MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.
Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.
Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.
Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.
Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”
Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.
Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.
Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.
Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.
Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.
Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini
Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.
Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.
Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu ya Rais Kenyatta inashangaza kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi katika nchi zetu wanakusanyika zaidi mchana kuliko usiku!
Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.
Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.
Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.
Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!