huu 2011 unaoisha, wanamapinduzi na wapigania uhuru na haki waliuawa kwa maksudi kabisa na jeshi la polisi kupitia kwa askari polisi waliokuwa "wameamrishwa" kufyatua risasi za moto mbele ya umati ule wa viongozi na wafuasi wa CHADEMA, Lakini wengine ni wale kutoka chama cha mapinduzi(CCM) wenye mtazamo wa mapinduzi. Mimi nikiwa miongoni mwa wanamapinduzi naomba wenzangu tupange wenyewe tukumbuke Januari 5 kama sikukuu ya maadhimisho ya tukio lile la ARUSHA. Hizi ni harakati za ukombozi wa UMAJUMUI WA KIAFRIKA(pan africanism) awamu ya pili. Lakini sasa kutoka kwa wakoloni weusi. Wanamapinduzi wote(kama waliotutangulia) tumezoea kuteswa, kudharauliwa, kutukanwa, kuitwa majina ya ajabu kama; wapuuzi, wenye wivu, wajinga, wanafiki, wapika majungu, wafitini kn. Lakini hatutokata tamaa, TUNASONGA MBELE! Hadi pale tutakapoona mapinduzi ya kweli. Nipo tayari kusahihishwa. Nawasilisha!!!!
 
Naam! Ni kweli upo sahihi mkubwa wangu! Ila nina cha kufikiri halafu ntarudi kwn chanzo hii ni very important!
 
Back
Top Bottom