Jangwani: Kutoka kuwa Uwanja wa Simba SC hadi kuwa Soko Kuu la Machinga ni ubunifu mzuri

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,833
141,751
Naupongeza sana uamuzi wa Rais Samia kujenga soko la kisasa la Wamachinga pale jangwani.

Awali Jangwani palikuwa na viwanja vya kufanyia mazoezi timu za Simba SC aka Makolo, Pan Africans, Red Star na Cosmo na pale juu ndio wapo Yanga yaani Utopolo hadi leo.

Baadae jangwani ikawa stendi ya malori kabla ya ujenzi wa ofisi za Mwendokasi.

Naamini Soko kuu la Wamachinga litafanya Jangwani ipendeze na cha msingi ni kutilia maanani mabadiliko ya tabia nchi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
 
Dah wewe...ripoti centro.....nimecheka sana. Inashangaza mwendo kasi wenyewe hata manyunyu tu yakianza wanahamisha mabasi yote. mfanyabiashara gani atakubali kwenda pale.
 
Dah wewe...ripoti centro.....nimecheka sana. Inashangaza mwendo kasi wenyewe hata manyunyu tu yakianza wanahamisha mabasi yote. mfanyabiashara gani atakubali kwenda pale.
Yale maji yatarudishwa kwenye mkondo wake wa asili!
 
Sio kaz rahs kama unavyofikria , Kwa nchi yetu hii ya upigaji , inahtaji massive effort na strong engineer kurun hyo project kitu ambacho kibongo bongo haipo , labda mjeruman arudi kutawala
Subiri ujionee.

Mbona zamani maji yalikuwa hayajai!
 
Mto Msimbazi wasipoujenga kwa kuuchimba na kuweka kingo ngumu za cement kwa ajili ya kuruhusu maji kupita haraka na kwenda baharini, nasema hivi, Machinga watakuwa dimbwini.

Mto Msimbazi kipindi cha mvua za masika maji yatajaa maduka ya machinga, ni kuwa makini sana. Kama litajengwa ghorofa, wahakikishe mto unajengwa kwanza wakati soko likifuata.
 
Atakayeapitisha hilo akapimwe mkojo,vyura utopolo wenyewe wamekimbilia kigamboni,udart wamekula hasara mabasi yao,
 
wangewaachia simba uwanja wao ili siku mwamedi aka papa musofe, siku akienda kuangalia mazoezi asombwe na maji akatupwe bahari ya Hindi.
 
Yale maji yatarudishwa kwenye mkondo wake wa asili!
Siyo rahisi mkuu.
Pale si mkondo, ni bonde la bahari, ni kama ghuba kavu yenye maji kwa chini. Na hakuna juhudi za maana za kurekebisha. Miaka ya mwanzoni mwa 1990 magomeni - Fire ilikuwa imenyooka kabisa kwa sababu lilikuwa tuta. Viwanja vya jangwani vilikuwa vinaonekana viko chini sababu barabara ilikuwa juu-tuta kubwa lilijengwa na kajima (na alikuwa na ofisi pale). Nna madaraja yale ya jangwani chini kulikuwa vibanda vya vibaka walikuwa wanaishi.

Leo hii tuta halionekani, barabara imebonyea mpaka chini. Lile tuta halionekani tena. Limekwenda wapi?
 
Mto Msimbazi wasipoujenga kwa kuuchimba na kuweka kingo ngumu za cement kwa ajili ya kuruhusu maji kupita haraka na kwenda baharini, nasema hivi, Machinga watakuwa dimbwini.

Mto Msimbazi kipindi cha mvua za masika maji yatajaa maduka ya machinga, ni kuwa makini sana. Kama litajengwa ghorofa, wahakikishe mto unajengwa kwanza wakati soko likifuata.
Dawa ni kuuinua usawa wa ardhi ya fire hata ukichimba bado flow ya maji ni kubwa
 
Back
Top Bottom