Jane Goodall na jinsi asivyotambulika hapa nchini pamoja na kazi zake alizofanya

Huyu Bibi nilikuwa nikimuona wa Kawaida nikiwa mdogo Tukiishi jirani,sikuwa nikijua kuwa ni Icon kutokana na anavyoheshimika duniani.
mbona km vile alikufa kwa accident ya ndege zamani?
aliingilia anga za PK wakamtengeneza.
Yupo hai na huwa anakuwa nchini na kwao Uingereza. Kuhusu mambo ya HIV ndo leo nasikia.
 
Jane Goodall, ni mwanamama ambaye amweza kutangaza nchi yetu kwa utafiti wake wa Sokwe tangu mwaka 1960. Amefanya hii kazi bila kupumzika na sasa dunia nzima inatambua kazi yake na kuiheshimu.
Naandika hivi baada ya kuona documentary yake juzi kwenye BBC Earth na kuona kuwa serikali yetu ya Tanzania kama imemtambua haijawahi kumtangaza kama watu mashuhuri walioletea sifa nchi yetu. Yawezekana sababu ya rangi yake au sababu hajawahi fungamana na siasa. Nimecopy jinsi alivyoanza na anavyoendelea kutetea maisha ya viumbe hawa na mazingira kwa ujumla. Nimeweka na video yake hapo chini.
Equipped with little more than a notebook, binoculars, and her fascination with wildlife, Jane Goodall braved a realm of unknowns to give the world a remarkable window into humankind’s closest living relatives. Through nearly 60 years of groundbreaking work, Dr. Jane Goodall has not only shown us the urgent need to protect chimpanzees from extinction; she has also redefined species conservation to include the needs of local people and the environment. Today she travels the world, speaking about the threats facing chimpanzees and environmental crises, urging each of us to take action on behalf of all living things and planet we share.

Huyu mdada (akiwa bado kijana) aliwahi kutekwa na watu wasiojulikana ambao walidai pesa ili aachiwe, Rais Nyerere (wakati huo) aliwagomea watekaji na wakamwachia, hata hivyo sisi hatuthamini mambo hayo ila tunathamini siasa hasa ukiwa mwanaccm.
Amekulia kwenye msitu wa Gombe Kigoma akiwa mwanamke pekee mzungu na amezeekea hukohuko, mambo yote ya mjini hakuwa na habari nayo.
 
Kuna Mzee mmoja nadhani anakaribia 80 sasa hivi ni ex employee wa USAID, UN(WHO), na mashirika kadhaa yanayohusiana na medical researches ikiwemo NIMR ya hapa bongo akikuelezea habari za huyo mama wa kizungu wala hutataka awe anaendelea kuishi duniani maana ni shetani haswaa aliyekamilika

Mzee ni kama ana secret file la Jane Goodall na kwakifupi anamuhusianisha na kuenea kwa AIDS na UKIMWI Africa kwa makusudi na agenda zilizojificha sana

Mzee ambaye ni Doctor by professional anaongea kwa facts and evidences ambazo zitakuacha umeduwaa, but hua yuko so reserved. Nilizoeana nae sababu mtoto wake ni business partner wangu
Mkuu unaweza kupata wasaa, utusimulie kidogo visa vya huyu mama?
 
Huyu mdada (akiwa bado kijana) aliwahi kutekwa na watu wasiojulikana ambao walidai pesa ili aachiwe, Rais Nyerere (wakati huo) aliwagomea watekaji na wakamwachia, hata hivyo sisi hatuthamini mambo hayo ila tunathamini siasa hasa ukiwa mwanaccm.
Ni kweli huyu mama angekuwa alishajihusisha na siasa basi kila mtu angemfahamu. Naona anazushiwa kuleta HIV wakati yeye si daktari .It is a pity that watu wanasikiliza maneno ya mitaani.
 
Hata kama stori hii itakuwa ya kweli nani anaweza kumhakikishia ulinzi wake na familia yake ?na amwamini nani kwenye jamii ya watu neno mzungu wanatoa z na kuanza kuabudu? nadhani hata kumwambia huyo jamaa kajitahidi sana....wakati wa vita baridi kulikuwa na tuhuma za wamerikani kujaribu kutengeza super soldier kwa kutumia vinasaba vya sokwe huko congo kwa techolojia ya sasa ya GENE EDITING si kitu cha ajabu kufanyika angalia link hii hapa halafu unganisha na mradi wa mbu uliokuwa ukiendelea nyuma ya hospitali muhimbili miaka miaka ya hivi karibuni hhttps://www.youtube.com/watch?v=OI_OhvOumT0
Mkuu iweke tena hiyo link
 
Ni kweli huyu mama angekuwa alishajihusisha na siasa basi kila mtu angemfahamu. Naona anazushiwa kuleta HIV wakati yeye si daktari .It is a pity that watu wanasikiliza maneno ya mitaani.
Inaonekana una nufaika nae tena personally kiasi kwamba hutaki kusikia habari mbaya kumuhusu yeye?
 
Wazungu baada ya kukamilisha kufanya uhuni walio mtuma sasa wanaanza kumpongeza, sasa nashindwa kuelewa kama ni kweli kuhusu huyu mama kutufanyia uhuni kwa mwamvuli wa kulinda sokwe, usalama wa taifa wanakuwa wanafanya nn sasa?
Vipi mkuu unaweza kufunguka kidogo? Naskia pale hifadhi ya Gombe kuna laboratory ya SIRI.
 
Inaonekana una nufaika nae tena personally kiasi kwamba hutaki kusikia habari mbaya kumuhusu yeye?
Sijawahi kutana naye zaidi ya kumwona kwenye vyombo vya habari. Watu wanapomlaani mchonga je, wangapi walifaidi utawala wake? Watu wanapomlaani Ghadaffi wangapi walifaidi kwake? Huyu bado yupo hai na kama angekuwa amefanya hayo mnayoyasema, serikali au UN ingemshtaki. Hata wewe unaweza fungua mashtaka kumhusu yupo hai bado.
 
Kisa alikuwa hana muda na mapenzi ambavyo huenda yangempa mimba zisizotarajiwa huko msituni na utafiti ungeishia hapo.
For your information, huyu mama alikuwa ameolewa. Mme wake ndo alikuwa mpiga picha mashuhuri wa kwenye mbuga za Ngorongoro na serengeti. Waliachana sababu mama alikuwa commited kwenye utafiti wake na baba aliwaza kupiga picha lakini ndo alikuwa na yeye wakati wanaanza utafiti. Walijaliwa watoto wawili. You can google.
 
Sijawahi kutana naye zaidi ya kumwona kwenye vyombo vya habari. Watu wanapomlaani mchonga je, wangapi walifaidi utawala wake? Watu wanapomlaani Ghadaffi wangapi walifaidi kwake? Huyu bado yupo hai na kama angekuwa amefanya hayo mnayoyasema, serikali au UN ingemshtaki. Hata wewe unaweza fungua mashtaka kumhusu yupo hai bado.

Kwanini hutaki kusikia baya lolote alilofanya?
Unadhani kwanini watu wanamzushia ubaya?
Unadhani UN wanaumakini linapokuja suala la kuumia muafrika zaidi ya maslahi yao?
Kwanini serikali hampi umaalumu wowote huyo mama?
 
Nipe majibu ya hayo maswali basi!
 
Jane Goodall, ni mwanamama ambaye amweza kutangaza nchi yetu kwa utafiti wake wa Sokwe tangu mwaka 1960. Amefanya hii kazi bila kupumzika na sasa dunia nzima inatambua kazi yake na kuiheshimu.

Naandika hivi baada ya kuona documentary yake juzi kwenye BBC Earth na kuona kuwa serikali yetu ya Tanzania kama imemtambua haijawahi kumtangaza kama watu mashuhuri walioletea sifa nchi yetu. Yawezekana sababu ya rangi yake au sababu hajawahi fungamana na siasa. Nimecopy jinsi alivyoanza na anavyoendelea kutetea maisha ya viumbe hawa na mazingira kwa ujumla. Nimeweka na video yake hapo chini.

Equipped with little more than a notebook, binoculars, and her fascination with wildlife, Jane Goodall braved a realm of unknowns to give the world a remarkable window into humankind’s closest living relatives. Through nearly 60 years of groundbreaking work, Dr. Jane Goodall has not only shown us the urgent need to protect chimpanzees from extinction; she has also redefined species conservation to include the needs of local people and the environment. Today she travels the world, speaking about the threats facing chimpanzees and environmental crises, urging each of us to take action on behalf of all living things and planet we share.

Labda wewe ndiyo kwanza umemfahamu, mbona tunamtambua siku nyingi sana...

HABARI ZETURAIS KIKWETE AKUTANA NA MHIFADHI WA SOKWE DKT.JANE GOODALL

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza mhifadhi wa Sokwe wa kimataifa Dkt.Jane Goodall wakati mhifadhi huyo alipomtembelea Rais Ikulu na kumwelezea kazi zake mbalimbali za uhifadhi nchini.Dkt.Goodall anajihusisha na uhifadhi wa Sokwe katika hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma na kazi yake imeipatia Tanzania umaarufu mkubwa Duniani.Dkt. Goodall ni mwanzilishi wa taasisi ya Jane Goodall Institute inayojihusisha na uhifadhi wa Sokwe. Picha na Freddy Maro
WWW.HAKILEO.BLOGSPOT.COM
 
Jane Goodall, ni mwanamama ambaye amweza kutangaza nchi yetu kwa utafiti wake wa Sokwe tangu mwaka 1960. Amefanya hii kazi bila kupumzika na sasa dunia nzima inatambua kazi yake na kuiheshimu.

Naandika hivi baada ya kuona documentary yake juzi kwenye BBC Earth na kuona kuwa serikali yetu ya Tanzania kama imemtambua haijawahi kumtangaza kama watu mashuhuri walioletea sifa nchi yetu. Yawezekana sababu ya rangi yake au sababu hajawahi fungamana na siasa. Nimecopy jinsi alivyoanza na anavyoendelea kutetea maisha ya viumbe hawa na mazingira kwa ujumla. Nimeweka na video yake hapo chini.

Equipped with little more than a notebook, binoculars, and her fascination with wildlife, Jane Goodall braved a realm of unknowns to give the world a remarkable window into humankind’s closest living relatives. Through nearly 60 years of groundbreaking work, Dr. Jane Goodall has not only shown us the urgent need to protect chimpanzees from extinction; she has also redefined species conservation to include the needs of local people and the environment. Today she travels the world, speaking about the threats facing chimpanzees and environmental crises, urging each of us to take action on behalf of all living things and planet we share.

Labda wewe tu ulikuwa humfahamu.mboa huyo bibi anafahamika sana na anatukuzwa sana Tamzania...
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL

2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na akiwa kwenye kikao na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
8
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.
12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu kinachomuelezea Jane Goodall na miaka 50 alioishi Gombe kutoka kwa Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.
19
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan
Chanzo: http://www.mtaakwamtaa.co.tz/2017/07/makamu-wa-rais-akutana-na-jane-goodall.html?m=1
 
Na wewe weka yako ya rohoni tujue kisa cha huyu mama kutotambulika. Kama ni hiyo issue naomba uiseme vizuri ili namimi na wana jamvi tuijue?
Mbona anatambulika sana tu, labda wewe ndiyo ulikuwa humtambui...

TANAPA YAMPATIA DK JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA
Jul 14, 2017
IMG_0099.JPG
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi Dk. Jane Goodall tuzo maalumu kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa miaka 60 wa maisha ya Sokwe pamoja na uhifadhi wa wanyama wengine kwenye hifadhi ya Gombe, mkoani Kigoma katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Tuzo hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa). Habari zaidi zitaletwa punde.

Na Richard Mwaikenda
Jane ambaye ni raia wa Uingereza alianza utafiti katika Hifadhi ya Gombe mnamo miaka ya 60 akiwa na umri wa miaka 26.

Katika utafiti wake amegundua mambo mengi ikiwemo jinsi Sokwe wanavyojitambua, kuwa na hisia na jinsi wanavyoishi kwa ushirikiano kama walivyo binadamu.

Akizungumza katika hafla hiyo jane anasema wakati anaanza kufanya utafiti ilikuwa vigumu Sokwe hao kumkaribia kwani walikuwa wanamuogopa na ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kumuona mtu mweupe, lakini alifanya jitihada hadi wakamzoea na kuanza kumsogelea na kumuona mtu wao wa karibu.

Anasema alitumia mbinu mbalimbali kama vile kuwapatia ndizi na vyakula vingine hadi wakamzoea.

Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Utalii katikati ya jiji la Dar es Salaam, viongozi na wageni waalikwa walipata wasaa wa kuangalia picha mbalimbali za matukio ya sokwe wakiwa na Jane Goodall.

Katika utafiti wake amefanikiwa kuanzisha chuo na kutunga vitabu pamoja na video zinazoelezea maisha yake na Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma.

Katika hafla hiyo walihudhuria Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali George Waitara, Mwanasiasa Mkongwe, Getrude Mongela, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Goodall, Lembeli, Balozi wa Uingereza nchini, mabalozi mbalimbali pamoja na waalikwa.
Dk. Jane akikabidhiwa cheti cha kutambua mchange wake kwa Tanzania kwa kuhifadhi Sokwe na wanayama wengine

Jane akipatiwa pia zawadi ya kinyago cha Sokwe

Jane akikabidhiwa picha ya Sokwe

Mama Mongela akimvisha Jane zawadi ya vitenge

Dk Jane akitoa maelezo kuhusu maisha ya Sokwe

Waziri Maghembe akipata maelezo kuhusu maisha ya Sokwe yalivyo

Wasanii wa Tanapa wakitumbuiza kwa wimbo

Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Mjeshi Mstaafu, Jenerali Waitara akitoa shukrani nyingi kwa Dk Jane kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuiletea Tanzania sifa lukuki duniani

Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini wakati Waziri Maghembe akihutubia katika hafla hiyo, ambapo alisema kuwa Dk. Jane ambaye wakati anaaza utafiti yeye alikuwa darasa la pili, lakini utafiti wake umeiletea sifa kubwa Tanzania na utakuwa ni urithi wa kipekee maishani

Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini

Profesa Magembe akihutubia katika hafla hiyo ya kumpatia tuzo Dk. Jane

Baadhi ya mabalozi waliohudhuria hafla hiyo

Dk Jane akielezea historia yake na jinsi alivyofanikiwa kufanya utafiti huo wa sokwe

Lembeli akitoa neno la shukrani

Jane akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi waliohudhuria hafla yake pamoaja na viongozi mbalimbali

Jane akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari baada hafla kumalizika

POSTED BY: BASHIR NKOROMO AT 7/14/2017
 
Back
Top Bottom