Janga la ajali za barabarani linatisha. Ardhi inakunywa damu ya wasafiri wajameni

Hapo ukitega li ndagu lako barabarani lazima uwe tajiri

Minoti kama yote ina miminika

Au nasema uongo nyie watu wa ule mkoa ?
Mawazo kama haya ukiyaendekeza bro utakuja ufe maskini wanao waje kukutukana pale wakiona watoto za waliotumia akili na juhudi zao wakifurahia maisha.
 
Huko sahihi kabisa, hili janga linasababishwa na uzembe wa binadamu na liko ndani ya uwezo wetu kulimaliza. Jambo la kusikitisha sana hakuna anayeonyesha kuwajibika au kuwajibishwa kutokana na haya maafa makubwa yanayotokea barabarani. Hiki kiwango cha kutojali uhai na uzima kinatisha.
Ajali SIO kazi ya Mungu it's someone Fault, barabara zetu bado sana tena sana,alama za usalama barabarani almost hakuna kabisa,hii T1 alama zake hazionekani kabisa hasa usiku, vibao vya umbali kati ya miji hakuna kabisa, ufinyu wake na magari mengi hayana sifa ya kuwa barabarani, trunks nyingi hazina kabisa tailing lights, pls waziri wangu wa mawasiliano fanya road trips ndani ya Zambia, Botswana na Namibia (usifike SA maana utaruka kichaa)angalia wenzetu walivyojenga hizi freeways zao.
 
Tatizo ni barabara vinyu, siku hizi magari mengi mapya...

Barabara zimechimbwa na kuachwa hivo hivo
... uko sahihi. Usijaribu ku-overtake milori kizembe; siku hizi yana spidi sana.
 
Watu wanakufa, wengi wanabaki vilema, watoto wanabaki yatima kwa ajali za barabarani ambazo zimekuwa nyingi sana kwenye nchi hii.

Ni kama vile watu wamekuwa sugu kwa hizi ajali sasa. Katika nchi zilizoendelea ikitokea watu 20 au 10 wamekufa mara 2 au 3 ndani ya mwaka mmoja kwa mpigo kwa chanzo kile kile kimoja basi Rais, wabunge, wanaharakati lazima wajitokeze na hata maandamano makubwa kutaka uwajibikaji. Hapa kwetu salamu za rambirambi tu zitatumwa na itakuwa kama siku kama siku nyingine baada ya ajali iliyoua watu 15 au 20.

Haya mambo matatu angalau tuanze nayo:

1. Iundwe WIZARA ya Usalama wa raia kusimamia polisi na kazi zao. Kuwachanganya polisi na RITA, uhamiaji, magereza, vitambulisho n.k kunafifisha sana usimamizi wa utendaji wao.

2. Iundwe mamlaka ya usimamizi na usalama BARABARANI inayojitegemea kwa ajili ya kupendekeza sera na sheria, kuweka miongozo na kushirikiana na polisi kusimamia leseni za wasafirashaji barabarani.

3. Mawaziri wa uchukuzi na mambo ya ndani kwa sasa wawajibishwe mpaka hayo mawili hapo juu yatakapofanyiwa kazi. Hawa mawaziri wawili kama hawawezi kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu kutatua janga la ajali basi hawafai, hawatoshi na hivyo waondolewe haraka na wakija wengine wakishimdwa nao waondolewe pia.

Maisha yetu raia yanahitaji kupewa uthamani stahiki na wale wanaolipwa kwa kodi zetu kwa kazi hiyo kuhakikisha yanakuwa salama muda wote.
Kuna uwekezaji mkubwa unafanywa siyo kwa lengo la kudhibiti ajali lengo ni makusanyo na 10% kwenye procurement
 
Tatizo sio miundo mbinu wala nini kwanini zamani kulikuwa hakuna barabara nzuri kama hizi leo ila ajari hazikuwa kama sasa, Tatizo ni ulimbukeni wa vyombo vya usafiri wengine mafunzo duni then wanajifanya madereva konk lakini pia abiria kutokemea miendo kasi ya madereva wao! watu wapewe elimu sana la sivyo ardhi iendelee kunywa tu!
... nakubaliana na wewe ulimbukeni na kutozingatia sheria ni sehemu ya tatizo ila miundombinu pia inachangia. Kwa mfano, zamani hapakuwa na bodaboda wala babajaji, etc.

Miundombinu iliyopo haikuzingatia uwepo wa hivyo vyombo. Mfano rahisi ni mijini na sehemu zenye vimji; je, bodaboda kwao ni ruksa kupita katikati, kushoto, kulia kwa magari? Kulitakiwa kuwe na miundombinu ya ku-accommodate hivyo vyombo.
 
Sielewei kwa nini serikali wanaruhusu Bajaji hadi barabara kuu. Mkoa kama Mbeya bajaji zimejaa barabara kuu ya Mbeya-Tunduma zinapishana na malori ya makubwa ya mizigo, na mabasi ya abiria yaliyo kasi sana huku barabara yenyewe iko na matuta kama msuko wa twende kilioni!

... kichekesho ni pamoja na Dar es Salaam. Waliondoa daladala na vipanya kuingia katikati ya mji kwa kisingizio vinasababisha foleni na capacity yake ni ndogo.

Badala yake nafasi zao zimekuwa replaced na bajaji na bodaboda huku watendaji wakiangalia tu! Unajiuliza kati ya Coaster inayobeba abiria zaidi ya 30 na bajaji inayobeba abiria 3 ni ipi ilipaswa kutoingia mjini kwa kisingizio cha capacity?

Bajaji na bodaboda zimehanikiza barabarani katikati ya jiji hadi kero. Popote kwao ni kituo kushusha, kupakia, kugeuza, etc. Overtaking na chomekeachomekea za kijinga.
 
Sielewei kwa nini serikali wanaruhusu Bajaji hadi barabara kuu. Mkoa kama Mbeya bajaji zimejaa barabara kuu ya Mbeya-Tunduma zinapishana na malori ya makubwa ya mizigo, na mabasi ya abiria yaliyo kasi sana huku barabara yenyewe iko na matuta kama msuko wa twende kilioni!
Suluhisho ni reli SGR ikikamilika mpaka Isaka malori yatapungua kiasi ila itategemea utashi wa kiongozi mkuu wa nchi vinginevyo itakua km TAZARA ilivokufa kifo cha Mende
 
Tatizo sio miundo mbinu wala nini kwanini zamani kulikuwa hakuna barabara nzuri kama hizi leo ila ajari hazikuwa kama sasa, Tatizo ni ulimbukeni wa vyombo vya usafiri wengine mafunzo duni then wanajifanya madereva konk lakini pia abiria kutokemea miendo kasi ya madereva wao! watu wapewe elimu sana la sivyo ardhi iendelee kunywa tu!
Umeongea ukweli

Madereva hawasikii,abiria nao

Wako kama mazombie,dereva anaendesha speed ya ajabu abiria
Wame nyuti tuuu

Mwisho wa siku wanachinjwa

Ova
 
Wakati tunafikiria SGR itakayofika Isaka miaka 10 au 20 ijayo tufikirie kwanza waliokufa jana , watakaokufa leo, kesho na keshokutwa kwenye ajali za barabarani na pia wewe ukiwa mhanga mmojawapo wakati tunasuburia SGR ambayo haijulikani itamalazika mwaka upi.
Suluhisho ni reli SGR ikikamilika mpaka Isaka malori yatapungua kiasi ila itategemea utashi wa kiongozi mkuu wa nchi vinginevyo itakua km TAZARA ilivokufa kifo cha Mende
 
Hapa Arusha maeneo ya uswahilini wiki iliyopita waligongwa watu watatu wa familia moja wakawa kama chapati alafu leo tena mbele yake barabara ya east Africa nasikia wengine Tena watatu wamegongwa tena wakafa 🤔
 
Hivi hawa wakipatwa na ajali kuna kulaumu kweli....
Acha watu wazidi kujifanya vichaa huku wakifa kama inzi
Yoda

Ova
 
Wee naye usitutishe bwana, ukiona mtu kafa ujue muda wake ndo umeishia hapo, kila nchi ina udhaifu wake na Aina yake ya vifo vya watu wake
 
Kichwa kama tikiti maji
Wee naye usitutishe bwana, ukiona mtu kafa ujue muda wake ndo umeishia hapo, kila nchi ina udhaifu wake na Aina yake ya vifo vya watu wake
 
Ukaguz barabarani wahusika wakazane.....magari mengi ni mabovu Yako huru tu barabarani.Tuna watoto jaman
 
Kuna sehemu za barabara matukio ya ajali huwa yanajirudia rudia mara nyingi sana lakini wahusika hata hawajui au hawakumbuki kuweka nguvu za ziada maeneo kama hayo!
Hapa Arusha maeneo ya uswahilini wiki iliyopita waligongwa watu watatu wa familia moja wakawa kama chapati alafu leo tena mbele yake barabara ya east Africa nasikia wengine Tena watatu wamegongwa tena wakafa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom