Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Ndugu zangu,
Awali ya yote naomba niseme naijua kiasi fulani historia ya taifa hii. Kwa mtazamo wangu, kuna 'legacy tricks' zinazotoka toka kipindi cha ujamaa ambazo tumezishikilia, hasa systems za nchi hii, kwa kuwa kwa mtazamo wao zilifanya kazi huko nyuma kwa hiyo hawataki kuziacha.
Hii tabia ya kutaka viongozi wawe maarufu kuliko mtu mwingine yoyote inatuharibia sana. Kwa mtazamo wao katika kila ngazi, kiongozi ndiyo wanataka awe maarufu na anayekubalika zaidi. Matokeo yake, mtu mwingine yoyote anayechipuka anayetaka kuwaibia umaarufu wao wanamuona ni tishio kwa usalama wa nchi. Ndiyo maana tunaona viongozi wanashindana na madogo katika majukwaa ya muziki, katika vyombo vya habari, katika michezo, katika mitandao ya kijamii, nk. Hatujui nafasi ya kila mmoja wetu katika jamii hii ni ipi.
Nimeileta hii mada maana mnaweza kuiona ni ndogo lakini inatuharibia katika sekta nyingi sana kuanzia elimu, uhuru wa vyombo vya habari na hadi katika sanaa na michezo. Hizi sekta hazitakuja kukua kamwe kama hili suala halitarekebishwa na tukaachana na dhana hii potofu.