'Janja' yamuokoa JK Karatu • Watu wasombwa majimbo mbalimbali kumnusuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Janja' yamuokoa JK Karatu • Watu wasombwa majimbo mbalimbali kumnusuru

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by sijui nini, Oct 25, 2010.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, jana alilazimika kukusanya watu kwa mabasi kutoka Arusha mjini kwenda wilayani Karatu kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wake wa kampeni.
  Habari za kuaminika kutoka Karatu zinasema hali hiyo inatokana na Karatu kuwa ngome ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
  Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15, anaonekana kuliteka jimbo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo amekuwa akizianzisha.
  “Huwezi kuamini, jana hapa Karatu yaliingia mabasi matano kutoka Arusha yakishusha wafuasi wa CCM kwa ajili ya kuja kujaza watu wa kumsikiliza Kikwete, unajua hapa ni ngome ya CHADEMA ndugu yangu… sasa inawezekana walihofu kukosa watu,” kilisema chanzo chetu cha habari.
  Aidha, chanzo hicho kimesema uongozi wa CCM Mkoa wa Arusha, uliagiza kila mgombea ubunge katika majimbo yote ya mkoa huo kuhakikisha anasafirisha watu kama alivyoagizwa ili waweze kuhudhuria mkutano huo.
  “Huwezi kuamini mpaka jana nyumba za kulala wageni zilikuwa zimefurika ndugu yangu, utadhani kuna ugeni wa kitaifa… hawa jamaa hapa hawakubaliki kabisa,” kilisema chanzo chetu.
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amekuwa kiongozi kwa kwanza mstaafu kujitokeza hadharani kumnadi Kikwete mbele ya wananchi, tangu kampeni hizo zilipozinduliwa Agosti 21, mwaka huu.
  Sumaye aliwataka wananchi wa Karatu kumchagua tena Kikwete ili aweze kutekeleza ahadi ambazo amezitoa kwa ajili ya faida ya taifa.
  “Mko tayari kumchagua Kikwete Oktoba 31, mwaka huu? Mchagueni ili atimize ahadi alizotoa kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu,” alisema Sumaye kabla hajapanda jukwaani kumuombea kura Kikwete.


  Source: Tanzania Diama


  My Take: huyu jamaa bado hajaacha tu hii tabia!???
   
 2. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kuna vitu viwili naviona hapa .1. mpango huu unafanywa na ccm ili kuidanganya dunia kwamba JK anapendwa ili watimize azma yao ya kuiba kura ama kupora uchaguzi kwa nguvu kwa kutangaza JK ameshinda hata kama ameshindwa. 2.kama sio hapo juu basi ccm wamemchoka JK na wanamuadaa kwamba bado anapendwa wakati si kweli. jambo ambalo siliamini sana.nasaha watz tukapige kura na kumchagua mkombozi dr. slaa na kisha tulinde kura zetu na Mungu atamdhoofisha kiravu na makame wa NEC na njama zao za kutaka kupora
  http://jamiiforums.com/m
   
Loading...