Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,041
2,000
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.

Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.

Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.

Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”

Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.

Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.

Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.

Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.

Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.

Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini

Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.

Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.

Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu ya Rais Kenyatta inashangaza kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi katika nchi zetu wanakusanyika zaidi mchana kuliko usiku!

Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.

Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.

Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!
 

troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
13,980
2,000
Ila huyu mzee namsifu hapa tu. Kwa kweli kwa huku Africa swala la watu kubaki nyumbani ni haliwezekani. Tusidanganyane.

Huko Kenya kama hivo hali tete imebidi wabadili msimamo. Uganda hali ngumu mpaka wanachapana bakora.

Hivi mimi uniambie nikae nyumbani na hela ya kula sina? Serious?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
MsemajiUkweli ,

..Tz haina CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi, na kuwatibu, wagonjwa wa Corona ikiwa ugonjwa huo utaingia hapa nchini.

..Kutegemea msaada wa serikali hii ni UENDAWAZIMU. Hivyo basi ni bora kumuomba MUNGU atuepushe kwasababu hatuna serikali ya kuitegemea.

..Uamuzi wa Raisi ulikuwa very simple. He does not have the options ambazo mataifa mengine yanayo. Uamuzi hapa ni KUSUBIRI tuone nini kitatokea. Kwa wale wenye imani wanatakiwa KUSALI.

..Hatuna vifaa, hatuna wataalamu, hatuna fedha. Lakini tunaweza KUSALI.
 

hoffman

Senior Member
Jul 21, 2011
178
250
Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JPM) yupo sawa. Raia hatuna hata fridge na wenye nazo bado umeme unaweza kuwa tatizo kwa upande wa kuhifadhi chakula cha muda mrefu. Nampongeza sana kwa kuliona hilo.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,676
2,000
Magu hakulaumiwa kwa hayo uliyosema bali kalaumiwa kwa mambo kama pale aliposema hawezi kuzuia watalii kuingia nchini! Uzuri ni kwamba, hao watalii wenyewe wana akili na wanafahamu risk iliyopo kwa wao kuendelea kusafiri, na kwahiyo wameamua kujizuia wenyewe huko huko kwao!

Na kwavile ndege nyingi zimesimamisha international flights, hiyo ndo nafuu yenyewe kwetu vinginevyo lau kama airlines na watalii wangekuwa na akili kama za JPM, balaa ambalo lingekuwa limeshatokea tungekuwa tunatafutana hivi sasa!

Zanzibar kwa mfano, wanapokea watalii wengi sana kutoka Italy! Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo Watalii wa Italy wangeendelea kuingia?!

Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo wananchi kwenye mataifa yaliyoathirika wangeendelea kumiminika kwa sababu tu Mpiga Ramli mmoja anaamini coronavirus haifui dafu mbele ya ibada?!

Lingine alilolaumiwa JPM ni kauli yake ya majuzi kwamba eti watu waendelee tu kumiminika kwenye nyumba za ibada na kwamba eti COVID-19 haiwezi kuishinda Damu ya Yesu!!

Ni mtu wa ajabu tu ndie anaweza kutetea ujinga kama huu kwa sababu hakuna janga hata moja lililowahi kuzimwa kwa watu kujazana makanisani na misikitini!

And FYI, zipo nchi nyingi tu ambazo zilidhani zingeendelea kuwa salama! Spain kwa mfano, daktari mmoja alifikia hadi kusema ni ngumu sana kwa Spain kupata maambukizo mengi kwa sababu tu walidhani kuto-share mpaka na Italy ingeweza kuwa salama kwao!

Leo hii, it's a matter of time kabla Spain hawajaifunika Italy!!

Hata Trump nae mwanzoni wala hakudhani ingekuwa serious issue kwa US! Leo hii US imeyapiku mataifa yote kwa idaidi ya maambukizi!!

So, endeleeni tu kutetea ujinga kwa sababu ndicho mlichoapa kukifanya!!
 

bizplan

JF-Expert Member
Jun 28, 2013
458
500
MsemajiUkweli,
Huu ndio ukweli halisi kwa mazingira yetu. Labda niongezee tu,

Hizo nchi za Rwanda na Uganda wana hatari ya kumaliza watu wao kuliko Tanzania na Burundi.

1. Mtu mwenye njaa inafikia hatua yupo tayari kwa lolote. Pata picha upo ndani watoto wanakulilia njaa njaa njaa, ukitoka unaweza kufa, ukibaki ndani unakufa kwa hakika so mtu anaona bora atoke ajaribu bahati yake.

2. Wote wanaofanya lock down hakika wanajisumbua. China ilijaribu Wuhan, yes kumekuwa na mafakinio lakini bado maambukizi mapya yamekuwepo na yanaendelea kuongezeka. Sasa hili likija kwetu ni ngumu kuliko maelezo.

3. Si kweli kuwa lockdown wataifanya siku zote, ipo siko wataachia. Watakapoachia wale ambao wana virusi ila hawana dalili wanaweza kusambaza tena kwa wengine.

Solution ipatikane kinga/chanjo na dawa ila hizi nyingine ni kujilisha upepo tu.

Na serikali itakayoingia mkenge kufata hizi policy za wazungu, itakuwa impoteza kila kitu for sure.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,676
2,000
Ila huyu mzee namsifu hapa tu. Kwa kweli kwa huku Africa swala la watu kubaki nyumbani ni haliwezekani. Tusidanganyane.

Huko Kenya kama hivo hali tete imebidi wabadili msimamo.
Uganda hali ngumu mpaka wanachapana bakora.
Hivi mimi uniambie nikae nyumbani na hela ya kula sina? Serious??
Acha kupotosha watu wewe!

Hakuna aliyewahi kumlaumu Jiwe eti kwa sababu ya kuacha watu waendelee kufanya kazi bali watu walimlaumu kwa mambo kama alivyokuwa anaongea kwa mbwembwe kwamba hawezi kuzuia watalii kuingia nchini, kufuta international flights na huu ujinga wa last week kwamba eti watu waendelee tu kujazana kwenye nyumba za ibada na kwamba COVID-19 haiwezi kufua dafu mbele Damu ya Yesu!

Ni rahisi wa hovyo hovyo tu kama Magufuli ndie anaweza kuaminisha watu eti unaweza kupambana na coronavirus kwa maombi!
 

bizplan

JF-Expert Member
Jun 28, 2013
458
500
Lazima utete ujinga... utatetea hadi suala la serikali kumvua madaraka Dr. Janabi kwa sababu aliongea ukweli kuhusu COVID-19. Na kwavile Janabi ameshatiwa adabu, hakuna daktari hata mmoja atakayeweka wazi ukweli kuhusu janga!
Mkuu, revisit your details. Kwa jinsi nilivyoiona hiyo barua ni kuwa Prof anajulisha watu wa taasisi yake kuwa kuna mtu A hatakuwa ofisini hivyo mtu B atakaimu nafasi yake ktk hiyo idara kipindi huyo mhusika hayupo. Simple like that.

Unless uwe haujui mambo ya office au hujawai kukaimisha au kukaimishwa.
 

kamjabari

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
528
1,000
Upo sahihi , nilishangazwa sana na watu wanaosema serikali ifunge mipaka sisi wengime tuliona kufunga mipaka ni sawa na kujifungia ndani kwa kumkimbia adui na ndani huna kitu , ina maana adui anaweza hata akaja kugonga mlango wako na ukaogopa kufingua mda wote kitakacho tokea ......hatari, tufikiri mara nyingi zaidi na kuchuja mawazo yetu kabla ta maamuzi.

Nampongeza Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,041
2,000
JokaKuu,
Kwani baadhi ya nchi kama Uganda, Rwanda, South Africa na Kenya ambao wametoa amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao wana CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi na kuwatibu wagonjwa wote wa COVID-19?

Kwani wao hawakuwa na option kama ilivyofanya serikali ya Tanzania?

Nadhani hujajua hata msingi wa mada yangu!
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,967
2,000
Ni kwa sababu Corona aijawa tatizo Tanzania na tuombe hali iendelee kubaki ivyo.

Wanaotaka watu kubaki majumbani sio kwamba wana hela za mchezo za kugawa isipokuwa hiyo ndio njia pekee ya kupunguza kasi ya ukuaji vinginevyo ingekuwa ni balaa.

Kubakiza watu majumbani ni maamuzi ya kisayansi sio kupenda ukiacha watu waendelee na shughuli kama kawaida mtu mmoja anaweza unga chain ya watu mianne ndani ya mwezi na ukifungia watu mtu mmoja anaweza sababisha chain ya watu 30 ndani ya mwezi unaweza ona tofauti kubwa sana hapo kwenye rate ya maambukizi.

Lengo la hatua hizo ni kuweza ku manage capacity ya utoaji wa huduma za afya ambazo hata kwa kufungia watu bado resources azitoshi kuhudumia wagonjwa ndio maana unaona hotel, sports centre zinageuzwa hospitals, wastaafu wanaitwa kurudi kazini, manesi wa mwaka wa mwisho washaajiliwa bila ya ku graduate na voluntary zaidi ya laki mbili na nusu wanahitajika NHS nchi kama UK.

Ukisema uache mambo yaendelee kama ilivyo ndio kabisa ni death sentence kwa watu wengi kwa sababu watakuwa hawana hiyo capacity ya ku deal na idadi ya wagonjwa kutokana na rate ya maambukizi.

Ndio maana wengine tunaomba hili janga mungu atuepeshuie mbali kama lilivyowakumba wengine maana sijui itakuwaje.
 

bizplan

JF-Expert Member
Jun 28, 2013
458
500
MsemajiUkweli ,

..Tz haina CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi, na kuwatibu, wagonjwa wa Corona ikiwa ugonjwa huo utaingia hapa nchini.

..Kutegemea msaada wa serikali hii ni UENDAWAZIMU. Hivyo basi ni bora kumuomba MUNGU atuepushe kwasababu hatuna serikali ya kuitegemea.

..Uamuzi wa Raisi ulikuwa very simple. He does not have the options ambazo mataifa mengine yanayo. Uamuzi hapa ni KUSUBIRI tuone nini kitatokea. Kwa wale wenye imani wanatakiwa KUSALI.

..Hatuna vifaa, hatuna wataalamu, hatuna fedha. Lakini tunaweza KUSALI.
Mkuu, umeongea kwa hekima sana. Afu unaonekana ni mtu wa imani sana. Tofauti na jina unalotumia humu.....kweli dont judge the book by its cover.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,041
2,000
Ila huyu mzee namsifu hapa tu. Kwa kweli kwa huku Africa swala la watu kubaki nyumbani ni haliwezekani. Tusidanganyane.

Huko Kenya kama hivo hali tete imebidi wabadili msimamo.
Uganda hali ngumu mpaka wanachapana bakora.
Hivi mimi uniambie nikae nyumbani na hela ya kula sina? Serious??
Baada ya wiki moja wakiwa kwenye amri ya kutotoka nje hali itakuwa mbaya zaidi kwa sababu hata kile kidogo walichonunua kwa pesa kidogo walizonazo kitaisha.

Kwa nchi zetu za Afrika unaweza kutoa amri hiyo ya kukaa ndani iwe kwa siku moja au mbili lakini siyo kwa zaidi ya wiki moja!
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
Kwani baadhi ya nchi kama Uganda, Rwanda, South Africa na Kenya ambao wametoa amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao wana CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi na kuwatibu wagonjwa wote wa COVID-19?

Nadhani hujajua hata msingi wa mada yangu!
..kuwaweka watu majumbani huku huna CAPACITY ya kuwapima na " kuwachomoa" waathirika na kuwahifadhi haisaidii chochote.

..Magufuli hakuwa options zozote zile. Kuwaambia wananchi waongeze MAOMBI amekuwa mkweli.

..Wananchi wasio na maji salama ya kunywa utawaambiaje waoshe mikono mara kwa mara, tena watumie na sabuni? It is unrealistic.
 
Top Bottom