Janga: MV Tanzania

whizkid

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
357
240
Mliofunga poleni na swaum. Wenye misiba poleni kwa kufiwa. Samahani kama nitawaudhi kutumia neno "Meli".

Tujadili mikakati ya kututoa hapa tulipo. Cheki tunavyobanana ndani ya hii meli. Ni siasa pekee zimetufikisha hapa tulipo? Tulifumbwa macho, tukazibwa midomo na kukatwa mikono? Hapana. Siongelei meli halisi. Hii ni meli tofauti. Hebu fikiria:

Mimi na wewe bado tunao wajibu wa kudai hata kupiginaia haki zetu tunazodhulumiwa. Tumepayuka sana humu JF na penginepo lakini bado hatupati majibu ya maswali mengi tu ya msingi. Marking scheme haijulikani, kila mtu anadhani yupo sahihi zaidi ya mwingine. Meli inaenda tu.

Kama tutakubali kuendelea kukaa ndani ya mgahawa mdogo ndani ya meli inayonuka damu na kunyweshwa pombe ya matapishi ya sera na kauli zisizofaa, kunong'ona chini ya carpet na kusubiri miujiza, kuwabeza wadai haki kama madaktari wanaogoma kisa maslahi na huduma duni, kuridhika na hali ilivyo, kupoteza muda kujadili watu badala ya hoja, kusifia ujinga na kutetea wapinga haki, basi kamwe tutaendelea kuwa wasafiri ombaomba wapiga kelele tunaodhulimiwa haki zetu na wajanja wachache ndani ya meli. Ujanja wao au uzembe wetu ndio umezidi? Sina hakika.

Wewe na mimi ndio tunaoweza kuikomboa meli hii? Rais wa JMT (captain) na serikali yake (wasaidizi) wamejaribu mpaka sasa japo wengi tunaona wameshindwa. Tuna kila sababu ya kuwanyooshea vidole hata kuwazomea japo haisaidii maana hawana aibu. Wao wanaweza wakawa wamefaulu sana kwa malengo yao kuwa tofauti na ya abiria. Ahadi zao kwetu si muhimu kama ahadi za maswahiba wao. Matumbo yao ni muhimu kuliko ya mama wajawazito wanaotaabika kujifungua kwa tabu. Inaumiza sana kichwa. Tuvumilie?

Wananchi ndio tumewapa ajira? Mbona hawatutumikii sisi? Tulikubali washike uskani wa meli chakavu MV Tanzania? Kura tulipiga wenyewe. Zilipopungua waliiba mpaka zikatosha. Tukawaacha. Meli ndio hii wamehangaika nayo kibishi na sasa inaelekea usawa wa miamba baada ya kupigwa na dhoruba safari nzima. Tujiulize maswali machache:

1. Turuke tuogelee kabla haijagonga mwamba?

2. Tumtoe captain ashike uskani mwingine tunayedhani anao uwezo kama yupo?

3. Tuendelee kuwa na imani labda captain wetu atafanya miujiza?

4. Liwalo na liwe?

ANGALIZO: Meli ikizama kufa au kupona hakutegemei chama, dini, kabila, ukoo, kipato, marafiki au maadui.
 
Ujumbe umefika ila sasa umetufikia watu wachache sana ktk Tz, kwani humu jf tu wastani wa watz elfu 84 na point kadhaa ni asilimia zero point kadhaa na siyo wote tutakaousoma ujumbe huu iliyopo sasa ni sisi wachache tuliobahatika kuusoma ujumbe huu tuwajulishe na wenzetu hata kwa kila mmoja kuwalisha waTz walao 10 nao hao 10 kufanya hivyo na mwisho wake wote utatufikia na kujiandaa kufanya uamuzi thabiti na wenye manufaa hapo 2015
 
Message Delivered!
Japokuwa ujumbe umekuwa mrefu 'Nina wasiwasi' na wenzetu kama wanaweza kuusoma wote (Japokuwa unavutia).
Mengi nayatamani kata hilo la kumtosa Nahodha kabla 'Meli' haijagonga mwamba. Ila na 'Tukome' 2015 kumchagua Nahodha asiye na Misuli ya Ubongo.
 
.......tafakari.....chukua hatua!.....
Mliofunga poleni na swaum. Wenye misiba poleni kwa kufiwa. Samahani kama nitawaudhi kutumia neno "Meli".

Tujadili mikakati ya kututoa hapa tulipo. Cheki tunavyobanana ndani ya hii meli. Ni siasa pekee zimetufikisha hapa tulipo? Tulifumbwa macho, tukazibwa midomo na kukatwa mikono? Hapana. Siongelei meli halisi. Hii ni meli tofauti. Hebu fikiria:

Mimi na wewe bado tunao wajibu wa kudai hata kupiginaia haki zetu tunazodhulumiwa. Tumepayuka sana humu JF na penginepo lakini bado hatupati majibu ya maswali mengi tu ya msingi. Marking scheme haijulikani, kila mtu anadhani yupo sahihi zaidi ya mwingine. Meli inaenda tu.

Kama tutakubali kuendelea kukaa ndani ya mgahawa mdogo ndani ya meli inayonuka damu na kunyweshwa pombe ya matapishi ya sera na kauli zisizofaa, kunong'ona chini ya carpet na kusubiri miujiza, kuwabeza wadai haki kama madaktari wanaogoma kisa maslahi na huduma duni, kuridhika na hali ilivyo, kupoteza muda kujadili watu badala ya hoja, kusifia ujinga na kutetea wapinga haki, basi kamwe tutaendelea kuwa wasafiri ombaomba wapiga kelele tunaodhulimiwa haki zetu na wajanja wachache ndani ya meli. Ujanja wao au uzembe wetu ndio umezidi? Sina hakika.

Wewe na mimi ndio tunaoweza kuikomboa meli hii? Rais wa JMT (captain) na serikali yake (wasaidizi) wamejaribu mpaka sasa japo wengi tunaona wameshindwa. Tuna kila sababu ya kuwanyooshea vidole hata kuwazomea japo haisaidii maana hawana aibu. Wao wanaweza wakawa wamefaulu sana kwa malengo yao kuwa tofauti na ya abiria. Ahadi zao kwetu si muhimu kama ahadi za maswahiba wao. Matumbo yao ni muhimu kuliko ya mama wajawazito wanaotaabika kujifungua kwa tabu. Inaumiza sana kichwa. Tuvumilie?

Wananchi ndio tumewapa ajira? Mbona hawatutumikii sisi? Tulikubali washike uskani wa meli chakavu MV Tanzania? Kura tulipiga wenyewe. Zilipopungua waliiba mpaka zikatosha. Tukawaacha. Meli ndio hii wamehangaika nayo kibishi na sasa inaelekea usawa wa miamba baada ya kupigwa na dhoruba safari nzima. Tujiulize maswali machache:

1. Turuke tuogelee kabla haijagonga mwamba?

2. Tumtoe captain ashike uskani mwingine tunayedhani anao uwezo kama yupo?

3. Tuendelee kuwa na imani labda captain wetu atafanya miujiza?

4. Liwalo na liwe?

ANGALIZO: Meli ikizama kufa au kupona hakutegemei chama, dini, kabila, ukoo, kipato, marafiki au maadui.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom