Janja ya CCM aliyoirithi kwa mkoloni ya "divide and rule" sasa ukingoni.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Janja ya CCM aliyoirithi kwa mkoloni ya "divide and rule" sasa ukingoni..........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Oct 17, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Kwa miaka takribani 50, CCM/TANU/ASP imekuwa mwanafunzi mzuri wa ukoloni wa mwingereza wa kugawa raia ili kuwatawala. Mkoloni alitugawa kwenye makundi ya udini na ukabila kwa kutumia peremende na dola katika kututhibiti na CCM sasa imekuwa gwiji kwenye hiyo taaluma ya kidhalimU. Hii amani CCM inayoiongelea ni ya kwenye majukwaa tu ya siasa lakini haitoki moyoni na wala haiko kwenye vitendo vyake.

  Sasa hivi CCM imetugawa kwenye makundi ya udini, kimapato na kikabila ili kuendeleza ubabe wake wa kututawala.

  Lakini historia yatufunza ya kuwa penye dhuluma mkombozi Mwenyezi Mungu atatutafutia na kwetu Dr. Slaa ndilo chaguo la Mwenyezi Mungu mwenye rehema kebekebe...........

  CHAGUA DR. SLAA............CHAGUA CHADEMA ILI KAZI YA UJENZI WA TAIFA IANZE
   
Loading...