Janja ya Pinda: Achagua kumsulubu DED wa Ukerewe badala ya DC, ambayhe ni kada wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Janja ya Pinda: Achagua kumsulubu DED wa Ukerewe badala ya DC, ambayhe ni kada wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 13, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Taarifa ya habari ITV ya saa mbili usiku huu imeonyesha jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyomsulubu hadharani Mkurugenzi wa Wilaya ya Ukerewe, kwa kutosimamia vizuri mipango ya maendeleo na hivyo wilaya kurudi nyuma katika umasikini ikilinganishwa na wastani ya nchi nzima. Suluba hiyo ilifanyika katika mkutano wa hadhara mjini Nansio.

  Swali langu ni: Kwa nini Pinda hakumsulubu DC, kwani yeye (DC) ndiye msimamizi wa sera za chama tawala katika wilaya -- kutokana na kauli yake mwenyewe Bungeni katika kikao kilichopita Dodoma.

  Kwa mtazamo wangu Pinda amefanya makusudi tu ili isionekane CCM ndiyo ya kulaumiwa katika ukosefu wa maendeleo huko Ukerewe. Kimakusudi kaamua kumbebesha lawama huyo DED kwa lengo la kutuaminisha kuwa hawa ma-DED ni watumishi wa umma (civil servants) na hivyo wanatakiwa wasiwe na vyama, na siyo makada wa CCM, kitu ambacho siyo kweli sidhani iwapo kuna ma-DED ambao ni CDM kwa mfano.


  Mheshimiwa Pinda, tumeamua janja yako. Mbebeshe lawama huyu kada wenu DC hapo wilayani kwa uzorotaji wa maendeleo.
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwani wewe hujui kuwa akimgusa DC atakuwa amemchokonoa mkuu wake? Hapo si ukada tu, kama hujui sifa za kuwa DC jaribu kufatilia vizuri sasa.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani sasa hiyo ndiyo ni sera ya serikali, kuwasulubu ma-DED badala ya ma-DC. Mtakumbuka huko nyuma JK alikuwa akiwasulubu ma-DC anapotembelea wilaya.

  Sera sasa ni kwamba ubovu wote si wa makada wa CCM, ni watendaji wa serikali.

  Naona serikali inahangaika sana kujikosha kwa madudu yake. Tutaona mengi.
   
 4. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,627
  Likes Received: 2,046
  Trophy Points: 280
  Kwa siasa za Tanzania wenye nafasi za kisiasa huwa hawakosei na wakikosea huwa wanaundiwa tume alafu majibu hayatolewi lakini kwa watendaji wanapingwa chini tu
   
 5. M

  Magesi JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  C.c.m inakufa vibaya
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Damned if you do, damned if you don't.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  DED alikuwa na wakati mgumu sana
   
 8. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yeye kama ni mtendaji mzuri mbona nusra apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye?
   
 9. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pinda kwa Ma-DC ni kenge blue tu, hana uwezo wa kudeal nao coz ni presidential appointees like himself, so ili kujikosha kaenda kuonyesha makucha yake kwa mjusi kafiri DED
   
 10. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  kaangalie shule za msingi huko Igunga kwanza ndipo utachoka na DED wa huko! Ukifuatilia sana utendaji wa ded nchi nzima , basi utafukuza wote. Mkaguzi mkuu aliisha kupatia orodha ya wizi katika halmashauri za wilaya, sasa wewe baada ya kufanya mshike mshike kuwakama ma DC na DED waliohusika na wizi huo una msingle out mmoja na kumpatia karipio. Keep In Mind, Pinda, the meek will inherit the world!
   
Loading...