Janga linaloikumba nchi yetu linaanzia katika kutokuwa makini katika kupanga vipaumbe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Janga linaloikumba nchi yetu linaanzia katika kutokuwa makini katika kupanga vipaumbe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Feb 9, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa baadhi yetu,bunge hili la sasa halitupi matumaini yeyote. Hii inatokana na ukweli kwamba tangu kuchaguliwa kwake limeonyesha udhahifu mkubwa katika kuweka vipau mbele vyake. Tuanzie na hili la semina elekezi; kwa mujibu ya katiba yetu, bunge pamoja na mambo mengine, limepewa jukumu la kusimamia serikali, kama hivyo ndivyo, inawezekanaje kiongozi wa serikali hiyo inayopashwa kusimamiwa na bunge akaandaa semina ya kuelekeza bunge namna ya kutekeleza majukumu yake, na yeye ndiye akawa mwenyekiti wa semina hiyo, kama ilivyofanyika hivi majuzi! Mbali na hayo, jana nzima bunge lilipoteza muda wote, kujadili hoja inayolenga kupunguza nguvu za chadema katika kudhibiti ubadhirifu serikalini. Na kama hiyo haitoshi, hivi sasa bunge hilo limepanga kujadili hatuba ya rais, aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa bunge, kwa siku tano.Kwa kuzingatia ukweli kwamba, kwa kila siku ya Mungu bunge linapokuwa limekaa, linatumia zaidi ya Tshs.100 milioni, kwa hizo siku tano bunge litateketeza zaidi ya Tshs 500 milioni kwa kupongezana tu, wakati nchi hii inakabiliwa na matatizo chungu nzima.
   
Loading...