Janja ya CCM kutaka kutuchagulia viongozi wanaowataka imegundulika mapema sana!


M

Mwaisumbe

Member
Joined
Sep 13, 2011
Messages
9
Likes
1
Points
0
M

Mwaisumbe

Member
Joined Sep 13, 2011
9 1 0
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. W. Slaa, ndio viongozi makini na wenye busara ambao wakati huu wanahitajika sana kuliko wakati mwingine wowote. Chadema kwa kupitia wanachama wake inatambua kazi zao na uadirifu wao kwa Chama.

Wanachama. wapenzi na wadau, hawahitaji kuambiwa na mtu mwingine yeyote kwani sisi ndio tunaojua ukweli na hakika ya matendo yao kwa Chadema.

Ngwe iliobaki ni ngumu kuliko miongo miwili iliopita, kumbuka kuwa kunapo karibia kuchwa ndio giza tololo lina tanda tunahitaji viongozi majasiri, wenye nia ya dhati na thabiti, ambao wapo tayari kwa mapapambano ya kutetea haki na kuleta mabadiriko kwa wanyonge, tunahitaji kiongozi asiye msaliti hata kwa sekunde moja, tunayo imani kubwa kwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu katika kuongoza jahazi hili.

Usawa, Uwazi, Ukweli, Upendo na Mshikamano ndio nguzo kuu iliyo shika msingi na paa la Chadema na kufanya chama kutoyumba siku zote. Chadema ni Chama cha mfano wa kuigwa, na ndio kimbilio la wanyonge na wapenda haki katika nchi hii.

Kuindoa CCM hakuhitaji vyeti vya darasani au itifaki, dhana hii inathibitishwa na vyama vilivyo tangulia kuwa maarufu. Mapambano ya bila kuchoka, uzarendo, na nia ya dhati katika kupigania haki,ndio jibu pekee la kuiondoa ccm katika sanduku la kura.

Shetani hasifiwi, wala shetani hatukanwi kwani ubaya ndio sifa yake, wana Chadema tunajua na kutambua fika lipi jema na lipi baya. Kamanda Mkuu Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Slaa, songa mbele kumbukeni mti wenye matunda!!!! Na sisi tunalitambua hilo tupo nyuma yenu na kundi linazidi kuongezeka,
Chadema ni kama treni ya ajabu watu wanapanda na hawataki kushuka kwenye vituo maana kila mtu alipanda mwenyewe na kwa hiari yake.
People's
 

Forum statistics

Threads 1,237,476
Members 475,533
Posts 29,289,871