Tonge
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 695
- 12
Duuuuuuuuuh kweli dunia tambara bovu, Kwa maoni yangu Sitta si mtu wa kunyimwa uspika katika bunge hili ila kwa kitendo cha Chenge kuandaa press conference ya kumponda sitta tena kwa taarifa iliyoandikwa kwa mkono ni dhahiri kulikuwa kuna kundi lilijipanga ili kuonyesha kuwa Chenge na Sitta wanaugomvi au kumchafua Sitta ili kamati kuu ya CCM iwateme wote na nafasi yake ichukuliwe na Ana Makinda maana hawa Ana Abdallah na Kate Kamba ni wasindikizaji tu.
Mafisadi kwao huu ni USHINDI wa kishindo na sasa wanakunywa mvinjo, Nimekuwa nikifuatilia mara kibao bunge lililopita na mara nyingi Makinda anapokuwa spika huwa haruhusu mijadala au hoja toka kwa wabunge pinzani (Marehemu Wagwe na Makinda, Zitto na Mkinda) nahisi kama ndie yeye ambaye angekuwa spika kipindi hicho basi hoja kama za RICHMOND, MEREMETA NA RADA tusingezijua kwani angezikatalia kujadiliwa au kupelekwa bungeni, CCM kweli ni CHAMA CHA MAFISADI na hawana uchungu na nchi hii bali ni kuchukua chao mapaemaaaaaaaaaa.Mh mzee wa VIJISENTI tambua kuwa watanzania wa leo sio waleeeeeee wa zama za Julius, tunaelewa na tuna upeo wa kutambua janja zenu nyie mafisadi.
Mh Sitta aluta continua "mapambano yanaendelea" na kwa kuwa sasa wewe sio spika huu ndio wakati wako wa kupenyeza hoja bungeni na kuzichangia hasa zile zinazo husu ufisadi nchini kwani tuna imani unajua mengi na una siri kubwa za kina Lowasa, Rostam na Chenge(mafisadi).
Mh Chenge hivi huoni hata aibu, umempa Hosea vijisenti na kakutetea kwamba wewe ni mtu safi kwenye skendo ya RADA, umeona sasa Uingereza wamemuumbua? Chenge hizi kweli wewe ni mtanzania? maana inaonyesha kuwa huna uchungu na nchi hii na wananchi wake,tumekuchoka CHENGE.