cutelove
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 3,317
- 7,509
Zikiwa zimebaki siku 4 muda kuisha wa serikali ambao walisitisha masomo kwa shule na vyuo ili kuzuia maambukizi ya corona, bado serikali imekaa kimya hadi wazazi na wanafunzi wanabaki kuulizana kuwa huenda siku zikaongezwa au wajiandae kurudi shule.
Kuna wazazi na walezi ambao watoto wao wanasoma mikoani hivyo wanatakiwa kuwafanyia maandalizi kadha wa kadha na kuandaa usafiri mapema ili kuepuka adha za usafiri kama ilivyokuwa siku ya kufunga shule.
Wazazi, walezi, wadau na wanafunzi wanaomba tamko rasmi kama shule na vyuo vitafunguliwa jumatatu ijayo ili wazazi wawaandae watoto wao mapema ama siku zitaongezwa.
Tunaomba tamko la serikali mapema iwezekanavyo.
Sent using Jamii Forums mobile app