Jane: Nini kilichomfikisha hapo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jane: Nini kilichomfikisha hapo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 18, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  YUMKINI wengi wanaomuona Jane Sosovele katika maeneo ya Posta Mpya na mengine ya jirani hudhani kwamba ugonjwa wake wa akili alionao haukumpa fursa ya kujua kusoma na kuandika.

  Wanapomuaona akiongea maneno yasiyokuwa na mbele wala nyuma, akiwa amebeba mfuko wa plastiki ambao ndani yake huwa na makaratasi ya kuokoteza, huku akiomba chochote kwa wapita njia huamini kwamba hana analolijua.

  Hao wamekosea. Mwanamke huyu ni msomi aliyekuwa tegemeo kubwa katika fani ya mawasiliano ya simu katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

  "Jane Sosovele alikuwa mtumishi wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania kuanzia Julai 31, 1987 katika nafasi ya 'Telecomms Controller' baada ya kuhitimu Shahada ya Bsc General ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam... Kufuatia kugawanywa kwa Shirika la Posta na Simu Tanzania na kuundwa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Shirika la Posta Tanzania (TPC) mwaka 1994, aliendelea na utumishi katika kampuni ya Simu Tanzania hadi Julai, Mosi 1998 alipostaafishwa kwa sababu za kiafya," anasema Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa TTCL, Juvenal Utafu.

  Pengine hiyo ndiyo sababu ya Jane kupendelea kukaa maeneo ya hayo ya Posta Mpya kwani ni sehemu inayomrejeshea kumbukumbu njema za maisha yake ya zamani ambayo kuyapata tena ni kudra za Mungu.

  Hata unapobahatika kukaa naye utagundua kuwa ni msomi 'aliyepata ajali' kwani mbali ya kutumia misamiati mingi ya Kiingereza, anazungumzia mambo kadha wa kadha ya kimataifa hata kama ni katika njia ambazo hazieleweki vyema. Kwa mfano, mara kwa mara hupendelea kusema wakuu wa posta wapo katika mkutano mkuu Geneva (Uswisi), safari yake ya Lebanon imekaribia, magari yake yamepotea bandarini au akisema, anatunza risiti ili akalipwe pesa za vikao.

  Ni vigumu kufanya naye mahojiano kwani anachanganya mambo. Lakini nilibahatika kuzungumza naye na alinieleza yafuatayo:
  “Ni vigumu kutatua tatizo ambalo limejitokeza kwa muda mfupi kwani mabadiliko ya mume wangu yalikuwa ya ghafla mno,” anasema na ghafla anachanganya habari za risiti.

  Anaendelea: “Nilipokuwa Ujerumani nilinunua magari matatu, makochi na friji lakini sijui vilipotelea wapi, wanasema vimeibiwa bandarini, nilikuja na zawadi nyingi za watoto sijui kama walizichukua!”

  Mmoja wa watu wanaomfahamu kwa karibu mwanamke huyo anasema: “Huwezi kuamini, Jane ambaye wengi humpita hapa na kumdharau wakiwa hawana habari naye, kabla ya kuvurugika akili alikuwa ni Injinia.”

  Anasema kama si kupata matatizo hayo ya akili Jane angekuwa miongoni mwa watu wenye nyadhifa mkubwa katika tasnia ya sayansi kwa sababu anasema alikuwa mwerevu na mchapakazi hodari na makini kwelikweli.

  Kuna simulizi nyingi zinazotolewa juu ya ni sababu gani iliyomfikisha mwanamke huyo katika hali hiyo. Inayotajwa zaidi ni mtikisiko wa ndoa yake mnamo mwaka 1997.

  “Jane ni msomi huyu! Usimuone hivi. Ameshatembelea nchi nyingi tu duniani lakini mapenzi ndiyo yaliyomfanya awe hivi, mume wake ambaye ni Profesa wa hapo Mlimani ndiye aliyemsababishia matatizo hayo,” anadai mwanamke mmoja ambaye alikuwa akifanya naye kazi bila kutaka kutaja jina lake na kuongeza:

  "Inasikitisha kuona mtu ambaye angekuwa na maisha mazuri lakini sasa hivi ana ombaomba, akiwa hajui familia yake iko wapi na wala hajielewi! Lakini yote hayo yamesababishwa na mapenzi ambayo yamekuwa yakitajwa kila siku kuwa ni sumu."

  Ndugu wa Jane aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mariamu, anasema mama huyo wa watoto wawili akiwa Chuo Kikuu, mwaka 1984 alibeba ujauzito wa mtoto wake wa kwanza Daudi kabla ya kufunga ndoa mwaka 1986. Mwaka mmoja baadaye aliamua kumfuata mumewe Ujerumani pamoja na kusoma.

  Safari yake ya Ujerumani ilimgharimu kwani kwa mujibu wa taarifa ya Utafu, aliomba likizo ya bila malipo ambayo ilikataliwa na mwenyewe kuamua kuondoka bila kibali hivyo kufutwa kazi Januari, 1988.

  "Aliomba likizo bila malipo baada ya miezi mitatu tu ya ajira kwa ajili ya kwenda Ujerumani kuishi na mumewe ambaye alipata nafasi ya kusoma katika iliyokuwa Jamhuri ya Ujerumani Magharibi hapo mwaka 1987 hadi 1988 lakini likizo hiyo ilikataliwa kwa sababu kanuni za utumishi hazikuruhusu likizo bila malipo kwa mtumishi aliyekuwa bado kwenye kipindi cha majaribio."

  Mama Mariamu anasema wakati ndugu yake huyo akiwa safarini Ujerumani alikuwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili, Ibrahim na matatizo ya ndoa yalianzia huko kwani aliporudi hakuwa na amani tena.

  Baada ya kurejea, Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa TTCL, anasema Jane aliomba tena kuendelea na kazi... "Aliajiriwa upya kuanzia Januari 23, 1989 kwa vile sifa yake kielimu ilikuwa inahitajika ndani ya shirika."

  Hata hivyo, Utafu anasema: "Tabia yake ilianza kubadilika na kuwa isiyokuwa ya kawaida kwa kile alichodai kwamba ana matatizo yake binafsi ya kifamilia na alionyesha wazi kwamba amechanganyikiwa. Hatua zilichukuliwa na alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili wakati huo kwa muda mrefu bila mafanikio. Kwa ushauri wa jopo la madaktari, alistaafishwa kazi kwa ajili ya ugonjwa Julai Mosi, 1998."

  Kwa upande wake, Mama Mariamu anadai kuwa baada ya kuona mke wake amechanganyikiwa, mumewe alimrudisha kwa dada yake Mabibo ambako ndipo alipomuolea.

  “Tulishangazwa na kitendo cha Sosovele kumrudisha mama Ibrahim (Jane) akiwa amechanganyikiwa tena bila kufafanua chochote na wala kufuatilia afya ya mke wake na mpaka leo amekuwa hana ukaribu kabisa na sisi hatuna mawasiliano naye hiyo inatuhakikishia kuwa yeye ndiyo chanzo cha yote,” anasema.

  Anasema anafahamu kwamba mume huyo yupo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini hajui anakoishi na watoto wa ndugu yake.

  Akizungumzia madai hayo, mume wa Jane, Profesa Hussein Sosovele anasema: “Mimi na Jane tumeachana muda mrefu. Mambo yake na yangu yaliisha miaka zaidi ya 10 iliyopita kwa hiyo habari zake sizijui.”

  Profesa Sosovele anakiri kwamba yeye na Jane walipitia matatizo ya ndoa na akamrudisha kwa wazazi wake, tofauti na madai ya Mama Mariamu, profesa huyo anadai kwamba wakati wanaachana mtalaka wake alikuwa hana tatizo lolote la akili.

  Anasema hata alipopata taarifa juu ya matatizo yaliyomsibu, alijaribu kumsaidia lakini hakupata ushirikiano kutoka kwa ndugu zake.
   
 2. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  Incredibly touching and sad episode....
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha!
   
 4. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  inasikitisha! Mungu amuepushie na mabaya ya Dunia hii.
   
 5. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  kama kuna ndugu yake ananisikia hapa, mchukue Jane kama livyo, mpeleke pale Kawe kwa gwajima, akili zake zinaenda kurudi kwa maombi tu. kuna siku moja Yesu alikuwa anapita akamkuta kichaa aliyekuwa ameshindikana, alikuwa na mashetani mengi kiasi cha kuitwa jeshi. aliyatoa yale mashetani, yule kichaa lipona akaenda mjini na kuendelea maisha. yale aliyoyafanya Yesu yanafanyika hata leo hii, Yesu alisema, yeyote aniaminiye mimi kazi zile nizifanyazo yeye pia atazifanya, naam, na kubwa kuliko zile. hivyo kama Yesu aliponya, nasi kwa Jina lake twaweza kuponya, kama alifufua, kama aliponya machizi hata sisi kwa Jina lake tunaweza kufanya hivyo, naam na mambo makubwakuliko hata yale ambayo Yesu aliyafanya, sisi tutayafanya. Neno la Mungu li hai, linatenda kazi, halitapita kamwe hata yote yatimie...

  upande mwingine, nyie ambao hamjaokoka, nawapa ushauri, HAMPO SALAMA. wakati wowote mnaweza kuwa machizi, vichaa wagonjwa etc. wakati mwingine inaweza kuwa ni kwasababu ya visa mtaani penu, wakati mwingine ni kwasababu ya madawa ya kazi mnayochukua kwa mganga wa kienyeji yaani mahirizi ya kazi hayo, wakati mwingine mme wako au mke wako anataka kukutoa wewe kafara, wakati mwingine mmegombana na mmeo au mkeo na yeye anakufanya jambo la ajabu ambalo anaju ahautakuja upone hata utembee wapi. duniani kuna mengi.

  Juzi juma tano nilikuwa nimeenda kusali pale kwa gwajima jioni, akaamurisha watu wale ambao walishawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji ili wakawadhuru wenzao kwasababu ya visa etc, waje mbele ili watubu na kuombewa....ujue pale watu wapya wanakuja kila siku...namba ya watu waliotoka mbele was alarming...wengine wamekaa karibu nawe huamini kama lishawai kwenda kwa mganga ili akamdhuru mtu mwingine...wengine wamefanya hivyo kwasababu ya wivu tu wa maisha mazuri ya jirani yake, wengine walikuwa wanagombania mwanamke...wengine nyumba ndogo imekuchanganya akili ili wamchukue bwanako etc...ni wengi mno....pale kanisa la gwajima, kila siku watu wapya wanakuja...walioshindwa maisha wanakuja pale, waliokuwa wachawi uchawi wao ukawarudi wanakuja pale, waliokuwa wabaya wanakuja pale wanatubu, Mungu anawasamehe na wanaendelea na maisha mapya ndani ya Kristo, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya...

  hata itakuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya. HIVYO KAMA KUNA MTU HAPO, MCHUKUENI, MLETENI PALE, NAKWAMBIA ATARUDI NA AKILI ZAKE, NA HUYO ALIYEMLOGA, ALIYEMCHUMOA ETC, ANAWEZA KUHARIBIKIWA MAMBO YAKE. how? wakati mwingine, mchawi anaweza kukuchomoa wewe wa ndani halafu ukabaki kopo ndani yake akaweka jini..so sio wewe bali ni jini ndani yako...na wewe unavyokuwa chizi, unapopata matatizo yeye mambo yake ndo yanazidi kuwa mazuri,..so ukipona yeye ndo anaharibikiwa...beware, hii ndo dunia.
   
 6. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Omg!
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana.Ndoa zina mengi wajamini. Ngugu yangu Hute si kila binadamu anaechanganyikwa anakuwa kalogwa,kaonewa wivu au ni mapepo.Ndo maana siku hizi makanisa mengi yanateka waumini kwa miujiza ya kutoa mapepo wengine mashetani majini nk huku wakipiga kelele. Kisa cha huyu mama ni sychological effect inatokea pale mtu unapokuwa na mambo mengi yanayokukwaza na kama binadamu akili inashindwa kuhimili, Hata computer huwa inajamu hivo elewa ubongo nao unafanya kazi kama computer.Lau angepata ushauri mapema kabla hajachanganyikiwa angesaidika tatizo nadhani linakuja mtu anapokuwa na tatzio kubwa analibeba mwenyewe bila kumshirikisha mtu madhara yake ndo kama hayo.Huko mjini kuna vichaa wengi sana mbona basi hatuoni hao wachungaji wakienda kuwaombea? Yesu hakuwa na kanisa alikuwa anazunguka mitaani na kuponya watu hivo hivo basi na wachungaji wa leo wafanye hivo.Sikatai kuwa akiombewa atapona yawezekana akapona kwa imani hii ni kwa kufunga na kusali. Wataalamu wa saikolojia watufafanulie zaidi hili tatizo na jinsi ya kumsadia yaonekana anaweza kukumbuka matukio yalopita atasaidika.
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  inauma balaaa
   
 9. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mola amponye na matatizo yanayomsibu
   
 10. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ndoa ndoano inasikitisha sana binadamu wengine huwa hawawezi beba mikiki mikiki ya maisha lazima kichwa italipuka tumetofautiana sana jamani
   
 11. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Aisee, Inasikitisha sana!
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Sad story
  inasikitisha sana
  Maisha yanapoteza thamani muda wowote

  NB:-Mola mjalie mja wako afya yake tena. Amen
   
 13. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Terribo! Hivi jukumu la serikali yetu linaishia wapi?
   
 14. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  una picha yake uweke?
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  kusaini mikataba mbalimbali!
   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  jane ttcl.jpg
   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
 19. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
 20. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  wanaume sisi!!!!!!!
   
Loading...