Janga la mauaji ya Albino ni laana kwa Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Janga la mauaji ya Albino ni laana kwa Tanzania.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Dec 14, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tanzania imeshawahi kukumbwa na inakumbwa na matatizo mengi, ufisadi,ujambazi,rushwa,njaa,ajali za barabarani nk.nk.,lakini hili janga la Albino ni la aibu,la kutisha halafu ni la kushangaza sana.Tanzania tangu ipate uhuru haijawahi kukumbwa na tatizo la namna hii. Nimejaribu kutafakari sababu zinazotolewa na wadau mbalimbali kuhusiana na tatizo hili lakini naona zote haziingii akilini mwangu,wala sio sahihi ni za bora liende.Tatizo ni kwamba watu wengi wanashindwa kutofautisha kati ya "causes and effects."Kwa mfano wanasema mauaji ya albino yanaletwa na umaskini,ushirikina au tamaa nk.nk..Sawa, sasa umaskini,ushirikina au tamaa vinaletwa na nini?Ni mlolongo mrefu wa mambo ambao nisingependa kuuzungumzia,lakini hizo ni "effects",sasa visababishi ni nini vya 'effects" hizo?Watu wengi wanakwepa au wanakataa sababu za kiroho,lakini hata wakikataa au kukwepa haibadilishi ukweli kwamba mambo mengi sababu zake ni za kiroho,ingawa mambo yenyewe yanaonekana kimwili.Naomba twende pamoja,Biblia itatupa majibu.Katika kitabu cha Warumi,Sura ya kwanza,msitari wa 18-32,tunasoma maneno haya,"18KWA MAANA GHADHABU YA MUNGU IMEDHIHIRISHWA KUTOKA MBINGUNI JUU YA UASI WOTE NA UOVU WA WANADAMU WAIPINGAO KWELI KWA UOVU.19Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao,kwa maana Mungu aliwadhihirishia.20Kwa sababu mambo yake yasiyo onekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana,na kufahamika kwa kazi zake;yaani uweza wake wa milele na uungu wake;hata wasiwe na udhuru.21Kwa sababu walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao,na na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.22Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;23wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu,na ya ndege na ya wanyama,na ya vitambaavyo.
  24Kwa ajili ya hayo MUNGU ALIWAACHA KATIKA TAMAA ZAO ZA MIOYO YAO,WAUFUATE UCHAFU,HATA WAKAVUNJIANA HESHIMA MIILI YAO.26Kwa maana walibadili kweli ya Mungu kuwa uongo,WAKAKISUJUDIA KIUMBE NA KUKIABUDU BADALA YA MUUMBA anayesujudiwa milele.Amina.Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu,hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiso ya asili;27Wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke,ya asili wakawakiana tamaa,wanaume wakiyatenda yasiyopasa,wakapata nafsini mwao yaliyo haki yao.28Na kama waliyvokataa kuwa na Mungu Mungu katika fahamu zao,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa,wafanye yasiyowapasa;29WAMEJAWA NA UDHALIMU WA KILA NAMNA UOVU NA TAMAA NA UBAYA;WAMEJAWA NA HUSUDA;WATU WA NIA MBAYA,WENYE KUSENGENYA,30WENYE KUSINGIZIA,WENYEKUMCHUKIA MUNGU,WENYE JEURI,WENYE KUTABAKARI NK.NK.32Ambao wakijua sana hukumu ya haki y Mungu,ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti,wanatenda hayo ,wala si hayo tu ,bali wanakubaliana nao wayatendayo.

  Sasa maneno hayo hapo juu yana maana gani?
  1.Mauaji ya Albino ni ghadhabu ya Mungu juu ya Tanzania kwasababu tumekataa kumtii Mungu.Mungu anasema hakuna Mtanzania anayeweza kusema hamjui Mungu,Kwa kuwa yeye mwenyewe amejidhihirisha ndani ya kila mmoja wetu kupitia kwenye umbaji wake.

  2.Kwakuwa tumemkataa Mungu,yeye ametuacha.Kwa maana nyingine yanayotokea Tanzania,pamoja na mauaji ya Albino ni matokeo ya kuachwa na Mungu.Watu sasa wamegeuikia ibada za mashetani.Kumbuka kwamba Freemasonry ni "cult" inayokuwa kwa haraka sana Tanzania,hizi ni dalili za wazi za kuachwa na Mungu.Watu sasa wanamwabudu shetani kiumbe ambacho Mungu alikiumba, badala ya kumwabudu Mungu mwenyewe.Mistari hii inataja uovu mwingi ambao unaendana na kuachwa na Mungu.Lakini nataka u-note wanaume kwa wanawake kugeukiana wenyewe kwa wenyenye kimapenzi.Hii ni dalili pia za Taifa kuachwa na Mungu.

  3.Mwisho ni kwamba, kama Watanzania hawatageuka na kuuacha uovu wao,Taifa hili litaangamia kabisa.

  MPUMBAVU AMESEMA MOYONI MWAKE KWAMBA HAKUNA MUNGU
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Mimi naamini sio laana ni uelewa duni tu wa baadhi ya watu wanaoamini kuwa viungo vya Albino vina bahati ya pekee katika kupata pesa za haraka haraka!
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  First lady naomba usome thread yangu vizuri.Hiyo imani yako inatokana na nini,au base yake ni nini?Kwakuwa imani haitoki hewani tu.
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Imani yangu base yake ni kwa MUNGU!mimi sikubaliani eti hii ni laana jamani!yaani kweli laana isababishe mauji ya ma Albino wasio na hatia!
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ndugu tuko pamoja, hii ni laana kwa nchi na wakujilaumu ni sisi wenyewe! Inanikumbusha kisa cha Habili na Kaini kwenye Biblia. Baada ya Kaini kumuua nduguye Mungu alizungumza maneno magumu sana: "kwa kuwa ardhi imefunua kinywa chake kupokea damu isiyo na hatia; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako".

  Kumwaga damu isiyo na hatia ni laana na ni laana juu ya nchi. Sijaridhishwa na juhudi za Serikali kudhibiti mauaji ya Albino na ukweli ni kuwa serikali haiwezi kushindwa kuwatambua Wachawi walionyma ya mauaji haya, mbona Vicky Ntetema wa BBC ambaye ni layman tu aliweza? Kwa nini serikali pamoja na vyombo vyake vya ulinzi na usalama ishindwe? Sipati picha!
   
Loading...