Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limetoa wito wa kuchangisha kiasi cha dola milioni 130 za kimarekani ili kuwasaidia watu wanaokumbwa na njaa nchini Zimbabwe kwenye kipindi hiki maalumu cha mlipuko wa virusi vya Corona.
Shirika hilo limesema Zimbabwe imekumbwa na msukosuko wa ukosefu wa chakula kutokana na hali mbaya ya hali ya hewa na kupungua kwa ukuaji wa uchumi, WFP inahitaji dola milioni 130 za kimarekani kuendeleza operesheni ya dharura hadi mwezi Agosti, ili kuwaokoa mamilioni ya watu wa nchi hiyo watakaokumbwa na baa la njaa.
WFP imeongeza kuwa kutokana na ukosefu wa fedha, tangu mwezi Januari mwaka huu shirika hilo limeshindwa kuwasaidia watu milioni 4.1 nchini humo kila mwezi kama lilivyopangwa, na idadi hiyo ilikuwa milioni 3.7 mwezi uliopita.
Kwa sasa idadi ya watu wanaokumbwa na ukosefu wa chakula nchini Zimbabwe imefikia milioni 7.7, idadi ambayo imezidi nusu ya watu wote wa nchi hiyo.